Showing posts with label malezi. Show all posts
Showing posts with label malezi. Show all posts

Tuesday, April 11, 2017

WATOTO UWALEAVYO NDIVYO WAKUAVYO...MICHEZO !

 Michezo hii huwajengea watoto tunu njema kama umakini, furaha, urafiki, ubunifu, kuchemsha bongo na pia kutulia nyumbani na mengine mengi.
Hapa wakicheza mdako...nimekumbuka mbali sana maana nilikuwa nikipenda sana huu mchezo...hapa pia yahitaji umakini maana wakati wote ni kuhesabu tu...Vipi nawe ndugu msomaji una mchezo ambao ulicheza enzi hizo?

Monday, February 27, 2017

MALEZI:- WAACHE WATOTO WAWE WATOTO

Katika jamii yetu wengi wanadharu sana micezo ya watoto. Wanaona ni kupoteza mida tu lakini tukumbuka kwamba michezo yote wafanyayo watoto inachangia sana ukomavu wa ubongo wao maana pale hawachezi tu wanajifunza kitu pia. Kwa mfano katika michezo mingi ya watoto kuna kuhesabu kwingi sana, hapa tayari anajifunza kitu...tuwape nafasi watoto kuwa watoto na pia kama wazazi tujaribu kuwa pamoja nao na kushiriki baadhi ya michezo.
CHUKUA DAKIKA TU ANGALIA HII VIDEO HAPA CHINI ......

UJUMBE:- WAZAZI/WALEZI WATOTO WETU WANATUHITAJI SANA TUTENGE MUDA KWA AJILI YAO. TUSIWASAHAU NI JUKUMU LETU.

Monday, August 8, 2016

KUANZA KUPOTEA KWA DESTURI YA UKARIBU WA KIFAMILIA KUNAVYOATHIRI MALEZI

Malezi katika mazingira yetu ya ki-Afrika ni suala nyeti. Kwa kutambua umuhimu wa malezi katika kujenga jamii yenye ustawi, wa-Afrika tumekuwa na desturi ya kuelekeza nguvu zetu nyingi katika malezi ya wanetu. Kwa mfano, tangu mtoto anazaliwa, ilikuwa ni lazima alale kitanda kimoja na wazazi wake kwa muda unaozidi miaka miwili. Mtoto mchanga hakuachwa alale kwenye kitanda chake mapema kwa sababu za msingi zilizokubalika katika jamii zetu.


MAMA AKIWA KAMBEBA MWANAE
Aidha, mtoto daima alikulia mikononi mwa watu wazima aliowafahamu vyema. Watu hawa ama aliishi nao kwenye boma la wazazi wake au walitoka miongoni mwa jamaa inayomzunguka. Muda mwingi mtoto alibebwa mgongoni kwa mama yake au dada zake. Desturi ya kubeba watoto mgongoni ilifanya suala la ukuaji wa mtoto kufuatiliwa kwa karibu sana na imethibitika kisayansi kusaidia kujenga muunganiko wa kihisia kati ya mzazi na mtoto. Jambo hili, hata hivyo, halieleweki kwa wageni wa bara hili wanaodhani ni aina nyinine ya udhalilishaji wa mtoto.

Chakula cha pamoja ni kitamu sana

Wakati wa jioni, familia zilikuwa na desturi ya watoto kukaa na wazazi wao kijinsia. Baba aliota moto na watoto wa kiume akiwasimulia mambo mbalimbali ya kimaisha. Kadhalika, mama naye alifanya kazi za jikoni kwa ushirikiano wa karibu na watoto wa kike. Chakula kilipokuwa tayari kililiwa kwa ushirikiano. Muda wa chakula ulifahamika, na kwa kweli, kila mtoto aliwajibika kuwepo kupata chakula. Kwa kuwa chombo kilichotumika kulia chakula mara nyingi kilikuwa kimoja basi kila mmoja katika familia alilamizika kula kwa ushirikiano na wenzake.

Desturi hii ya kukaa karibu na watoto na kufanya mambo mengi kwa pamoja iliwasaidia wazazi kuwafundisha watoto maarifa na ujuzi wa aina mbalimbali. Vile vile, ukaribu huu ulikuza uhusiano wa karibu wa kifamilia. Kadhalika, karibu huu uliwahakikishia watoto usalama wao. Kisaikolojia walijua hawana wasiwasi kwa sababu baba na mama wapo na wangepigana na yeyote anayetishia usalama wao. Watoto waliwategemea wazazi wao.

