Nimekaa hapa nikiwaza jinsi enzi zileee nilipokuwa msichana mdogo. Shule moja, Kanisa moja, Hospital moja, gari moja la kijiji. Na hapo gari hilo lilikuwa likisafiri kwa wiki mara moja, na ujue likiondoka kurudi majaliwa. Hii picha haihusiani na maelezo yangu ila tu inafanana sana. Hasa nilipokuwa nikienda shule kutoka kijijini kwetu Kingoli na Litumbandyosi kwa kuchapa mwendo mpaka Peramiho kwa muda wa siku mbili. Alan Ntimba kama unasoma hapa najua nawe unakumbuka sana safari zetu za kwenda shule. Alan Ntimba ni rafiki yangu tulimaliza shule ya msingi pamoja. Kama kuna mtu anajua habari zake TAFADHALI nijuze au wewe mwenyewe Alan. Tulikuwa tukipata gari ambaloi limejaa kiasi hicho bahati sana. Juzi tu nilikuwa nikienda kumsalimia baba mkubwa Litumbandyosi usafiri ni bado yaani barabara si za kuridhisha. Je? hii itakuwa hivi mpaka lini? Au je ule Ujamaa bado upo? Maana naamini ilikuwa vile kwa vile tuliishi sana kijamaa....Mmmmm nawaza tu kwa sauti...
TUPO PAMOJA!