Katika jamii yetu wengi wanadharu sana micezo ya watoto. Wanaona ni kupoteza mida tu lakini tukumbuka kwamba michezo yote wafanyayo watoto inachangia sana ukomavu wa ubongo wao maana pale hawachezi tu wanajifunza kitu pia. Kwa mfano katika michezo mingi ya watoto kuna kuhesabu kwingi sana, hapa tayari anajifunza kitu...tuwape nafasi watoto kuwa watoto na pia kama wazazi tujaribu kuwa pamoja nao na kushiriki baadhi ya michezo.
CHUKUA DAKIKA TU ANGALIA HII VIDEO HAPA CHINI ......
UJUMBE:- WAZAZI/WALEZI WATOTO WETU WANATUHITAJI SANA TUTENGE MUDA KWA AJILI YAO. TUSIWASAHAU NI JUKUMU LETU.
Showing posts with label watoto. Show all posts
Showing posts with label watoto. Show all posts
Monday, February 27, 2017
Tuesday, February 2, 2016
TUPENDANE, TUSAIDIANE MAANA SISI SOTE NI NDUGU....
Watoto wengi wanatamani kuishi maisha ya furaha na upendo ebu tazama wanavyoishi watoto hawa katika mazingira magumu tuishi kwa kufikiriana kusaidiana. Ebu chukua dakika chache kusikiliza ujumbe wa wimbo huu wa Ben Paul na halafu linganisha na picha hii ya hawa watoto.
TULICHO NACHO TUGAWANE TUACHE UBAHILI SISI SOTE NI NDUGU NA BABA YETU NI MMOJA. UPENDO DAIMA!
Thursday, May 15, 2014
PICHA YA WIKI:- SIJUI HAPA WANASUBIRI WATEJA AU....
...labda ni mashindano ya pikipiki..ila huyo mwenye sweta nyekundu sijui vipi na hilo panga?? Watoto bwana wana ubunifu sana..Nimependa sana hii:-) PAMOJA DAIMA!!
Saturday, April 12, 2014
MAUA MAZURI YAPENDEZA...NAPENDA SANA MAUA NIMEPATA HILI KAMA ZAWADI NA....:-)
NIKAONA NILIIMBIE NA HUU WIMBO TULIOKUWA TUKIIMBA ENZI ZILEEEE je nawe unakumbuka kama hukumbuki basi ni hivi kuimba!!!
1. Maua mazuri yapendeza x 2
Ukiyatazama utachekelea
Hakuna mmoja asiyeyapenda x 2
Kwa kutaka kuimba bila kukosea basi fuata hii hapa:-)
Au pia tusiwasahau na watoto, si mnakumbuka na huu wimbo haya wazazi waimbieni watoto wenu kwa raha zote ni kama vile umsomeapo/msimuliapo hadithi :-
2.Mtoto msafi apendeza x 2
Ukimtazama utachekelea
Hakuna mmoja asiyependeza x 2
3. Mtoto mtii apendeza x 2
Ukimtazama utachekelea
Hakuna mmoja asiyempenda x 2
JUMAMOSI IWE YENYE UPENDO, FURAHA JUU YA KICHEKO. SI MNAJUA KUCHEKA/KICHEKO NI DAWA ISIYOLETA MADHARA.
KUMBUKENI TUPO PAMOJA!!
Monday, March 17, 2014
EBU JUMATATU HII YA LEO TUANZE NA MSEMA HUU CHEKA UNENEPE:- VICHEKESHO VYETU!!
Katika kuhakikisha wanafunzi wa darasa la kwanza wanaelewa, mara nyingi walimu hutumia mifano mingi sana, nakumbuka baba yangu alivyokuwa akitupatia mifano mingi ili tuelewe...haya fuatana nami na mahojiano yafuatayo ambayo mwalimu alikuwa anajitahidi kuwaelewesha wanafunzi wake:-
Mwalimu:- Nikikupa chapati sita halafu ukala mbili zitabaki chapati Ngapi?