Upo ushahidi wa kiutafiti kwamba kutegemewa kwa mzazi ni nguzo kuu ya malezi. Kwamba mtoto huiga mengi wa mzazi ikiwa anaamini mzazi huyo ni wa kutegemewa na yuko upande wake. Hali hii ilimfanya mtoto asiwe na wasiwasi na usalama wake pale yalipojitokeza mazingira ya kutengana kimwili na kwa hivyo wazazi kwa kweli hawakulazimika kuwa na watoto muda wote. Kama tutakavyoona katika mfululizo huu, hali hii ya mtoto kumwamini na kujisikia salama mikononi mwa mzazi inategemea sana uwepo endelevu wa mzazi kimwili na kihisia tangu siku za mwanzo za maisha ya mtoto.

Hata hivyo, kadri mwanadamu anavyozidi ‘kuendelea’ na ‘kustaarabika’, ndivyo desturi hii ya kupatikana kwa wazazi nyumbani inavyozidi kukosa umaarufu. Kwa mfano, ipo dhana inajengeka katika jamii kwamba maendeleo halisi ni vitu. Matokeo ya imani hii ni kutufanya tutumie muda mwingi ‘kuhusiana na vitu’ zaidi kwa gharama ya mahusiano na ustawi wa familia zetu.

Kadhalika, zipo changamoto nyingine za kijamii zinazotishia desturi ya familia. Kuna masuala kama kazi/ajira zinazowatenganisha wazazi na familia, misukosuko ya kimahusiano inayozaa talaka na/ama kulazimisha malezi ya mzazi mmoja, ujio wa shule za bweni kwa watoto wadogo pamoja na matatizo kadha wa kadha yanayofanya watoto wadogo wakue katika mazingira magumu yasiyo na uangalizi mzuri. Haya tutayaangalia wakati wake ukifika.

Kwa hiyo, ili kukabiliana na changamoto hizi mpya, upo umuhimu mkubwa wa kujadili tafiti zilizochunguza athari za mazingira haya mapya ya kimalezi ambayo kwa kiasi kikubwa hayakuwepo huko nyuma. Kwa mhutasari, tunaweza kutaja suala kuu linalojitokeza kwa haraka. Kwamba uhusiano kati ya mzazi na mtoto unaathiri mahusiano ya mtoto huyo na watu wengine. 

Tuesday, August 28, 2012

HAPA WENGI TUNAKUMBUKA MALEZI YA WATOTO!!


Katika malezi/makuzi watu tumetoka mbali, huyu binti hapa ananikumbusha mbali sana.Wazazi wanaondoka asubuhi huku wakitegeme binti mimi/huyu afanye kazi ya kuchota maji. Na hapo labda sio ndoo moja tu pipa zima. Na hapo hapo amtunze mdogo wake. Na labda kuchochea maharage pia. Hali hii kwa sasa hakuna kabisa maisha yamebadilika kabisa ndiyo kwanza utakuta mtoto anamtuma mzazi wake. Maisha siku hizi yamekuwa  watoto na TV, Komputa, simu nk. Hata kumwona mtoto siku hizi anasoma kitabu ni mara chache sana. Ndiyo maana  sisi tuliolelewa  katika malezi ya aina hii kama huyu binti inatupasa tuendeleza kwa kuwahimiza  watoto wetu waweze kufanya hivyo hata kama ni kidogo. Polepole ni mwendo...Hata hivyo najua hali hii ya watoto kusaidia kazi za nyumbani vijijini bado inaendelea. Binafsi niitazamapo picha hii najiona ni kama mimi...na naweza nikasema natamani niwe tena kama huyu binti...Je? umewahi kuifanya kazi hii? au labda kuchunga mbuzi na ngómbe kama watoto hawa hapa....


....na hapa ndipo watu wanapojifunza maisha  ni nini/ hawa ndiyo  wataweza kuyamudu maisha yoyote yale na pia kujua ugumu na uzuri wa maisha ....JUMANNE NJEMA!!!!

