Showing posts with label kujitegemea. Show all posts
Showing posts with label kujitegemea. Show all posts
Saturday, May 11, 2013
PICHA YA WIKI..MAMA NISHUCHE NATAKA KUCHEZA...
Inaonekana mtoto hataki kubebwa au sijui kaona kitu fulani anataka akachukua??? Au wenzangu mwasemaje? ...mmmmhhh nimetamani mchicha na chaina hiyo ngoja nami nianze kulima bustani yangu...JUMAMOSI NJEMA..
Monday, March 5, 2012
JE? HAPA BORA ELIMU AU ELIMU BORA?
Picha hii imenirudisha mpaka enzi nipo shule ya msingi. Naweza kusema mie nilikuwa na bahati kwa vile baba yangu alikuwa mwalimu, tulikuwa tukiishi nyumba za shule ambazo zilikuwa karibu sana na shule. Lakini kulikuwa na wanafunzi walikuwa wakiishi mbali sana, na mwanzo wengi walikuwa wakishinda na njaa. Ila baadaye ndo wakagundua mtindo huu ya kwamba walikuwa wakichukua mboga na unga na shule ilijenga jiko wakawa wanapika pale shuleni. Ila ilikuwa kazi yao kuangalia kuna kuni maji na kadhalika.Ama kweli maisha ni kujitegemea nikawa najisemea mwenyewe!!! Halafu nikawa najiuliza kweli hawa wanafunzi watasoma kweli au watakuwa wanafikiria jinsi ya kuanza kupika? halafu pia kusoma bila kula nako si vizuri.....maswali mengiiiiiiii....tujadili pamoja...
Thursday, December 8, 2011
KUJIFUNZA/KUJITEGEMEA MAISHA/KAZI ZA NYUMBANI!! AU MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO!!
Friday, November 11, 2011
NAPENDA KUWATAKIENI MWISHO WA JUMA HILI NA WIMBO HUU USEMAO MAISHA NI FORENI NA BONY MWAITEGE!!
IJUMAA NJEMA KWA WOTE na Tuwa na imani katika maisha tusikate tamaan na matokeo yake siku moja yatatokea. Pia nachukua nafasi hii kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunifikisha /tufikisha tarehe hii ya leo ambayo namba zake ni:- 11/11/11 AHSANTE MUNGU KWA KUWA MWEMA KWETU.
Tuesday, December 7, 2010
Elimu/kujitegemea na ushirikiano kati ya wanafunzi na wazazi!!.
Sokoni/Julmarknad!!Wikiend iliyopita ambayo ilikuwa kama ifuatavyo. Sasa tuendelee:- Wanafunzi wa darasa la sita ambalo binti yetu naye anasoma wanataka kufanya safari (skolresa) darasa zima ili kuona mazingira mengine. Na safari kwa kila mwanafunzi ni 700kr ni sawa na 140000Tsh.
Wakawa wanajiuliza tufanyeje ili tupate hizi pesa?. Mmmh! Tuchangishe pesa kila mtu/kichwa kitoe 700kr Hapana, tupite kuuliza kila nyumba kama tunaweza kusafisha magari , Hapana.
Bahati nzuri sasa ni kipindi cha majilio(christmas) na wikiend hii iliyopita kulikuwa na soko kwa ajili ya christimas (Julmarknad) basi wakapata wazo kuwa watushirikishe wazazi kutengeneza chochote kile kama vile keki, pipi, kuoka mikate, kutengeneza Kanawa, chai, chokleti nk. Hakika hutaamini jinsi wazazi tulivyo/walivyowaunga mkono, wacha kazi za kuoka zianze...... binafsi nilioka mikate kama 100 vile.
Na baada ya kuoka ikabidi wazazi na watoto/wanafunzi waende sokoni jumamosi na jumapili siku ya mapumziko. Tukaacha shughuli nyingine na kumbuka hii shughuli itafanyika nje na baridi sio mchezo. Hilo halikuwa tatizo Kabila wazazi na watoto tulikwenda huko sokoni (julmarknad) na Kuuza hivyo vitu ili watoto wapate ppesa na kuweza kufanya safari (skolresa) yao. Kwa kweli huu ni mfano ambao kama sisi waTanzania tungeiga nina imani tungekuwa na maendeleo. Sio kila kitu kutaka kupata kwa mteremko tu. Ebu ingia hapa na usoma makala hiii inafanana sana Milano yako na huu.