Mwanafunzi:- Ukinipa na chai ya maziwa haitabaki hata chapati moja.
HAYA NIKUTAKIE JUMATATU NJEMA SANA NA PANAPO MAJALIWA TUTACHEKA TENA JUMATATU IJAYO:-)

Sunday, August 25, 2013
NI DOMINIKA YA 21 YA MWAKA C..WATOTO
Watoto wana hali ya kimbingu. kwani wana kila sababu: unyofu. utulivu. amani, upendo, furaha, mapatano. umoja, ushirikiano. usikivu na unyenyekevu. Ndiyo maana hata Bwana wetu yesu Kristu alisema: "Waacheni wadogo waje kwangu." Hali hii inatakia kwa kila mmoja wetu ili baada ya maisha haya ya sasa tukafurahi pamoja na Mungu katika utatu, milele yote mbinguni.
JUMAPILI NJAMA
Thursday, February 28, 2013
TUUMALIZE MWEZI KIHIVI:- NANGOJA ANIUE, NIKIONDOKA WANANGU WATATESEKA!
Kama mnavyojua kuwa hivi karibuni nilikuwa huko nyumbani Tanzania, na nilikuwa pande za huko kwetu Ruhuwiko Songea ambapo nilikaa kama mwezi hivi.
Kusema kweli yapo mengi ya kushangaza, ya kutisha na yenye kufurahisha ambayo niliyashuhudia, na kusema kweli kuna mengi nimejifunza. Lakini labda niseme tu kwamba aina ya maisha niliyoyakuta huko kijijini, kwa kweli yalinipa picha kwamba bado kuna safari ndefu sana katika kuufikia ukombozi wa huyu kiumbe mwanamke.
Ninayo mifano mingi lakini tukio nililolishuhudia siku moja nikiwa katika matembezi yangu liliniacha mdomo wazi, na labda niseme kwamba limenikaa hadi leo akilini nikijaribu kuwaza na kuwazua lakini sipati jibu.
Sijui nianze vipi?...Ahh! Kuna siku katika matembezi yangu nikakutana na kundi la akina mama wamekaa wakipiga gumzo, lakini nyuso zao zilikuwa zimegubikwa na huzuni. Nilishikwa na tashwishwi, nikajongea pale walipo ili kujua kama kuna jambo gani limetokea kiasi cha kuwakusanya pale huku wakiwa na nyuso za huzuni.
Si mnanijua tena mie KAPULYA MDADISI. Nikawauliza, ‘jamani ndugu zanguni, kulikoni mmekaa na nyuso za huzuni, JE KUNA MSIBA?’
Wote waligeuka kuniangalia, lakini walionekana kusita kunijibu, na ndipo mmoja wao akaniambia kuwa usiku wa jana kulitokea kutoelewana kwa wanandoa wanaoishi hapo mtaani kiasi cha mume kumpiga mkewe mpaka akapoteza fahamu.
Niliuliza sababu ya ugomvi wao, na ndipo nilipoelezwa kwamba, sababu kubwa ni kwamba wanandoa hao wana watoto wanne ambao bado ni wadogo na mume anataka kuongeza mtoto wa tano, lakini mkewe hataki kwa kuwa hali ya uchumi hairuhusu, na pia bado wanalo jukumu la kuwalea hawa watoto wanne ambao kwa kweli ni wadogo. Hata hivyo alimshauri mumewe wavute subira kwanza ili watoto hao wakue.
Mume hakukubali ushuri wa mkewe na ndipo ugomvi ulipoanza.Walibainisha kwamba ugomvi wao ni wa mara kwa mara na sababu kubwa ni hiyo ila ugomvi wa safari hii ulikuwa ni mkubwa na kama sio majirani kuingilia kati basi mume yule angemuua mkewe.
