Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

Wednesday, November 14, 2012

UMESHAWAHI KUCHEZA MCHEZO HUU?!!

Maisha siku zote huwa tofauti toka ulipokuwa mtoto hadi kufikia uzeeni. Hatua hii hupitia mambo mbalimbali haswa za kimechezo. Nakumbuka nilipokuwa mtoto tulicheza michezo mingi ya heshima tofauti na watoto wa sasa hivi.  Haya yote yanasemekana ni kutokana na utandawazi ambao huwajengea watoto ufahamu zaidi.
Huu ni mchezo wa Kuruka kamba ambao tuliucheza utotoni na pia kiafya una umuhimu. Michezo mingine ni Kombolele(Mchezo wa kujificha), Utengenezaji wa magari, Ndege wakati wa mavuno, Midoli ya kutengeneza,  Kula mbakishie baba, Kutengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia udongo, ukutiukuti, Kioo Kioo, mdako mpira (lede ledesta) ,Kujipikilisha....................................pia katika mchezo huu wa kuruka kamba nakumbuka tulikuwa tukiimba  hivi:- Kamwambie baba baba sisi tunacheza cheza hatuogopi fimbo fimbo mtoto acha kuningínikax2.....
Sijui ndo uzee naona kama nimesahau basi tusaidiane kukumbushane ......!!!!!!!!
Tafakari juu ya mtoto wako ingawa sasa hivi tunawanunulia vitu vya kuchezea ila wanavitumia ipasavyo na halafu vinakuwa vingi mno. Nimekumbuka sana michezo hii ya utotoni ..je? nawe unakumbuka kitu?
MAISHA NA MAFANIKIO INAWATAKIA WOTE JUMATANO NJEMA SANA!!! DAIMA PAMOJA.




Saturday, April 21, 2012

JUMAMOSI NJEMA JAMANI!!! WANDUGU WANGU:)

Tazama  jinsi ilivyo veme, ndugu wakae pamoja kwa umoja Zab 133:1
Michezo huleta burudani na kujenga miili yetu. Itusaidie pia kuleta umoja na mshikamano kati yetu; badala ya sokomoko, chuki na fitina.

Monday, January 9, 2012

HABARI ILIYONISIKITISHA...MICHEZO NI YA WATOTO AU WAZAZI?

Jana jini nikiwa nasikiliza taarifa ya habari. Kukawa na habari ya michezo ya watoto. Ni mchezo wa innebandy/floorball, mtoto huyo mwenye miaka 10 jina halikutajwa baada ya mchezo timu yake ilishindwa. Na hapo baba yake mzazi alikasirika, na kumwacha mtoto huyo nje akiwa na jezi tu na wakati nje kulikuwa na baridi. Baada ya muda mzazi mwingine alikuwa akipita akamwona yule mtoto akamchukua na kumpeleka kwao. Usiku wote nikawa nafikiria na kujiuliza hivi hii michezo ni kwa ajili ya watoto au wazazi?

Monday, October 17, 2011

MICHEZO/HIVI NDIVYO WIKIENDI YANGU ILIVYOKUWA!!

Kuwa na watoto ni raha sana, ila kua wakati unaweza kusema kaaazi kwelikweli. Maana hakuna kupumzika. Kama uonavyo hapa hivi ndivyo wikiendi yetu ilivyokuwa da´Camilla alikuwa katika mechi, hapa yeye ni huyo karibu na kipa huyo mwenye jezi nyeupe na nywele nyeusi ...bahati mbaya timu yake ilishindwa ila kwa kweli walijitahidi na mchezo ulikuwa mzuri sana. Ni handboll/mpira wa mikono.

Friday, October 7, 2011

MICHEZO: MPIRA WA MIGUU SWEDEN FINLAND 2-I!!

Jioni hii kulikuwa na mechi katio ya Sweden na Finland na Sweden imeshinda na mabao 2. na Finland 1. Mechi/mchezo ulichezwa nchini Finlanda. Hongera Sweden!!!!