Monday, March 23, 2009
KUJIFUNZA KUPIKA UGALI+KUJITEGEMEA+KUMSAIDIA MAMA
Monday, October 27, 2008
SIO KUSUKA MIKEKA TU HATA KUKAA SIKU NZIMA KUSUBIRI WATEJA NI MOJA YA KUJITEGEMEA
Monday, October 13, 2008
KUJITEGEMEA
Tuesday, September 30, 2008
KAZI+USAFIRI NA KUJITEGEMEA
Bila kuvuka hapa basi hafiki nyumbani ,ila ningekuwa mimi sijui kwani nahisi kuna mamba hapa.Thursday, August 14, 2008
AGOSTI 15, 2008 MAISHA YANGU
Kila nikiwaza sipati jibu, kwani maisha yangu ni tofauti sana na ndugu zangu. Mara nyingine naona kama nimetokea hewani (yaani sina ndungu na pia sina mama wala baba) niliondoka nyumbani mapema. Nikiwa na miaka 16, nilianza kujitegemea mapema sana kuliko ndugu zangu. Sijaishi sana na wazazi wangu na sijawategemea sana. Sijafaidi kuwa mtoto wao kama mwenzangu. Na pia sijawategemea sana kwa jambo la uchumi ila kwa namna nyingine. Yaani kama nilivyokuwa shuleni nilipata pesa za matumizi labda kama 200-500Tsh, na hiyo ilikuwa ni matumizi ya mwezi mzima au zaidi. . Wakati nilikuwa mdogo nilikuwa na kanga upande mmoja, vyupi viwili, magauni mawili moja la kuchezea na moja la jumapili. Nilikuwa narithi magauni ya mama, anapunguza na ananishonea mimi. Viatu nilikuwa nasikia jina tu nikipata ndala (za matairi ya gari) nilikuwa najisikia kweli. Fikiria mwenyewe kwenda mstuni kutafuta kuni bila viatu. Unachomwa na miba, unaweza kukanyaga nyoka n,k. Sio kusema wazazi wangu hawakuwa na uwezo hapana. Ila hawakuona kama ni muhimu watoto kuwa na vitu vingi. Pia nilipokuwa mdogo mambo ya kunywa soda, kula pipi hayakuwa kabisa kichwani mwangu. Kwani hatukuzoeshwa Sio kusema maisha yangu yalikuwa mabaya hapana. Mahitaji muhimu nilipata kama kawaida. Lakini sasa watoto wengi hawaridhiki na gauni/shati au suruali moja. Pia wanataka viatu. Na halafu wanataka kila mtu na chumba chake cha kulala. Mimi nilikuwa nanalala chumba kimoja na kitanda kimoja na kaka yangu . Kila mtu alionyesha kichwa upande wake. (mzungu wa nne) Lakini leo mdogo/ndugu zangu wana karibu kila kitu. Kwa jambo hili mara nyingi najisikia nipo peke yangu hapa duniani.
Maisha yangu kwa ujumla hayajawa rahisi. Kipindi kile nasoma kuwa karani nilipata shida sana mimi, asubuhi nilikuwa naamka kuandaa chai na baadaye kwenda shule kwa mguu labda kama saa moja au dakiki 45 hivi. Mchana nilikuwa nabaki shuleni, kwani mwanzoni nilikuwa narudi na sikupata chakula. (Bali ilikuwa kwenda kuchota maji unajua tena foleni kubwa.) Niliporudi na maji kuanza kuandaa chakula, na baadaye muda wa kurudi shuleni umefika. Basi ni kugeuza tena tu bila kula kwani ningekula basi ningechelewa. Nilikuwa naishi kwa "ndugu" lakini nilikuwa kama MFANYAKAZI (mama wa nyumba alikuwa mkatili mno sio mchezo). Jioni baada ya shule kufika tu bila kula kitu amekwishaandaa mahindi kwenda kusaga na niliporudi tu ni kuchukua ndoo kwenda kuchota maji na pia kuandaa mboga. Usidhani hapakuwa na watoto wao, walikuwepo. Lakini walikuwa wanacheza, kufanya homework au walikaa tu. Kila siku hivyohivyo kwa muda wa miaka 2. Labda ndio maana maisha yangu sio kama ndugu zangu, na ndio maana sikuweza kufanikisha masomo yangu vizuri. Kwa namna nyingine namshukuru (mama wa nyumba) amenifundisha jinsi ya kujitegemea, kuishi peke yangu. Ila jamani tembeeni mwoone mmh maisha ni safari ndefu.

Subscribe to:
Posts (Atom)