Mapera yakiwa mtini na hapo unaweza kujua lipi lipo tayari kuliwa.... kuna wengi wanashindwa kula mapera kutokana na kuwa na .....
....mbegumbegu kama uonavyo hapa...basi ni bora kunywa juisi yake ni tamu sana....Nimeyatamani sana mapera leo....Je kuna tunda wewe umelitamani kwa hivi karibuni?
Showing posts with label tunda la pera. Show all posts
Showing posts with label tunda la pera. Show all posts
Tuesday, October 10, 2017
Tuesday, December 8, 2015
TUNDA LA PERA SIO TUNDA TU ISIPOKUWA :- MAJANI YA MPERA KWA NYWELE ZINAZOKATIKA NA KUPUNGUA
Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika hata kama bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike.
Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika.
Jinsi ya kuyatengeneza kama dawa
Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.
Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.
Ukimaliza fanyia masaji nywele zako kama mtu anayepaka mafuta nywele zote.
Baada ya hapo unaweza kuacha kwa muda kisha ukaosha.
Fanya hivi mara kwa mara, naamini utaona mabadiliko.
Subscribe to:
Posts (Atom)