Saturday, June 18, 2011

Erik Klaesson; kinda wa Tanzania aliyeko Sweden

Erik akiwa uwanjani na mpira


“Soka letu linaumwa. Kwahiyo vijana wadogo kama hawa ni tiba kubwa ya soka letu, tuwekeze kwao.” Haya ni maneno ya Waziri wa Habari na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi wakati akizindua michuano ya Copa Cocacola mwaka huu katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Wakati akizungumzia vijana hao ambao walidhihirisha kwamba nchi yetu imejaliwa vipaji vingi sana vya soka, ndipo upesi nilimkumbuka kijana mdogo kabisa Erik Klaesson, ambaye amejaliwa vipaji vingi maishani mwake, ikiwemo soka.
Ukimtazama umbile lake unaweza kumfananisha na aliyekuwa kiungo mahiri wa Pamba ya Mwanza, Simba ya Dar es salaam na Taifa Stars, Hussein Amani Masha.
Lakini sura yake inakuvuta na kumfananisha na beki mahiri David Luiz wa Chelsea ya England. Erik Kalesson anafanana na beki huyo Mbrazil kutokana na kuwa na nywele nyingi (Afro) ambapo mwandishi wa makala haya anamwita jina la utani, Ras Erik (kwa lugha ya Kiswidi, tamka Irik).
Bila kujali umri wake, anachokuambia kijana huyu utabaini kuwa amejengwa katika misingi imara ya soka. Nilimuuliza juu ya wanasoka mahiri wa Sweden, alisema, “nilipenda kumwangalia Henrik Larsson akicheza hapa Sweden, lakini amezeeka na sasa tunamtazama Zlatan Ibrahimovich, nami nimfikie.”
Anaongeza kwa kusema, “nawapenda Robinho, Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Zlatan. Nataka kuwapiku”
Erik Klaesson mapema Jumanne katikati ya wiki alikuwa kwenye mechi za watoto kati ya timu yake ya IFK Skoghall dhidi ya timu ya Norrstrands IF Rod, zote za Sweden.
Uwezo wake kumiliki mpira ni mkubwa kulingana na umri wake. Anaweza kucheza kwa ufasaha beki wa kushoto na kiungo nambari 10. Hii ni kutokana na kasi, chenga na ujuzi wake unaojitokeza tangu akiwa kinda.
Harakati zake za kucheza soka zinamfanya kuwa na ndoto za kuchezea klabu mashuhuri AC Milan ya Italia. Kinda huyu anaeleza wazi hisia zake kwamba hapendi kucheza soka la kulipwa nchini Sweden anakoishi sasa, kwani amepania kucheza nje ya nchi hiyo. Na mawazo yake yanaelekea kucheza ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A, pindi umri wake utakaporuhusu.
“napenda kucheza je ya Sweden hasa Milan. Kama nitaanzia hapa Sweden basi nitachezea timu ya Malmo, naipenda sana,” anasema Erik.
Mwandishi wa makala haya alimuuliza Mama yake, Yasinta Ngonyani juu ya kinda huyo kuchagua timu ya taifa kati ya Sweden au Tanzania.
Naye bila kusita alisema, “Binafsi napenda miaka ijayo achezee Tanzania. Lakini ni ngumu kwa sasa kuzungumzia kwani ana vipaji vingi. Kwa mfano ana kipaji cha kucheza Floorball na Fiddle.”
Hata hivyo aliongeza kwa kusema, “Yeye (Erik) atachagua ni timu gani anataka kuchezea kati ya Tanzania na Sweden, akitaka ushauri wetu atapata, nadhani unajua nipo upande gani hapo.”
Suala hili na wimbi la makinda wengi kukumbwa na tatizo la kuchagua nchi za kuchezea linaendelea kushamiri huku baadhi yao wakiwa na mabadiliko ya uamuzi kulingana na hali halisi inayowatokea wanapochezea nchi fulani.
Kwa mfano mshambuliaji wa klabu ya Sevilla ya Hispania Frederick Kanoute aliichezea timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa, lakini aliamua kuacha kisha kuchezea timu ya taifa ya wakubwa Mali, ambako ni asili ya wazazi wake.
Mwingine ni Danny Wellbeck ambaye anachezea timu ya taifa ya vijana ya England na ameshachezea timu ya wakubwa ya nchi hiyo kwenye pambano la kirafiki dhidi ya Denmark. Hata hivyo anaweza kuchagua kuchezea England au Ghana.
Wengine ni Kevin-Prince Boateng ambaye alizaliwa Ujerumani na kuamua kuchezea Ghana ambako wametokea wazazi wake, pia nduguye Jerome Boateng aliamua kuchezea timu ya taifa ya Ujerumani badala ya Ghana.
Lakini kwa upande wa kinda huyu Erik Klaesson moja kwa moja anaweza kuiwakilisha Sweden kutokana na uraia wa kuzaliwa na baba yake, lakini anaweza kufanya uamuzi wa kuchezea Tanzania kutokana na asili ya mama hivyo kuukana uraia wa Sweden.
Uwezekano wa hili la pili ni mkubwa kwakuwa Erik Klaesson amekuwa akiwasili nchini mara kwa mara ndipo ndoto ya kuanzisha timu yake pindi akistaafu soka, ilipoanza kumea. Na vilevile msukumo wa baba yake ambaye ni mpenzi mkubwa wa Tanzania na amekuwa akimweleza kijana huyo umuhimu wa nchi hii.

