Friday, October 7, 2011

BABA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA KOSA LA KUMSHINIKI​ZA MKEWE KUNYWA SUMU HADI KUFARIKI

01.Mtuhumiwa Bwana Mohamed Mwawipa ambaye alimshinikiza mkewe Nuru Masuba kunywa sumu baada ya kumtuhumu kuwa amemwibia fedha taslimu shilingi laki nne na elfu hamsini akionesha askari wa upelelezi eneo alilonywea sumu mkewe

02. Mweyekiti wa kijiji cha Ijumbi kata ya Ruiwa wilaya ya Mbrali Bwana John Mkalimoyo akimfariji dada wa marehemu Nuru Masuba aitwaye Stumai Wilson ambapo marehemu alikuwa akiishi naye Kijiji cha Mapogolo kapunga.

03.Mwili wa marehemu Nuru Masuba aliyeshinikizwa kunywa sumu baada ya kutuhumiwa kumwibia fedha shilingi laki nne na elfu hamsini na Mumewe Mohamed Mwawipa akipelekwa kuhifadhiwa kaburini, baada ya uchunguzi wa daktari na polisi kukamilika.
Picha na habari na- Mbeya yetu Blog

Mohamed Mwawipa mwenye Umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Ijumbi kata ya Luwiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya ameshikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa tuhuma za kumshinikiza mkewe kunywa sumu baada ya kumtuhumu kumwibia shilingi laki nne na elfu hamsini.
Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa marehemu Nuru Masuba alikuwa na ugomvi kwa kipindi kirefu na mumewe hali iliyopelekea wakatengana lakini October 4 walirejeana upya mahusiano yao hadi kifo kilipomfika.
Akiongelea tukio hilo mwenyekiti wa kijiji cha Ijumbi John Kalikumoyo amesema mtuhumiwa alikiri kutenda tukio baada ya kuhojiwa na uongozi wa kijiji na kwamba endapo mwanamke huyo asigekubali kunywa sumu angetumia silaha ya jadi aina ya kisu kumuangamiza kama fedha hizo hazitoonekana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alipomuulizwa juu ya kukamatwa kwa Mohamedi Mwawipa alisema kuwa taarifa hizo bado hazijamfikia na kwamba atazitolea ufafanuzi pindi atakapo pata taarifa kamili kutoka kwa mkuu wa polisi wilaya ya Mbarali.

7 comments:

sam mbogom said...

kifo nikitu cha ajabu sana. mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu.amina.mengi yatasemwa lakini mungu anamakusudi yake mpaka kumwachia dada huyu kunywa sumu kwa kusimamiwa na kipenzi mumewe.kuna kitu cha kujifunza hapa,hasa katika imani zetu .kitu muhimu katika tukio hili,ni kwa kiasi gani mtuhumiwa alivyo pitisha mahakama yake ya kisheria kumshinikiza mtuhuiwa wake anywe sumu kwa madai ya kupotelewa na laki zake,ambazo aliziona hazifanani na thamani ya uhai wa mkewe.tusubiri tuone sheri itasemaje. kaka S.

EDNA said...

mweeeh! Mungu na ailaze roho ya marehem mahala pema peponi.

Yasinta Ngonyani said...

Pole sana wanadungu najua hili ni pigo sana kwa wazazi. dada,mama na kila jamaa- Roho ya marehemu ilale mahali pema.

George Olloo said...

Kwa klwali dada inasikitisha sana

Salehe Msanda said...

Ni hatari.
Pesa inatupelekesha kiasi cha kukosa utu;

Mija Shija Sayi said...

Hatari sana..

Penina Simon said...

Hii nayo kali yaani 450,000/= zinatoa roho ya mtu? Huyu mume alikuwa anampenda kweli?