Msimu ni ule majira ya kupukutika kwa majani. Kwa hiyo ni msimu wa uyoga pia kwa hiyo wapenzi wa uyoga tunafurahia sana kwenda mstuni na kuchuma/kutafuta uyoga. Kumbuka uwapo msituni sio unachuma uchoga tu ...La hasha ni mazoezi makubwa sana na pia kama ulikuwa na msongo wa mawazo basi msitu ni sehemu nzuri sana na kuwa.
Nawatakieni kila la kheri tuonane tena panapo majaliwa.....kapulya wenu!
Showing posts with label uyoga. Show all posts
Showing posts with label uyoga. Show all posts
Tuesday, October 1, 2019
Tuesday, September 12, 2017
VYAKULA AVIPENDAVYO KAPULYA WENU ...AU KUNA MWINGINE ANAPENDA KAMA MIMI??
NI WALI NA KUNDE...KWETU UNGONINI TWAITA (NGUNDI MANGI)
Baada ya chakula nilipenda sana haya matunda ...kwa mara nyingine tena kikwetu twaita MADONGA....
Nikikosa hivyo basi nakula uyoga....Je wewe kuna chakula hujala siku nyingi na sasa watamani kukila? Nawatakieni wote jioni njema!!!
Wednesday, September 7, 2016
NJIA NZURI YA KUWEZA KUTAFAKARI PALE UNAPOPUMZIKA NI KWENDA MSTUNI ...KAPULYA WENU HUTUMIA MUDA HUO KUTAFUTA UYOGA NA KUTAFAKARI....
Leo ni siku yagu ya mapumziko, na siku kama hii napendakuitumia kwa kwenda mstuni kutafuta uyoga. Ndiyo natafuta uyoga, lakini la muhimu zaidi kwangu ni kunyoosha viungo na bila kusahau kuwa mstuni peke yako ingawa hujui kama upo peke yako ni njia moja ya kufikiri mambo mengine katika maisha. Ila pia kama leo nimepata kitoweo:-)
JIFUNZE KUTAFAKARI KWA KWENDA MSTUNI:-) KWANI NI SEHEMU TULIVU SANA...
Friday, September 13, 2013
MDADA KAPULYA SI MTU WA KUTULIA ..MSIMU WA BUSTANI UNAKARIBIA KWISHA NA SASA WAJA MSIMU KUCHUMA UYOGA NAYE NI MPENZI SANA WA KAZI HII KWA HIYO LEO ALIKWENDA MSTUNI NA HAPA NI MATOKEO YAKE....
Kuchuma uyoga ni kitu ambacho nakipenda sana , unakuwa na wakati mzuri wa kutafakari, pia mazoezi nahalafu unapata mboga ..Mboga hii mimi nimeipata bure leo mstuni lakini kama ningekwenda kuinunua dukani kwa kilo ni kama kwa kila shilinga 23000/= . Nami nilipata lita kama tano hivi. Sasa kazi nyingine unaporudi nyumbani ni kuusafisha na ndio hapo nafanya kutoa mchanga na takataka nyingine,,,,
Baada ya masaa matatu uyoga tayari umetolewa takataka zote na upo safi kwa kuliwa.....
...Uyoga upo kwenye plain pan tayari kwa kuandaliwa kwa ajili ya mlo wa jioni......
.....baada ya dakika tano umepungua kiasi hiki na maji mengi yamejitokeza ..naendelea kukausha maji...
---Maji yamekakamia na hapa sasa ni kuweka chumvi, sukari kiduchu kwa ajili ya ladha..na pilipili manga kidogo na kikubwa zaidi siagi kama kijiko kimoja cha mezani unakaanga kwa dakika kumi....
...baada ya hapo unaweka krimu ya maziwa na kama huna krimu basi weka unga wa ngano kijiko kimoja cha mezani na maziwa kikombe cha chai,,,,
Na mwisho mlo ukapatikana hivi:- Wali, kuku, uyoga uloungwa kama nilivyosema hapo juu ikiwa na nyanya kutoka bustanini kwetu, tango na majani ya ruccula. Na hivi ndivyo ilivyoisha IJUMAA YA KAPULYA na mpishi ni YEYE MWENYEWE KAPULYA:-) TUTAONANA TENA PANAPO MAJALIWA !!

Thursday, August 9, 2012
NIPENDAVYO MSIMU HUU WA JOTO NI KAMA HIVI KWENDA MSTUNI NA KUPATA VITU KAMA HIVI!!!
Hapa ni blåbär/ blueberries kwa kiswahili sijui zinaitwaje anayejua naomba mnisaidie...Basi leo jioni yangu ndo imesiha hivi kwenda mstuni kuchuma ..bluberries unaweza kula kama zilivyo,kula na maziwa, kutengeza keki, kutengeneza kinywaji, kutengeza jam/jelly...nk. ..Halafu nikakutana na ugonjwa wangu.......
...UYOGA..Hakika nikiwa mstuni kuchuma/kutafuta uyoga hakuna mtu anaweza kunipita...nakuwa mawazo yote ni uyoga tu na leo nimepata lita 2...nadhani utakuwa mlo wa jioni hii. Kitu kimoja nipenda wakati huu wa joto hapa ni mambo haya kwenda mstuni na kupata vitu freshi kabisa ...kama NYUMBANI...KARIBUNI TUJUMUIKE....

Tuesday, August 23, 2011
MDADA HUYU /YASINTA SIO MPENZI WA SAMAKI KWA UGALI WA MUHOGO TU BALI ....
Tuesday, August 12, 2008
AGOSTI 12,2008 RAHA YA KUWA NA MISITU
Subscribe to:
Posts (Atom)