Nikataka kujua kama anapata kipigo cha aina hii kila mara kwa nini asirudi kwao?
Wakanijibu kuwa, kwanza hana nauli ya kurudi kwao kwani si mtu wa Songea. Pili anaogopa watoto wake watateseka.
Mh! Nilishusha pumzi, ujinga gani huu. Hivi sisi wanawake ni nani ameturoga, yaani unakubali mtu anakutesa na kukunyanyasa kiasi chakutaka kukutoa roho lakini wewe umo tu! Ukiulizwa sababu unadai, eti watoto wangu watateseka!
Bado najiuliza hivi watoto wanne bado hawatoshi? Hili tukio kwa kweli nimekuwa nikijiuliza tangu nirudi huku Sweden, na mpaka leo sijapatajibu kwamba tatizo ni nini? Kutokuelewa haki zetu, ujinga au ni nini?
NAWATAKIENI WAOTE MWISHO MWEMA WA MWEZI HUU FEBRUARI (PILI)

Monday, February 11, 2013
JUMATATU HII TUANZA HIVI:-DHULUMA KWA WATOTO YATIMA...
Je huu kweli ni uungwana... tutafakari pamoja..kila la kheri!!
Sunday, January 20, 2013
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA JUMAPILI NJEMA SANA!!!!! MICHEZO NI FURAHA!!!!
Licha ya kuwafundisha watoto elimu ya kitabuni, wanahitaji pia michezo ili waweze kujengeka kimwili, kiakili, kiroho na kuwa na maadili mema.. JUMAPILI NJEMA SANA....
Thursday, December 6, 2012
JINSI WATOTO WA KIKE WANAVYOJIFUNZA MAISHA ...
....mtoto umleavyo ndivyo akuavyo..ila kuna wakati katika jamii yetu huwa tunazidisha kidogo..mtoto anakuwa kama mtu mzima kabisa. Kwa maana hiyo anakosa ule muda wa kuwa mtoto. Ila tumejifunza mengi na tumekuwa kwa kiutu uzimauzima si kama sasa..au wenzangu mliopitia maisha haya mnasemaje?..Duh! siku zinakimbia tayari leo ni Alhamisi ya tarehe 6/12/2012..KILA LA KHERI WANDUGU!!!!
Wednesday, November 14, 2012
UMESHAWAHI KUCHEZA MCHEZO HUU?!!
Maisha siku zote huwa tofauti toka ulipokuwa mtoto hadi kufikia uzeeni. Hatua hii hupitia mambo mbalimbali haswa za kimechezo. Nakumbuka nilipokuwa mtoto tulicheza michezo mingi ya heshima tofauti na watoto wa sasa hivi. Haya yote yanasemekana ni kutokana na utandawazi ambao huwajengea watoto ufahamu zaidi.
Huu ni mchezo wa Kuruka kamba ambao tuliucheza utotoni na pia kiafya una umuhimu. Michezo mingine ni Kombolele(Mchezo wa kujificha), Utengenezaji wa magari, Ndege wakati wa mavuno, Midoli ya kutengeneza, Kula mbakishie baba, Kutengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia udongo, ukutiukuti, Kioo Kioo, mdako mpira (lede ledesta) ,Kujipikilisha....................................pia katika mchezo huu wa kuruka kamba nakumbuka tulikuwa tukiimba hivi:- Kamwambie baba baba sisi tunacheza cheza hatuogopi fimbo fimbo mtoto acha kuningínikax2.....
Sijui ndo uzee naona kama nimesahau basi tusaidiane kukumbushane ......!!!!!!!!
Tafakari juu ya mtoto wako ingawa sasa hivi tunawanunulia vitu vya kuchezea ila wanavitumia ipasavyo na halafu vinakuwa vingi mno. Nimekumbuka sana michezo hii ya utotoni ..je? nawe unakumbuka kitu?