Wednesday, July 4, 2012

MAMA MZAZI NA MAMA WA KAMBO.!!!!

NIMEONA TU TUENDELEA NA HII PIA ...Hata mie huwa najiuliza kila siku hivi akina mama kwa nini wanawatesa watoto wasio wao? Uchungu si uleule jamani? Nimesikiliza sana wimbo huo hapo chini sijaelewa wanasema nini ila matendo nimeelewa. Mada  hii hapa chini nimeipata hapa.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------
Naamini HAKUNA mama anapenda kuwa MAMA WA KAMBO.Hakuna mwanamke anazaliwa kuwa MAMA WA KAMBO.Mama yeyote yule anaweza kuwa MAMA WA KAMBO baada ya kuwa na sifa ya kuwa MAMA.
Sifa moja wapo ya kuwa mama ni
..Uwezo wa kubeba, kuzaa kiumbe, kunyonyesha, kuhudumia, kukitibu kiumbe mtoto...
Mwanamke bila mtoto hawezi kuitwa MAMA.
Sasa basi......Mwanamke yeyote yule ambaye kajifungua mtoto anaweza kuwa MAMA wa KAMBO.
Baadhi ya Sifa za MAMA WA KAMBO.
KATILI.
JEURI.
MBINFASI.
Kabla Mama hajaitwa MAMA WA KAMBO hana hizo zifa za MAMA WA KAMBO lakini akishaukwaa UMAMA WA KAMBO basi ananyakua hizo sifa.
SWALI.
Hii siku ya mama duania inawahusu na MAMA WA KAMBO?

Labda twende mpaka huko Botswana na kumalia na wimbo huu STEPMOTHER/MAMA WA KAMBO...

TUACHE UKATILI AKIMA MAMA..MTOTO WA MWENZAKO NI WAKO NA WAKO WA MWENZAKO.....

Friday, May 4, 2012

CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA PICHA YA WIKI :- JE? HUU NI UBUNIFU AU?

Nimetumiwa picha hii na msomaji wa Maisha na Mafanikio kwanza nikashikwa na butwaa, na pili nikajiuliza ni ubunifu? Na tatu nikajiuliza kukosa mtu wa kumtunza mtoto au chekechea? Nawaachia mwenzangu tusaidiana kujadili hapa...Duh! ila sidhali kama mtoto huyo anapata raha hapo.....MCHANA MWEMA MAJEMANI!!!

Thursday, May 3, 2012

EBU ANGALIA HAPA KAAAZI KWELIKWELI MAISHA HAYA JAMANI!!!


Habari/simulizi kama hii niliwahi kusikia wakati ule naishi Madaba/Matetereka kuwa akina mama walikuwa wakienda kilabuni walikuwa wakiwanywesha watoto pia. Kisa walikuwa wanataka watoto wasiwasumbue, maana wakipata pombe basi wanalala...duh! kweli tembeo uone!!! NAWATAKIENI WOTE JIONI NJEMA INGAWA KWANGU YAMEIBUKA MASWALI KIBAO KICHWANI BAADA YA KUONA HII HABARI. !!!

Thursday, August 25, 2011

PICHA ZA WIKI HII:- MAMA NA MWANA!!!


CAMILLA NA MAMA YAKE YASINTA (mwaka jana 2010 mwezi wa saba)




NA HAPA NI MALIA NA MAMA YAKE MICHELLE

Ni ujumbe tu mfupi ambao unaweza kukufanya utafakari kitu fulani....PAMOJA DAIMA!!!