Akizungumzia, mawazo ya mwanaye miaka ijayo alisema, “huwa anasema anataka kuanzisha timu yake Tanzania pale atakapokuwa mkubwa na ana ndoto nyingi nasi tunazifuata.”
“kuna kipindi alikuwa akienda sana kwenye mazoezi ya Fiddle, lakini akatuambia akili yake inafikiria mpira wa miguu 100% na anahitaji msukumo wetu.”
“nina hamu sana kumwona (Erik) akicheza mpira wa miguu hata kama hatavaa jezi za AC Milan kama anavyoazimia, muhimu ni kucheza mpira wa kulipwa nje ya Sweden, nasi tunakubali hilo.” Anasema Torbjorn Klaesson, baba wa Erik.
Akaongeza kusema, “nikimtazama mtoto huyu (Erk) naamini atakuwa moto wa kuotea mbali, kwanza anabidii, utulivu wake na uwezo wake anapokuwa na mpira. Walimu wake wananiambia subiri matunda kwa kijana wako muda si mrefu.”
“napenda mpira kupita kiasi, na Sweden unajua tunavyompenda Henrik (Larsson) tangu akicheza Glasgow Rangers kule Uskochi (Scotland) na baadaye Barcelona kule Hispania na kidogo Manchester United. Alikuwa na uwezo mkubwa na anajituma, nami sikujua kama nitapaja kijana mwenye kipaji cha soka, lakini naambiwa nivute subira, namuunga mkono,” anasema Torbjorn Klaesson
Alipotokea Erik Klaesson
Kinda huyu kwa sasa ana miaka 11. Alizaliwa tarehe 3/6/2000 nchini Sweden. Ana kipaji kikubwa cha kucheza soka, na michezo mingine kama floorball /innebandy.
Kama tulivyoona hapo mwanzo, baba yake ni Torbjorn Klaesson, raia wa Sweden na mama yake ni Yasinta Ngonyani, ambaye ni Mtanzania na mzaliwa wa Songea mkoani Ruvuma.
Jambo moja kubwa ni kwamba baba wa kijana huyu anapenda mila na desturi za Mtanzania, na hana shaka juu ya mwanaye endapo atachagua kuwakilisha Taifa Stars miaka ijayo.
Kutokana na yeye kuishi na kufanya kazi kwa muda mrefu hapa nchini, suala ambalo anatoa kipaumbele kwa kijana wake ni kumhimiza kutimiza ndoto zake.
Kwa sasa kinda huyu analelewa kwenye kikosi cha timu ya IFK Skoghall ya Sweden ambako anajifunza mambo mengi kuhusu soka. Ni umri huu ndiyo unakuwa tiba kwa wanasoka mahiri ulimwenguni, hivyo kauli ya Waziri wa Habari na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi kuhusu kuwalea vijana inatakiwa kuungwa na mkono.
Kwani tayari tunaye kinda Erik Klaesson mwenye asili ya Tanzania anayekuja juu kisoka aliyeko nchini Sweden. Kazi kwao TFF.
Na Markus Mpangala, shukrani nyingi zikufikie.Gonga hapa kumsoma habari zake nyingie Nyasa na hapa .

