Showing posts with label kifo. Show all posts

Friday, March 22, 2013
KWA KWELI SIKU YA KUFA HAIJULIKANI NI MUNGU TU ANAJUA UTAKUFA LINI NA VIPI....
IJUMAA IWE NJEMA KWENU NA TUZIDI KUOMBEANA...
Thursday, January 24, 2013
HABARI YA KUSIKITISHA SONGEA:- MWANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA SONGEA BOYS AJINYONGA
MWANAFUNZI wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wavulana ya Songea mkoani Ruvuma amekutwa amekufa baada ya kujinyonga kwenye mti uliopo kandokando ya njia kwenye eneo la milima ya matogoro ya hifadhi ya msitu ya taifa nje kidogo ya manispaa ya Songea.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma mrakibu mwandamizi wa polisi George Chiposi alisema kuwa tukio hilo lilitokea januari 21 mwaka huu majira ya 12.30 asubuhi huko katika eneo la milima ya matogoro
Kaimu kamanda Chiposi alimtaja mwanafunzi huyo aliyekutwa amekufa baada ya kujinyonga kuwa ni Ahabu Richard Ng’ondya (21) wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wavulana ya Songea ambapo alidai kuwa siku hiyo ya tukio watoto wawili ambao walikuwa wakipita njianimajira ya saa za asubuhi ghafla waliona kama kuna mtu ananing’inia kwenye mti mrefu ambao upo kandokando ya njia hiyo.
Watoto hao baada ya kuona hali hiyo walikimbia na kukutana na mtu aliyejulikana kwa jina la Osward Kahongo walimwonyesha tukio hilo ambaye nae pia aliwasiliana na polisi ambao walifika kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na daktari.
Alisema baada ya polisi kufanya uchunguzi ulibaini kuwa alikuwa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Songea ambaye anadaiwa aliondoka kwenye eneo la shule katika mazingira ya kutoroka siku chache kabla ya kutokea tukio hilo.
Alibainisha zaidi kuwa upelelezi wa awali wa polisi umebaini kuwa chanzo cha kujinyonga kwa mwanafunzi huyo ni kwamba alikuwa amefukuzwa shule na uongozi wa shule baada ya kutofanya mitihani ya majaribio hivyo uongozi wa shule ulimtaka arudi nyumbani kwao Matamba Uwanji wilaya ya Makete mkoani Njombe ili akamlete mzazi wake.
Alieleza zaidi kuwa baada ya kuambiwa hivyo mwanafunzi huyo alitoeka kwenye eneo la shule na kwenda kusikojulikana hadi hapo alipokutwa akiwa amekufa kwa kujinyonga, hata hivyo alieleza kuwa mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Matamba Uwanji nyumbani kwa wazazi wake kwa ajili ya mazishi
CHANZO:- Songea yetu.
Wednesday, November 28, 2012
UPUMZIKE KWA AMANI HUSSEIN RAMADHANI A.K.A SHARO MILIONEA!!
SISI TULIKUPENDA LAKINI MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI UPUMZIKE KWA AMANI TUTAKUKUMBUKA DAIMA.
Thursday, May 31, 2012
SIJUI TUNAKOKWENDA NI WAPI? AU NI SHETANI ANATAWALA?
Najua wengi mtajiuliza mbona alisema AMEFUNGA MWEZI HUU WA TANO kama ilivyo hapo chini. Lakini baada ya pitapita nimeshindwa kuvumilia na habari hizi zimenisikitisha sana na ndio nikaona niziweka tu nazo kwani ni moja ya habari muhimu katika maisha yetu wanadamu.
Mama mzazi wa Mtoto aliye nyongwa Mtotot wake kwa kumuvunjwa shingo akiwa chumba
cha kuhifadhia maiti wakati mtoto akifanyiwa uchunguzi
Dakitari wa hospilata ya Mkoa Ruvuma Dakitari Mchirika akiuangalia mwili wa mtoto/malaika huyu. Masikini mtoto mdogo mwenye umuri wa miaka mitatu akiwa amelala chumba cha kuhifadhia maiti baada ya mama yake mzazi akishirikiana na hawara yake ambao wana tuhumiwa kumua mtoto huyo ili asiwabuguzi wawapo kitandani. Na baada ya mauaji hayo waliahidi kuoana. Hebu angalia watu walivyo hawana huruma akina mama, akina baba, wazee wetu utamaduni wa Mwafirika Mmeuweka wapi ? CHANZO CHA HABARI ni HAPA. Halafu soma na hii HAPA . INASIKITISHA SANA KWA KWELI....