Monday, June 13, 2011

SHUKRANI ZANGU KWA WALEZI/WALIMU

Leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa WALEZI/WALIMU kwa kazi kubwa waifanyayo. Sijui kama wewe mwenzangu umewahi siku moja kufikiria ya kuwa hakuna mlezi/walezi wazuri kama walimu. Fikiria mtoto aanzapo chekechea, unampeleka huko chekechea/”shule ya Vidudu” na wewe mwenyewe unaenda kazini na baadaya ukishamaliza kazi unaenda kumchukua.
Na unakutana mtoto mwenye furaha tele kabisa. Na pia inawezekana baada ya muda mtoto atakuwa kamzoea zaidi mwalimu kuliko hata wewe na mwalimu atamfahamu zaidi mwanao kuliko wewe/mimi mwenyewe.
Nimejaribu kufikiria sana, sisi wazazi jinsi tulivyo na muda mchace sana kuwa na watoto wetu. Je? wewe pia umefikiria hili? Yaani hapa unaweza kusema walimu wa chekechea wao ndio wazazi kamili. NA INAWEZEKANA HATA KUANZA KUTEMBEA NA HATA KUSEMA MANENO YA KWANZA ANAANZIA HUKOHUKO CHEKECHEA.
Kwa kweli mnastahili PONGEZI WALIMU.
Na baada ya miaka ya kuanza shule ifikapo, hapo ndio inakuwa pia mtoto anaondoka asubuhi kwenda shule. Muda wote anakuwa na MWALIMU/WALIMU. Na mwalimu/walimu ndiye/ndio wamleao kwa asilimia kubwa. Kwani anakuwa muda mwingi san ana mtoto /watoto wako/wetu kuliko sisi WAZAZI. Nimejaribu kufikiria kwa mfano mimi mwenyewe binafsi, mara nyingi tunaagana asubuhi na halafu tutaonana tena kesho alasiri nirudipo katika mihangaiko yangu . Na kwa wengine huwa hawakutani kabisa na watoto asubuhi. Kwa vile labda baba au mama anahitajika kuwahi sana kazini, na anaporudi jioni watoto wanakuwa wamelala na kesho yako hivyo hivyo huondoka kabla watoto hawajaamka.


Kwa hiyo mimi kama mzazi napenda kutoa shukrani zangu kwa WALEZI/WALIMU WOTE KWA KAZI NZURI MUIFANYAYO. MAANA MNASTAHILI KWA KWELI. AHSANTENI SANA!!!!

Tuesday, February 22, 2011

SIKU AMBAYO SITAISAHAU

Restieli akiwa amejipumzisha nyumbani
kwao Njoro baada ya kutoka shuleni
Leo hii nimepokea waraka huu kutoka kwa binti Restieli Moses Mbwambo aishiye kule Moshi Kilimanjaro, waraka ambao umetumwa kwa msaada wa mdau wa BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO aliyeko kule MOSHI. Na mie bila kuongeza wala kupunguza neno nauweka kama ifuatavyo:

Ni siku ambayo niliungua na mafuta wakati nilipokuwa mdogo wa umri wa mwaka mmoja na nusu. Ukweli ni kwamba nilisimuliwa na wazazi wangu jinsi tukio hilo lilivyotokea kwa kuwa mri wangu ulikuwa ni mdogo. Walinisimulia kuwa tukio hilo lilitokea hapo mnamo tarehe 17 Julai 2002, siku ya Jumatano jioni.
Siku hiyo mama yangu alikwenda kurekodi nyimbo zao za kwaya huko Arusha na baba alikwenda kanisani kuhudhuria ibada ya jioni katika kanisa lao la Njoro SDA lililopo hapa mjini Moshi, hivyo akaniacha na jirani ili aniangalie.
Wakati baba ananiacha na jirani yao, alikuwa ndio kwanza anajiandaa kuchoma maandazi yake kwa kuwa alikuwa ni mfanyabiashara wa maandazi pale mtaani.
Kutokana na sijui udogo au utundu naambiwa kuwa nilikwenda kwenye kikango cha mafuta na kukishika ambapo kilipinduka na yale mafuta ambayo yalishakuwa yamepata moto yalinimwagikia mwili mzima na kunisababishia majeraha na maumivu makali.
Baba alijulishwa na aliporudi nyumbani akakuta nimeshapelekwa hospitali ya Mawenzi na baadae nikahamishiwa Hospitali ya KCMC kwa ajili ya matibabu.
Mama alirudi majira ya saa kumi na mbili jioni na kujulishwa juu ajali iliyonipata, akaja haraka hospitalini.
Kwa kweli niliungua sana kwa kuwa mafuta yalikuwa ni ya moto sana. Watu walitoka kanisani walipokuwa wakimuimbia mungu na kuja Hosptalini kuniona.
Siku ya Jumamosi ambayo ni siku a sabato ilitangazwa pale kanisani juu ya ajali iliyonipata hivyo waumini wote walipotoka kanisani walikuja moja kwa moja kuniona na walikuwa wengi sana.
Nikiwa ndio nimetimiza miaka kumi mwaka huu, nimelikumbuka sana tukio hili na ndio maana nikaamua kukaa chini na kuandika kumbukumbu hii na kumpa mama na baba yangu kama kumbukumbu ya tukio hilo la kusikitisha.
Namshukuru mungu sana kwa kunilinda mpaka sasa nimetimiza miaka kumi, jina la Bwana lipewe sifa.
Pia nawashukuru wazazi wangu, majirani na washirika wa kanisa la Njoro SDA kwa kuwa karibu na wazazi wangu katika kipindi chote cha madhila yangu.
Natoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini wanapokuwa au wanapoachiwa watoto wadogo kuwaangalia, kwa kuwa watoto hawajui vitu vya hatari, kama moto, visima, magari na kadhalika.
Tarehe 17 Julai 2002 ni siku ambayo sitaisahau
Ni mimi Restieli Moses Mbwambo wa Njoro Moshi.

