Showing posts with label ugali. Show all posts
Showing posts with label ugali. Show all posts

Thursday, June 22, 2017

MLO WA MCHANA WA LEO:- UGALI,TEMBELE NA DAGAA

 Kuna watu tembele wanaona kama mboga duni sana, wanakosa uhondo kwa kweli. Ni hivi:- kwanza chambua vizuri, kisha osha tembele lako, mimi huwa naanika kidogo lakini kuna wengine wanapika moja kwa moja baada ya kuosha yaani bila kuanika. Weka sufuria/chungu motoni, weka mafuta ya kutosha, maana tembele linahitaji mafuta la sivyo utalichukia na ndio sababu wengi hulalamika matembele sio mazuri, kumbe mapishi duni. Tia kitunguu geuza geuza kisha tia nyanya zako na chumvi kidogo. Nyanya zikiiva weka tembele lako. Ligeuze hapo mpaka linywee weka maji kidogo sana kisha funika, sio sasa ndo utoke....utaunguza. Watakiwa uwe hapo hapo unalichungulia kama limeiva. Ukiona bado ongeza maji kidogooo usiweke maji menge, ukiona linanywea zaidi hapo mambo tayari/limeiva.
Mwisho mwidho kamulia kipande cha ndimu au limau geuza dakika mbili -tatu  tayari kwa kula sasa.
UGALI,TEMBELE NIMEONGEZA NA DAGAA
Weka mezani kama hutakipenda hiki chakula, basi nimeshindwa. NATUMAINI UTAJILAMBA VIDOLE:-) MCHANA MWEMA.

Monday, February 13, 2017

JUMATATU HII IANZE HIVI:- JIKONI LEO UGALI

 Ugali, mchanganyiko wa maharege na viazi  pia matembele
...na hapa ni ugali na mboga iliyoungwa karanga...
Binafsi nachagua ule mlo wa kwanza maharage na matembele kwa vile SIPENDI KABISA MBOGA au CHAKULA CHOCHOTE KILICHOWEKWA KARANGA....Ndiyo maana nimeandaa aina mbili isije nikashinda njaa:-)

Friday, June 24, 2016

NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA ...NYASA HII! CHAKULA AKIPENDACHO KAPULYA

Ugali wa muhogo, Kisamvu, dagaa wabichi na kipande cha samaki tena kichwa...nakwambia hapo ni utamu tu....


Wednesday, June 15, 2016

NIMEOTA NDOTO NIPO LUNDO/NYASA NAKULA UGALI KWA SAMAKI NA KISAVU... MLO AUPENDAO KAPULYA...

Nilipoamka kumbe sio...maana hapa nilipo hata unga sina wa kusonga huo ugali sina. Nitabaki kula kwa macho tu......Ngoja nikatafute unga......

Sunday, May 8, 2016

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JIONI HII YA JUMAPILI YA LEO KWA MLO HUU...

UGALI, KACHUMBALI NA SAMAKI WA KOKA
Mwenyezi Mungu na aubaribi mlo huu na watakaokula nao pia washibe na kupata baraka zake. JUMAPILI NJEMA SANA PIA JIONI NJMEA. KAPULA/KADALA

Monday, August 24, 2015

KARIBUNI TUJUMUIKE: UNAKUMBUKA ENZI HIZOOO UTOTONI HASA KWENYE MSOSI???

Chakula tayari ni watu wanakosekana kuushambulia msosi huu mtamu...Mimi hapo hizo dagaa ndo natamani kwelikweli-------Kapulya !

Friday, June 26, 2015

MLO HUU NIMEUTAMANI SANASIKU YA LEO:- UGALI, SAMAKI WA KUKAANGA NA MLENDA/BAMIA

Ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi huu wa sita, Yaani hata siamini mwezi huu ulivyoisha haraka. Na katika siku hii ya leo ningependa sana kula mlo huu, Je? wewe ungependa kula nini siku hii ya leo au nawe kama Kapulya. IJUMAA NJEMA PIA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA:-)

Saturday, April 25, 2015

KARIBU:- KUNA USHIBE!!