Friday, October 7, 2011
BABA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA KOSA LA KUMSHINIKIZA MKEWE KUNYWA SUMU HADI KUFARIKI
Picha na habari na- Mbeya yetu Blog
Mohamed Mwawipa mwenye Umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Ijumbi kata ya Luwiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya ameshikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa tuhuma za kumshinikiza mkewe kunywa sumu baada ya kumtuhumu kumwibia shilingi laki nne na elfu hamsini.
Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa marehemu Nuru Masuba alikuwa na ugomvi kwa kipindi kirefu na mumewe hali iliyopelekea wakatengana lakini October 4 walirejeana upya mahusiano yao hadi kifo kilipomfika.
Akiongelea tukio hilo mwenyekiti wa kijiji cha Ijumbi John Kalikumoyo amesema mtuhumiwa alikiri kutenda tukio baada ya kuhojiwa na uongozi wa kijiji na kwamba endapo mwanamke huyo asigekubali kunywa sumu angetumia silaha ya jadi aina ya kisu kumuangamiza kama fedha hizo hazitoonekana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alipomuulizwa juu ya kukamatwa kwa Mohamedi Mwawipa alisema kuwa taarifa hizo bado hazijamfikia na kwamba atazitolea ufafanuzi pindi atakapo pata taarifa kamili kutoka kwa mkuu wa polisi wilaya ya Mbarali.
Friday, May 7, 2010
Ijumaa ya tusikilize wimbo huu:- siku ya kifo!!
IJUMAA NJEMA KWA WOTE NA MUWE NA WAKATI MZURI IJUMAA YA LEO. NA PIA WIKIENDI NA TUONANE TENA WAKATI MWINGINE!!
Wednesday, November 11, 2009
POLE KWA MSIBA DA MDOGO KOERO MKUNDI
Nimetoka kazini nimerudi nyumbani, baada ya muda nafungua computer na nasoma ujumbe wenye kicha cha habari NIMEFIWA kutoka kwa da mdogo Koero Mkundi usemao hivi:- DADA KUNA MAPOROMOKO YA MLIMA YAMETOKEA HUKO UPARENI KIJIJINI KWA MAMA YETU NA KUNA WATU ZAIDI YA 20 WAMEPOTEZA MAISHA MIONGONI MWAO KUNA NDUGU ZAKE MAMA YAANI SHANGAZI YAKE NA WATOTO WAO NA MJOMBA PIA WAMEKUFA, HIVYO KESHO NASAFIRI NA MAMA KWENDA UPARENI KUHANI KWANI WAMEZIKWA LEO HII...... WOTE TUKO HAPA NYUMBANI TUNAOMBOLEZA...........ILA BIBI KOERO NI MZIMA TEGEMEO LANGU. Habari zaidi soma hapa.
Friday, March 27, 2009
MAISHA BAADA YA KIFO
Nimesoma mjadala uliowekwa na Shabani Kaluse uliokuwa na kicha cha habari kisemacho "BADO WATU WANA HOFU JUU YA KIFO" Nami nimeona niendeleze mjadala huu kwa mada hii.
Baada ya kifo kinatokea nini?
Kuhusu kifo kuna mitazamo mbalimbali inayotofautiana kadiri ya imani ya mtu. Katika maisha ya binadamu kwa kipindi chote cha maisha yake, amakuea akipambana vikali sana na swali hili: “Baada ya kifo changu kitaendelea nini?” Jibu la swali hili lina maana sana katika maisha yetu hapa duniani, ingawa watu wengi wanaogopa kuongea juu ya jambo hilo. Madhehebu mbalimbali ya dini yamekuwa yakitoa majibu ya swali hili kadiri ya imani ya mapokeo yao.
Wakristo wanaamini nini?
Lakini katika imani hizo zote, tumaini la wakristo ni la uhakika kwa sababu kuu mbili. Moja, Ufufuko wa Kristo na Pili ni ushuhuda wa Maandiko Matakatifu. Biblia inatupatia picha ya kweli na kamili kuhusu kitakachoendelea baada ya kufa. Hata hivyo, wakristo wengi wameelewa vibaya juu ya maisha baada ya kufa. Wengine wanaamini kwamba watakuwa miongoni mwa malaika, wengine wanaamini wataingia katika hali ya usingizi wa roho, wakati wengine wanaamini kwamba watakuwa wanaelea katikati ya mawingu.