Tuesday, August 24, 2010

Ilikuwa Jumapili ambayo sitaisahau!!

Kanisa la Makwai Lundo hapa ni 2007!!



Nataka leo kuwasimulieni kisa kilichonipata wakati nilipokuwa miaka 8-9 hivi:- Haya ungana nami katika simulizi ya kisa hili.

Ilikuwa siku ya jumapili asubuhi wote tukiwa katika maandalizi ya kwenda kanisani. Kanisa letu la Makwai Lundo (Nyasa). Nadhani baadhi yenu mnajua kuwa baba yangu alikuwa mwl. Ndiyo!! basi kama sikosei kulikuwa ni wakati wa kufanya mitihani. Na baba alikuwa na tabia ya kuchukua kazi zake za shule na kufanyia nyumbani.

Asubuhi hii ilikuwa si nzuri kwangu. Baba alikuwa bafuni akioga, kujiandaa kwenda kanisani. Basi akaja kaka yangu na kuniambia "Yasinta njoo tuangalie hii mitihani tuone nani kafaulu, mmmhh! mimi nikasita nikamwambia mimi naogopa, akasema njoo baba anaoga hatatukuta". Nikanaswa nikaenda kwenye ile meza iliyolundikwa makaratasi ya mitihani na ndio nikawa mpekuzi wa ile mitihani na kaka akawa anaangalia kama baba anakuja? Lakini naye akataka kuona na sasa kukawa hakuna mwangalizi baba huyu akatokea.

Eeeehh! bwana weeee, mzeee alikasirika huyo sikuwahi kumwona. Akamtuma kaka yangu akakate fimbo/kiboko. Nawaambieni hapo nilikuwa natetemeka, jasho lilinitoka na nusu nijisaidia hapohapo. Fimbo/kiboka kikaja, baba akatoa amri Yasintaaaa lala chini na bana kanzu yako akiwa na maana nibane gauni langu. We acha tu, maana kiboko kiliingia hicho tena bado nakisikia, kwa jinsi kilivyodunda.
Je wewe unayesoma unadhani jumapili hii iliisha vipi? Na je? ungekuwa wewe ungefanya nini?

Ni mimi kama kawaida KAPULYA wenu au kama wengine waniitavyo MTEMBEZI. Tukutane tena wakati mwingine!!!!

Sunday, August 1, 2010

Malezi ya Watoto Katika Mpango wa Mungu!!!!