MAISHA NA MAFANIKIO INAWATAKIA WOTE JUMATANO NJEMA SANA!!! DAIMA PAMOJA.

Sunday, September 16, 2012
Ngoja leo tusali Sala ya Wazazi wakiwaombea Watoto wao
Tunawaangalia , Ee BwanaHawa uliotujalia.Katika hawa tunajiona sisi wenyewe. Je, kweli tulikuwa hivi sisi
Tulipokuwa watoto? Tulipigana hivi? Tulipaiga kelele hivi? Tulileta furaha namna hii. Na mateso namna hii kwa wazazi wtu? Tunashangaa na kujiuliza....Tunajaribu kukumbuka-----Kukumbuka jinsi ilivyokuwa
Tulipokuwa watoto wadogo bado. Tukiwatazama watu wakubwa.
Wakati mwingine wanatutia wasiwasi, Bwana. Au kwa namna nzuri zaidi, tunajitia wasiwasi sisi wenyewe
Kwani si rahisi kuwa sawa daima. Lakini kuna furaha pia, furaha kubwa wanayotuletea. Nao hutufanya tuone fahari,kwani ni watoto wema.
Tunakushukuru kwa ajili yao Bwana, wao ndiyo zawadi yako bora kwetu,baada yetu sisi wenyewe. Utusaidie tuunganisha mikono yetu na mkono yako Ili, Ee Baba,Wawe kweli Watoto wetu.
Amina.
JUMPILI NJEMA KWA WOTE

Tuesday, August 28, 2012
HAPA WENGI TUNAKUMBUKA MALEZI YA WATOTO!!
![]() |
....na hapa ndipo watu wanapojifunza maisha ni nini/ hawa ndiyo wataweza kuyamudu maisha yoyote yale na pia kujua ugumu na uzuri wa maisha ....JUMANNE NJEMA!!!!
Friday, August 24, 2012
IJUMAA YA LEO :- TUUNGANE NA NJOMBE INTERNATIONAL ACADEMY!!!
NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA NA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA!!!
Monday, July 23, 2012
PICHA YA MWEZI:- KUJIFUNZA MAPISHI (KUJIPIKILISHA)!!
Picha hii inanikumbusha mbali sana, jinsi ya kujifunza kupika MAPISHI. Eee bwana weee basi hapo ndiyo hapo hapo pa kujifunza maisha baba na mama...Je wewe msomaji uliwahi kucheza mchezo huu?.
Monday, June 25, 2012
Tuanze jumatatu hii kwa kuangalia jinsi watu walivyo:- Malezi ya watoto/Ukatili Kwa Watoto
Watu /binadamu tumeumbwa tofauti , labda pia ni jambo la kumshukuru Mungu. Maana fikiria kama wote tungekuwa wakatitili sijui ingekuwaje? Na kama wote tungekuwa wema sijui ingekuwaje??
Wednesday, June 6, 2012
Wanafunzi hawa wanafanyishwa vibarua
Ije jumatano ya KIPENGELE CHETU CHA MARUDIA NDIO LEO NA LEO NIMEONA KWA VILE WIKI ILIYOPITA TULIZUNGUMZIA KIDOGO KUHUSU ELIMU BASI TUENDELEE KIDOGO NA MADA HII YA SHULE NA ELIMU.
Wanafunzi wa shule ya msingi Ndingine mwambao mwa ziwa Nyasa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakifanyishwa kazi ya kusomba tofali muda wa masomo
LICHA ya serikali kupiga marufuku walimu kuwafanyisha vibarua wanafunzi wakati wa masomo,bado baadhi ya shule hasa katika maeneo ya vijijini,zinaendelea na tabia hiyo hali ambayo inachangia kuzorotesha elimu nchini.
Uongozi wa shule ya msingi Ndingine iliyopo kata ya Ngumbo mwambao mwa ziwa Nyasa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma bado unaendelea kuwafanyisha vibarua wanafunzi licha ya afisa elimu wa wilaya hiyo kupiga marufuku jambo hilo.