Tuesday, March 22, 2011

MICHEZO YETU!!


Netiboli....
Leo nimeamka na mawazo yangu yamefika hadi Lundo pia Kingoli wakati nasoma shule ya msingi. Nilikuwa mchezaji mzuri sana wa netiboli tena nilikuwa mfungaji magoli yaani mchezo huu ni raha kweli. Najiuliza sijui bado unachezwa mashuleni bado au?

Saturday, March 12, 2011

PICHA ZA WIKI HII:- KIDUKU...........

Picha hizi nimetumiwa na kaka yangu wa hiari Shabani Kaluse na katika picha hizo kuna shangazi yangu wa hiari mwanaye Kaka Shabani ni huyu kijana mwenye T-shirt nyekundu. Anaitwa Abraham.
Alianza huyu.....
Kisha huyu.....

Baadaye mweh....

Weweee..toka hapa

Subiri weweeeeeeeeee...

Ngoja tupige picha ya pamoja...
NAWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA NA MAPUMZIKO MEMA PIA TUTAONANA WAKATI MWINGINE!!!!!

Tuesday, January 25, 2011

UNAKUMBUKA MICHEZO KAMA HII?

Nimekumbuka michezo kama hii nilipokuwa mdogo, maana katika familia yetu watoto wa kiume ni wengi zaidi kwa hiyo tulikuwa hawanibagui katika michezo....haya wewe je uliwahi kusafiri na gari kama hili????:-) brrrrrrrrrrrrrrr kanyonyonyooooooo twendeeee....

Tuesday, October 26, 2010

Hawa ni ndio wacheza mpira watarajiwa!!

Hapa ni Erik mwaka huu mwezi wa nane anavyoufurahia mpira.
Na hapa ni shangazi zangu nao hawapo nyuma. Hawa ndio wale wanawake wa shoka Picha kutoka hapa

Na hapa nadhani wote mnakumbuka huu wimbo wa dada Shakira ebu sikiliza:-)

Saturday, August 28, 2010

Kumbukumbu:- Swali la leo nadhani wengi wetu tumecheza michezo hii tulipokuwa watoto au?

Wengi tumecheza michezo hii!!
Ndiyo, Ndiyo!! ndugu zanguni ngoja leo tukumbuke ya kale .. kuna michezo mbalimbali ya utoto ambayo ilikuwa ni burudani, vituko na wakati fulani ilizaa urafiki wa kudumu sana. Michezo ambayo watoto wetu leo hii wanaweza kuona kuwa haina maana tena na wamebakia kucheza na computer, TV nakadhalika.

Kombolela au rede
Kioo kioo
Ukuti ukuti
Kuruka kamba
Hiki na Hoko
Namtafuta rafiki
Tiari bado (mchezo huu ungepigwa marufuku!!!)
Kitambaa changu cheupe
Tukuone maringo yako!
Watoto wangu eh

Upi uliupenda na kwanini?
Kama kuna mchezo nimeusahau unaweza kuutaja.
Jumamosi njema wote!!

Friday, September 11, 2009

MICHEZO NI MOJA YA MAISHA HAPA NI HUKO HACHIOJI TOKYO

Hapa ni Mtanzania mwenzetu aliyekuwa kwenye mashindano ya karate huko Hachioji Tokyo Japani. Akipokea cheti.

Hapa akina dogo wakiwatoana jasho.

picha ya tatu akina dada nao hawapo nyuma .

Saturday, April 11, 2009

UBUNIFU WA MICHEZO +KUWAFURAHISHA WATOTO


Tazama hapa mtoto alivyo na furaha kwa mchezo huu wa kukaa kwenye plastiki chakavu na kuvutwa na kamba kama yupo kwenye gari vile. Lisifuni jina lake kwa michezo, mwimbieni kwa ngoma na zeze. Zab 149:3

Friday, October 31, 2008

TUFUNGE MWEZI KWA MICHEZO

Basket, huu ni mchezo wangu ambao naupenda kuliko michezo yote. Na nilipokuwa msichana mdogo nilikuwa naufaidi kweli lakini sasa mmh uzee.