Ndugu zangu wapendwa leo nataka kusema kitu ambacho kimekuwa kikinikera sana. Ni kuhusu makabila yetu, mnajua ya kwamba nchi yetu Tanzania ni nchi pekee yenye makabila 129-130? Nasikitika sana kuona/kusikia baadhi ya watu huwa wanayakana makabila yao.Kwa mfano utasikia mtu anasema mimi si mngoni, mimi siwezi kingoni kwanini kukataa uwewe? Uasili wako? KWANINI???
Nawaambia ukweli binafsi najivuna sana kuwa MNGONI na nilipenda kabila langu pia mila zake. Nachukua nafasi hii kumshukuru kaka Matondo kwa utundu wake ingia hapa ufaidi uhundo kwa wale/yule ambaye hajajua na pia wale waliojua si mbaya kujikumbusha. Mimi binafsi nimefaidi na ninaendelea kufaidi kwa mfano gonga hapa yaaani mpaka raha!!!!