Malezi bora kwa watoto


Watoto ni kitu cha thamani sana ambacho Mungu anawazawadia watoto wake kadiri apendavyo yeye. Inashangaza sana kuona watu wanavyosahau kuwa watoto wametoka kwa Mungu na wanapaswa walelewe kwa upendo na misingi ya neno la Mungu na badala yake wanawaona kama ni mzigo. Jinsi unavyomlea mtoto tangia akiwa bado mdogo kabisa ndivyo unavyoyajenga maisha yake ya baadaye.
Kwanza kabisa yakupasa uifahamu thamani ya mtoto ambaye Mungu amekupatia. Umhesabu kama zawadi toka kwa Mungu na sio mzigo hata kama haukupangilia kuwa naye kwa wakati huo maana Mungu alishamfahamu kabla hata hajazaliwa. Katika vitabu vya Yeremia na Zaburi tunaona kuwa Mungu anayafahamu maisha ya kila mtoto kabla hata mimba yake yaijatungwa.
Yeremia 1:5a Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa;
Zaburi 139:16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
Tambua kuwa Mungu amekuheshimu na kukupendelea kwa kukupa watoto/ mtoto ili umlee na kumtunza, kwa hiyo yakupasa umpende na kumlea kwa hekima ya ki Mungu na hata siku moja usimuone kama mzigo au kumsema vibaya kwa watu wengine. Hata kama mtoto wako atakuwa na mapungufu kitabia wewe kama mzazi unayemjua Mungu na unaitambua thamani ya mtoto uliyenaye, usimseme vibaya kwa watu bali umuombee, kumuelekeza kwa upendo na kumuonya kwa busara. Fahamu kuwa mtoto wako anathamani kubwa mbele za Mungu naye ndiye anayemjua vyema. Wewe kama mzazi unawajibika mbele za Mungu kwa jinsi unavyomlea mtoto wako ha hivyo yakupasa kujitoa kwa uaminifu katika kumlea kwa upendo na uvumilivu wote.
Tafuta kulifahamu neno la Mungu na kuitafuta hekima ya kiMungu katika malezi ya mtoto wako kuliko hekima ya mwanadamu. Jifunze Mungu anasema nini kuhusu malezi ya watoto na uyafuate hayo kwa uaminifu hata kama kibinadamu yanaonekana yamepitwa na wakati. Tumia muda kwenye maombi kumwombea mtoto wako na maisha yake ya kimwili na kiroho ili aweze kuongozwa na Mungu siku zote za maisha yake. Mfundishe mtoto wako tangia akiwa na umri mdogo habari za Mungu na kweli yote ya neno la Mungu. Katika maisha ya siku hizi ni kawaida kuona baba na mama wote wanafanya kazi nje na nyumbani hali inayopelekea watoto kubaki na mlezi muda mwingi wa mchana. Hali hii usipoiwekea mikakati katika malezi ya mtoto wako kiroho inaweza kuleta madhara makubwa hapo baadaye. Hakikisha muda unaoupata kuwa na mtoto wako unautumia kumweka karibu nawe na kumfundisha habari za Mungu.
Kuna njia nyingi ambazo mzazi unaweza kuzitumia katika kumfundisha mtoto wako habari za Mungu kwa ufanisi kuanzia katika umri mdogo kabisa. Anza kwa kuomba na mtoto wako wakati wote iwe ni asubuhi, wakati wa kula, usiku na wakati mwingine wowote ambao unafanya maombi. Mfundishe kuwa ni muhimu kuomba kabla ya kula na kulala na pia asubuhi baada ya kuamka. Kwa kufanya hivi mara kwa mara basi taratibu ataaza kuona kuwa maombi ni kitu cha muhimu na kadiri anavyokuwa mkubwa ataendelea na tabia ya maombi. Biblia katika kitabu cha mithali inasema mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee. (Mithali 22:6).
Msimulie hadithi za biblia kwa njia ya kufurahisha huku ukiwa unamsomea biblia. Mwanzoni itakuwa ngumu kukuelewa lakini kadiri unavyoendelea na kurudia rudia mara kwa mara itakaa ndani yae na itamjengea hamu ya kusoma biblia ili ajue kwa undani zaidi habari ambazo unamsimulia pale atakapokuwa anajua kusoma. Ukiweza mtafutie biblia ya watoto yenye hadithi fupifupi za biblia kwa picha. Waweza pia kutafuta video za hadithi za biblia kwa watoto na mkawa mnaangalia pamoja naye huku ukimsimulia , pamoja na kupata nafasi ya kumfundisha neno la Mungu pia utapata muda mzuri wa kufurahi na mtoto wako na kuwa karibu naye.
Mfundishe kuonyesha shukrani pale mtu anapompatia kitu au kumtendea jambo jema. Hata kama hajui kuongea mwambie sema asante hii itamfundisha kuwa ukitendewa jambo ni lazima kuonyesha shukrani. Mfundishe kumshukuru Mungu kwa kuamka salama, kupata wazazi wanaomlea vyema, kununuliwa michezo mbali mbali, n.k Moyo wa shukrani utamsaidia kumjua Mungu zaidi na atakuwa anatafuta mema ya kumshukuru Mungu kila siku. Ishi maisha ya upendo, furaha, amani na ukarimu wakati wote ili mtoto aone uhalisia wa Mungu katika maisha yako.
Nenda na mtoto wako kanisani kila jumapili na uwe unamwambia kwanini unaenda kanisani. Usisahau kumpa sadaka naye awe anatoa na umweleze kwa nini tunatoa sadaka kuwa ni njia ya kumshukuru Mungu kwa vingi alivyotupatia. Kumbuka kila mara kumkumbusha upendo wa Mungu, wema na ukuu wa Mungu.
Malezi ya mtoto ni huduma inayojitosheleza, ni jukumu ambalo umuhimu wake ni mkubwa sana na pale unapokosea matokeo yake kuyabadilisha huwa ni kazi ngumu sana. Mwamini Mungu katika jambo hili na mtegemee na kumtazamia yeye pekee, kama alivyokupa mtoto atakuwezesha kumlea katika njia impasayo.
–Magreth Riwa–