Wakristo wanaamini kwamba Kifo sio kitu cha kuogopa, badala yake katika kufa ndipo tutafikia kilele cha maisha yetu yaani kurudi kwa Baba Mbinguni. Kuishi maana yake tunadumu katika nchi ya kigeni. Kifo kimepoteza maumivu yake na sasa kifo ni ushindi kupitia Ufufuko wa Yesu Kristo Bwana wetu.
Wakana Mungu(Atheists)
Wakana mungu(Atheists) wanaamini kwamba mtu akifa ndio mwisho wake. Hakuna maisha baada ya kifo wala kwamba kuna roho ambayo inakwenda Mbinguni na itaendelea kuishi milele. Tunachotakiwa kutegemea maishani ni kwamba kifo hakiepukiki, binadamu lazima afe na maisha ya ulimwengu huu yana mwisho.
Wale wanaoabudu miungu(Pantheistics) wanafundisha kwamba mtu yumo katika mzunguko usio na mwisho na umwisho mpaka mzunguko huo unapovunjika ndipo mtu anakuwa kitu kimoja na mwumba wake. Namna mtu atakavyokuwa katika maisha ya baadaye inategemea namna gani aliyaishi maisha ya awali. Pale mtu anapounganika na muumba wake, palepale anakoma kuwa kuishi kama mtu, ila anakuwa sehemu ya nguvu za maisha matakatifu kama vile tone la maji linalotua Baharini.
Wale wanaoshikilia dini za makabila yanayosema kwamba vitu vyote vina roho(animistic) wanaamini kwamba baada ya kifo roho ya binadamu inabaki ardhini au inasafiri kwenda kuungana na roho zilizotangulia za mababu (wahenga) zilizoko duniani. Kwa milele wanatembea na wanatangatanga katika giza wakikumbana na furaha na huzuni. Baadhi ya roho hizo zilizotangulia zinaweza kuitwa tena kuja kusaidia na kuwatesa wale wanaoishi duniani.
Waislamu wanaamini nini?
Waislamu wanafundisha kwamba, mwisho wa dunia, Mungu atahukumu maisha na kazi za bainadamu. Wale ambao matendo yao mema yanazidi matendo yao mabaya wataingia paradizini. Wanaobaki wataingia ahera. Korani inafundisha kwamba paradizini watu watakuwa wanakunywa divai na kuhudumiwa na wasichana wa mbinguni na baadhi ya wasichana hao watakuwa wake zao.

Sunday, October 19, 2008
MAISHA BAADA YA KIFO
Baada ya kifo kinatokea nini?
Kuhusu kifo kuna mitazamo mbalimbali inayotofautiana kadiri ya imani ya mtu. Katika maisha ya binadamu kwa kipindi chote cha maisha yake, amakuea akipambana vikali sana na swali hili: “Baada ya kifo changu kitaendelea nini?” Jibu la swali hili lina maana sana katika maisha yetu hapa duniani, ingawa watu wengi wanaogopa kuongea juu ya jambo hilo. Madhehebu mbalimbali ya dini yamekuwa yakitoa majibu ya swalihili kadiri ya imani ya mapokeo yao.
Wakristo wanaamini nini?
Lakini katika imani hizo zote, tumaini la wakristo ni la uhakika kwa sababu kuu mbili. Moja, Ufufuko wa Kristo na Pili ni ushuhuda wa Maandiko Matakatifu. Biblia inatupatia picha ya kweli na kamili kuhusu kitakachoendelea baada ya kufa. Hata hivyo, wakristo wengi wameelewa vibaya juu ya maisha baada ya kufa. Wengene wanaamini kwamba watakuwa miongoni mwa malaika, wengine wanaamini wataingia katika hali ya usingizi wa roho, wakati wengine wanaamini kwamba watakuwa wanaelea katikati ya mawingu.
Wakristo wanaamini kwamba Kifo sio kitu cha kuogopa, baada yake katika kufa ndipo tutafikia kilele cha maisha yetu yaani kurudi kwa Baba Mbinguni. Kuishi maana yake tunadumu katka nchi ya kigeni. Kifo kimepoteza maumivu yake na sasa kifo ni ushindi kupitia Ufufuko wa Yesu Kristo Bwana wetu.
Wakana Mungu(Atheists)
Wakana mungu(Atheists) wanaamini kwamba mtu akifa ndio mwisho wake. Hakuna maisha baada ya kifa wala kwamba kuna roho ambayo inakwenda Mbinguni na itaendelea kuishi milele. Tunachotakiwa kutegemea maishani ni kwamba kifo hakiepukiki, binadamu lazima afe na maisha ya ulimwengu huu yana mwisho.

Subscribe to:
Posts (Atom)