Uchunguzi ambao umefanywa na mwandishi wa habari hizi katika kijiji cha Ngumbo hivi karibuni ulibaini wanafunzi baadhi wakiondolewa madarasani tena majira ya asubuhi na kwenda kufanyishwa kibarua cha kubeba tofali za kuchoma kutoka kwenye tanuli lililokuwa mtoni hadi mahali ambapo nyumba inajengwa umbali wa kilometa tatu.
Wanafunzi wa darasa la tatu na la sita kutoka shule hiyo walishuhudiwa wakisomba tofali hadi nne kichwani huku wakilalamika kuwa wanafanya kazi ambayo hawanufaiki nayo licha ya kuambulia maumivu kutokana na mzigo na umbali.
Baadhi ya wanafunzi wanasoma darasa la sita walipohojiwa ,walidai kuwa mwalimu amewaambia huo ni mradi wao ambao utawawezesha kupata fedha kwa ajili ya sherehe za mahafali ya kumaliza elimu ya msingi hapo mwakani watakapomaliza darasa la saba.
Hata hivyo wanafunzi wa darasa la tatu walilalamika kuwa wao wamelazimishwa na mwalimu kwa kuwa hawapati chochote na kwamba fedha zote wanachukua walimu,ingawa tofali zinachangia kuchafua sare zao za shule ambazo wakirudi nyumbani inawalamu wazazi kununua sabuni ili kufua nguo zao.
Miongoni mwa wazazi waliohojiwa kuhusiana na watoto wao kuendelea kufanyiwa kazi za vibarua,waliomba serikali ya wilaya kuwachukulia hatua walimu wa kata za Ngumbo na Liwundi kwa kuwa wamezoea kuwafanyisha kazi wanafunzi wao licha ya wazazi na walezi kukataa.
“Sisi wazazi kwenye vikao tulishakubaliana tutachangia shilingi 2000 kila mzazi ,walimu waache tabia ya kuwafanyisha kazi watoto wetu badala yake waendelea na kusoma lakini walimu bado wanaendelea kuwafanyisha kazi mbalimbali wanafunzi kama vile kuchota maji ya walimu,kubeba tofali,kukata matete,kubeba kuni pamoja na kazi nyingine nyingi’’,alisema Martha Nchimbi mkazi wa Mkili.
Hata hivyo mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ndingine Aidan Mbilinyi alipohojiwa kuhusiana na kuwafanyisha kazi za vibarua wanafunzi alidai kuwa katika shule yake wanafunzi hawafanyishwi vibarua badala yake wazazi wanachangia kila mwaka shilingi 2000 kwa ajili ya sherehe za mahafali ya darasa la saba .
Katika kikao cha walimu wakuu wote wa wilaya ya Mbinga ambacho kiliitishwa na idara ya elimu chini ya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Septemba 23 mwaka huu pamoja na mambo mengine waliazimia kuacha kuwafanyisha vibarua wanafunzi vikiwemo kusomba tofali na kuvuna kahawa.
Afisa elimu wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga David Mkali amekemea tabia ya walimu wakuu kuendelea kuwafanyisha kazi wanafunzi na kusisitiza kuwa kuanzia sasa atachukua hatua za kinidhamu kwa walimu wakuu wote ikiwa ni pamoja na kuwashusha vyeo vyao.
“Maazimio yalipitishwa tangu mwezi Septemba mwaka huu marufuku wanafunzi kufanyishwa vibarua,shule zibuni miradi ya kujitegemea itakayowawezesha kupata fedha,pia walimu kuwapatia wanafunzi maarifa ya kujitegemea kwa mfano kulima bustani baada ya saa za masomo’’,alisisitiza.