Naanza bila mpango, Kwa tenzi pia na tungo,
Niyafumbue mafumbo, Ugali na mbogamboga.
Wanadharau mapishi, Wanayabeza mapishi,
Mapishi ya Waswahili, Ugali na mbogamboga.
Umeyasifu matango, Mazuri sana kwa macho,
Huleta ngozi nyororo, Ugali na mbogamboga.
Na uyoga asilia, Kushiba bila ya kula,
Nashiba na kutazama, Ugali na mbogamboga.
Ugali huo wa sembe, Sembe nyeupe pepepe,
Na dona usiutupe,Ugali na mbogamboga.
CHANZO : KWA MJENGWABLOG

Monday, March 2, 2015

JUMATATU HII YA KWANZA TUANZE NA KUKARIBISHANA CHAKULA CHA MCHANA ...

Ni chakaula ambacho akipendacho sana Kapulya/dada mkuu...ni ugali samaki, maharagwe, na mbogamboga...KARIBUNI TUJUMUIKE:-

Friday, February 20, 2015

KARIBU CHAKULA CHA MCHANA ILA MJE NA MBOGA!!!

Maana mie mwenzenu nakula bila mboga wangono wanasema ("ugali wa kisuma")  au umewahi kula ugali na maji yaliyowekwa chumvi tu...
BASI NIWATAKIENI SIKU NJEMA NA TUONANE TENA PANOAPO MAJALIWA!!

Monday, September 8, 2014

MWENZENU NIMETAMNI KWELI MLO HUU JIONI YA LEO...DUH MATE YANACHURUZIKA TU HAPA...

Sina jinsi nimebaki kutamani tu leo maana nimeishiwa unga ... halafu ebu angalia  hayo maharage mabichi ...ila inakosekana mboga majani maana mimi na mboga damudamu.....je wewe utakula nini jioni hii au sijui mchana  huu?

Thursday, February 6, 2014

HII KWA KWELI ITAKUWA PICHA YA WIKI...UGALI KWA NYAMA PANYA !!!MMMMHHH KAZI IPO!!!

Ni muda mrefu nimekuwa nikisikia ya kwamba nyama ya panya na nyoka ni tamu kama ya kuku. Na pia nimesikia katika habari ya kwamba baaada ya miaka wadudu wote watakuwa kitowoe kizuri sana kwa binaadamu. Swali moja kutoka kwa kijana wangu linaulizwa hivi:- Iweje tule panya wakati anatuletea magonjwa? Na je nyoka si adui yetu na pia ana sumu?

Monday, August 26, 2013

HUU NI MCHANA MWINGINE YA JUMATATU .....KARIBU TUJUMUIKE HAPA JAMANI....

Picha hii imenikumbusha mbali sana huu ni mtindo mzuru sana kula hivi sahani moja ....Ila kuna kitu kimoja kilikuwa kinanishinda hapa nilikuwa nakula taratibu mno na ninaposhtuka ugani umeisha. Ni mtindo mzuri maana hapo ndipo wote mnaweza kukusanyika na kuongea pia ila si sana maaana kila mtu anakuwa hana nafasi ya kuongea.....isipokuwa kushiba....Je nawe msomaji unakumbuka hii?
JUMATATU NJEMA!!!!

Wednesday, December 5, 2012

MCHANA WA LEO NINGEPATA MLO KAMA HUU NINGEFURAHI SANA LAKINI SASA ITANIBIDI NILE KWA MACHO....

Ni ugali kwa mlenda uliochanganywa kwawa majani ya maboga na ambayo bamia. Halafu  bakuli la (ma)tembele la kuchemshwa kwa nyanya na kitunguu. Bila kusahau pilipili shamba.
Hakika hapa ni utamu, na tena ule wa asili kabisa ,yamu yamu yamu....NAWATAKIENI WOTE SIKU /JUMATANO NJEMA SANA.

Monday, October 1, 2012

NIMEUTAMANI KWELI MLO HUU UNGEKUWA MLO WANGU WA JIONI HII!!!

ila nitashindwa kwa vile kitu kikubwa zaidi ni kwamba sina unga ....mwisho nimebaki kumezea mate tu..hasa huyo samaki wewe acha tu...picha toka http://barakachibiriti.blogspot.se.
Nawatakieni kila la kheri au sijui jioni,mchana, asubuhi au usiku mwema.