Habari hii nimeipata hapa nikaona si vibaya kama nikieweka hapa katika blog ya Maisha na Mafanikio ili wengi tujifunze. PIA NACHUKUA NAFASI HII KUWATAKIENI JUMAPILI HII YA KWANZA YA MWEZI WA NANE IWE NJEMA SANA. MWENYEZI MUNGU AWE NANYI NA BARAKA ZAKE ZITAWALE NYUMBANI MWENU!!!!!!

Thursday, January 28, 2010

HATUA MUHIMU KATIKA MAKUZI YA MTOTO

Katika udadisi wangu nikawa nimepitia blog ya http://kaluse.blogspot.com/ na kukuta makala hii na nikashidwa kuiacha kwa vile najua wote katika hizi blog lengo letu ni moja kuelimisha jamii.

Hivi umeshawahi kujiuliza hata siku moja, kwa nini watu wengine ni walevi? Wengine waongeaji sana? Wengine wakimya sana? Wengine waongo sana? Wengine wana tamaa ya ngono kupita kiasi na kadhalika? Lakini pengine una maswali mengi ya namna hii ambayo yanaonyesha jinsi wanadamu wanavyotofautiana.

Kuna hatua 5 muhimu ambazo mtoto lazima afanye mambo ambayo yanastahili kufanyika katika hatua husika. Na iwapo hayatafanyika, hali hizo huhifadhiwa katika mawazo yake ya kina na hivyo kumsababishia matatizo makubwa ukubwani.
Hatua hizo ni kama ifuatavyo:-

Hatua ya kwanza – oral stage: Hatua hii huwahusu watoto wa kuanzia siku moja mpaka miaka miwili. Katika hatua hii ya kwanza, furaha na raha ya mtoto huwa imejificha mdomoni. Utakuta mtoto kila wakati anafurahia kunyonya maziwa ya mama yake, vidole au midoli. Mtoto anatakiwa atumie mdomo wake mpaka ile hamu yake yote iishe. Kama ni kunyonya basi aendelee kufanya hivyo mpaka pale utakapofika wakati mzuri wa kumwachisha ziwa. Kumnyanyasa mtoto wakati ananyonya au kumfanyia vitendo ambavyo si vya kiungwana ikiwa ni pamoja na kumwachisha ziwa mapema, husababisha hamu yake ya kuutumia mdomo ibaki na hivyo kuhifadhiwa kwenye mawazo yake ya kina. Anapokuwa mtu mkubwa hulipa kisasi bila kujua kwa kuutumia mdomo kwa kadri anavyoweza. Hivyo anapokuwa mtu mkubwa anaweza akawa muongo sana, mlevi kupindukia, mvuta sigara sana, muongeaji sana, au mmbeya sana. Kama kuna watu unawafahamu wenye tabia hizi, jaribu kupeleleza kama walinyonyeshwa bila kunyanyaswa au kama hamu yao ya kunyonya iliisha.