Mkali aliyataja mambo ambayo yamechangia kushuka kwa elimu na ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani Mbinga kuwa ni pamoja na wanafunzi kufanyishwa vibarua,utoro na ulevi kwa baadhi ya walimu,walimu kutofundisha siku zote 195 zilizopangwa na wizara,walimu wakuu kutofuatilia ufundishaji,ukaguzi wa maandalio na kazi za watoto.
Takwimu zilizokusanywa katika shule 321 katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga kuanzia darasa la tatu hadi la saba zinaonesha kuwa wanafunzi 15,128 kati ya 116,966 hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu
Makala hii nimeipata hapa JAMIIFORUM IMEANDIKWA NA Albano Midelo hapo decemba 13th 2011 pia kwa kuweza kusoma habari nyingi inayofanana na hii ingia hapa. TUKUTANO TENA JUMATANO IJAYO PANAPO MAJALIWA.
Monday, May 14, 2012
JUMATATU HII AU WIKI HII TUANZE NA:- DONGI DONGI EMBE!!!
Thursday, May 3, 2012
EBU ANGALIA HAPA KAAAZI KWELIKWELI MAISHA HAYA JAMANI!!!
Habari/simulizi kama hii niliwahi kusikia wakati ule naishi Madaba/Matetereka kuwa akina mama walikuwa wakienda kilabuni walikuwa wakiwanywesha watoto pia. Kisa walikuwa wanataka watoto wasiwasumbue, maana wakipata pombe basi wanalala...duh! kweli tembeo uone!!! NAWATAKIENI WOTE JIONI NJEMA INGAWA KWANGU YAMEIBUKA MASWALI KIBAO KICHWANI BAADA YA KUONA HII HABARI. !!!
Thursday, March 15, 2012
Uganda yaanza 'kutibu watoto wanaosinzia'
ugonjwa usiojulikana chanzo wa 'kusinzia'
Uganda imefungua vituo vya afya vya kwanza maalum kwa kusaidia maelfu ya wattoto ambao wana dalili za ugonjwa ambao haujajulikana chanzo chake wa 'kusinzia.’
Vituo hivyo vilivyo kaskazini mwa nchi, ambako ugonjwa huo umeenea, vinakusudiwa kudhibiti dalili mbaya za ugonjwa huo.
Chanzo cha ugonjwa huo hakijajulikana lakini unawapata watoto pekee, wanaoshambuliwa na dalili za kudumaa kiakili na kimwili na kusinzia.
Kuna taarifa za ugonjwa huo kuwa upo nchi za Sudan Kusini na Tanzania.
Kudhibiti dalili
Zaidi ya watoto 200 wenye ugonjwa huo walijitokeza Jumatatu kwa ajili ya matibabu katika vituo hivyo katika wilaya za Kitgum, Pader na Ramor, Kamishna wa Huduma za afya nchini Uganda Dr Anthony Mbonye aliiambia BBC.
Wafanyakazi wa afya hawawezi kutoa tiba yoyote maalum mpaka madaktari wagundue chanzo halisi cha ugonjwa huo –lakini Dr Mbonye anasema wamewapa mafunzo kusaidia maisha ya watoto kwa kudhibiti dalili za fadhaa kwenye mfumo wa neva.
Dawa za kupambana na kifafa zimekuwa na nguvu kutibu wagonjwa wa kusinzia, kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani.
Ugonjwa wa kusinzia unasababisha watoto kufaidhika na kutetemeka na hatimaye kufa.
Mwandishi wa BBC mjini Kampala Ignatius Bahizi anasema mbunge wa jimbo hilo Beatrice Anyor, amekuwa akiongoza kampeni kwa serikali kushughulikia zaidi tatizo hilo ambalo anasema limesababisha wasiwasi mkubwa maeneo ya vijijini.
Wizara ya Afya nchini Uganda imerekodi matukio 3,000 ya ugonjwa huo na karibu vifo 200 vimetokea tangu mwaka 2010.

via BBC Swahili
Subscribe to:
Posts (Atom)