Saturday, August 11, 2012

TUMALIZE JUMAMOSI HII KWA MLO HUU:- UGALI KWA MLENDA/BAMIA HALAFU KUKU!!!


UGALI WA MAHINDI
MLENDA /BAMIA AMBAYO HUPIKWA KWA KUCHANGANYA NA MBOGA YA MABOGA..Msiogope,,,yaani ugali na mletu tu ....hapana
atachinjwa na huyu jogoo akijitokeza mchinjaji kwani mwenyewe naogopa...Kwa hiyo jitokezeni ...
KARIBUNI SANA..KWA WENGINE SASA NI ASUBUH, WENGINE MCHANA , WENGINE WANAENDA KULALA NA HAPA SASA NI MUDA WA KUPIKA CHAKAULA CHA JIONI KWA HIYO KARIBUNI SANAAAAA....

Saturday, December 3, 2011

NATAMANI NINGEPATA MLO HUU MCHANA WA JUMAMOSI HII LAKINI....SINA. SIJUI NIFANYEJE?

UGALI......




......KWA DAGAA´


Nimepita mara mia kwa dada Rachel na kumezea meta au kujaribu kula kwa macho na nimeshindwa maana nina unga lakini sina dagaa...

JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE HATA KAMA BILA UGALI NA DAGAA:-)

Friday, January 21, 2011

JAMANI MWENZENU YAMENIKUTA LEO TENA NIMETAMANI KWELI HIKI CHAKULA KITAMU CHA NYUMBANI!!!!

Mlo huu sijala muda mrefuuuu!!
Jamani mwenzenu niko katika msimu mbaya sana, UNGA wa ugali umeniishia. Na nimepita kila duka, nimepata unga lakini ni wa njano PALENTA kwa aliyezoea ugali kama mimi haunogi kabisa. Kwa hiyo nilipoiona picha hii mate wacha yanidondoke. Hali hii inanifanya niimbe wimbo huu NARUDI NYUMBANI EEEH, NARUDI PERAMIHO, NARUDI SONGEA NAKWENDA KULA LIKOLO LA NANYUNGU..... Au labda tuusikie mwimbaji mwenyewe akiimba Marehemu Dr. Remmy Ongala


NA JAMANI IJUMAA NA MWISHO WA JUMA MWEMA. TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE!!!

Thursday, July 29, 2010

Nipo likizo na pia nimekuwa mkulima wa bustani na hapo mnaona matokeo yake!!

Mkulima ni mmoja na walaji ni wengi
Hapa mnaona matunda ni mboga ya maboga tena ile ya ubenani (Nyamuza)


Karibuni wote tujumuike kula ugali na mboga ya maboga na hapo kwenye boxi ni mchicha kwa hiyo likizo nzima ni mbogamboga tu na bila kusahau nitakuwa naweka akiba kwa wakati wa baridi. LIKIZO INAENDELEA NA TUNAPATA MVUA NYINGI SANA HAPA MWAKA HUU. TUTAONANA WAKATI MWINGINE KILA LA KHERI. NA KUMBUKENI SISI SOTE NI NDUGU.


Thursday, May 6, 2010

LEO NIMETAMANI KWELI HIKI CHAKULA KITAMUCHA NYUMBANI!!!!

Dagaa,ugali, samaki na ndizi,
mlo huu sijala muda mrefuuuu!!

Jamani mwenzenu niko katika msimu mbaya sana, mwaka jana nilichukua UNGA wa mahindi lakini sasa umeniishia. Na nimepita kila duka, nimepata unga lakini ni wa njano PALENTA kwa aliyezoea ugali kama mimi haunogi kabisa. Kwa hiyo nilipoiona picha hii mate wacha yanidondoke. Hali hii inanifanya niimbe wimbo huu NARUDI NYUMBANI EEEH, NARUDI PERAMIHO, NARUDI SONGEA NAKWENDA KULA LIKOLO LA NANYUNGU.....