Hatua ya pili – anal stage: Hatua hii humhusu mtoto wa miaka miwili au mitatu. Matumizi ya mdomo huwa yamekwisha na raha huhamia sehemu za haja. Katika hatua hii, mtoto hupendelea zaidi kutumia sehemu zake za haja kwa kukojoa au kwenda haja kubwa mara kwa mara. Katika kipindi hiki wazazi wengi hufanya makosa. Mzazi anashauriwa kuwa makini kwa kutoa mafunzo mazuri kwa mtoto wake, kumfundisha jinsi ya kujisaidia au jinsi ya kutumia choo. Kinyume na hivyo ni kumfanya mtoto awe na tabia ya kujifanyisha na hivyo kuwa na hali mbaya ukubwani. Mtoto aliyenyimwa huduma hii akiwa katika hatua hiyo hubakiwa na deni, anapokuwa mkubwa anaweza kupata matatizo ya kiakili. Watoto waliokosa huduma hiyo wanapokuwa wakubwa, mara nyingi huwa mashoga, na wengine huwa waoga kufanya mapenzi, lakini mbaya zaidi ni kukosa kabisa hamu ya mapenzi, wengine huwa wazembe na huwa na tabia fulani fulani ambazo zinahitaji msaada mkubwa wa wengine.

Hatua ya tatu – phallic stage: Hatua hii huwahusu watoto wenye umri wa miaka minne. Ni katika hatua hii ambapo mtoto huanza kutambua jinsia yake na hivyo kuwa karibu na mama yake au baba yake. Mtoto wa kiume hupenda kulala na mama yake na mtoto wa kike pia huwa hivyo hivyo hupenda kulala na baba yake (interest of opposite sex). Mtoto wa kiume humchukia baba yake bila kujua na kumuonea wivu mama yake na kuona kama anamfaidi baba yake jambo ambalo hulitaka liwe kwake, pia mtoto wa kike humchukia baba yake na kumuonea wivu baba yake na kuona kama anamfaidi mama yake jambo ambalo hulitaka liwe kwake. Watoto waliokosa kuwa karibu na wazazi wao wa jinsia tofauti katika hatua hii, wengi hupata matatizo, lakini hulipiza kisasi kwa sababu hawakuwa karibu na jinsia tofauti wanapohitaji kufanya hivyo. Usishangae kumkuta binti akiwa kwenye kundi la wavulana au mvulana akiwa kwenye kundi la wasichana.

Hatua ya nne – latency stage: Hatua hii huwahusu watoto wa miaka sita, minane na wakati mwigine mpaka miaka 12, ambapo mtoto macho yake yote huwa katika michezo ya kawaida na kwenda shule. Hakuna kitu cha ajabu kinachotokea katika hatua hii kati ya jinsia ya kike na ya kiume.

Hatua ya tano - genital stage: Hatua hii huwahusu watoto wa kuanzia miaka 13. katika kipindi hiki vijana wengi huanza kubalehe na kuvunja ungo. Katika hatua hii ndipo mtu hukabiliwa na vitu vingi katika maisha yake yote. Huanza kujishuhulisha na kutafuta maisha yake mwenyewe na ndipo hatua nyingine zote huanza kujirudia tena kama hazikufanywa vizuri katika umri huo. Raha ya mwanadamu yoyote katika kipindi hiki huwa ni mapenzi, lakini hutofautiana kiwango cha kupenda au kutamani kutokana na jinsi alivyolelewa katika hatua nne za mwanzo. Nakuomba sana kila unapokutana na watu waongo, wambeya, wakimya, wapenda ngono kupita kiasi n.k. waulize maisha yao ya utotoni.

Sunday, March 22, 2009

NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA WOTE

Anayekataa kufundishwa anajidharau mwenyewe,
Bali anayekubali maonyo hupata busara.

Aendeye kwa unyofu huenda salama,
Bali apotoshaye njia zake atajulikana.

Malezi bora ya watoto wetu ndio msingi imara wa taifa la kesho.

NA PIA

Binadamu tunapanga mipango yetu,
Lakini kauli ya mwisho ni yake Mwenyezi Mungu.

Ana heri mtu yule amsikilizaye,
Akisubiri siku zote mlangoni pangu,
Akingoja penye vizingiti vya milango