Showing posts with label matunda. Show all posts
Showing posts with label matunda. Show all posts

Wednesday, May 29, 2019

VYAKULA/MILO AIPENDAYO KAPULYA

Chakula cha asubuhi mayai, soseji na vinginevyo na bila kusahau matunda kama papai, nanasi na  zabibu. Bila kusahau chai(chingambwe) yaani chai isiyo na sukari

Hapa ni samaki mzima mkubwa aliyeokwa kwenye oven na aina nyingine za samaki kama pweza, kamba nk. Karibuni tujumuike wapendwa.
Hapa ni viazi  kwa samaki wa kuchoma/banika  yaani hapa ndo walinikumbusha kwetu LUNDO/NYASA.
PAMOJA DAIMA.

Monday, January 22, 2018

NYASA NI MAARUFU KWA KILIMO CHA MATUNDA

 
Hapa ni kijiji cha Ndengele katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma tulimkuta kijana anauza ndizi mkungu mzima shilingi 2000 tu.


Katika eneo la Liuli tulikuta mananasi matatu yanauzwa shilingi 1000.

NB; Albano Midelo

Friday, September 4, 2015

MATUNDA NI MUHIMU KWA AFYA ZETU!!

Nimeyatamani kweli machungwa...Niwaambie kitu nilipokuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza na pili. Shuleni kwetu Lundo kulikuwa na miti mingi sana ya matunda mbalimbali mojawapo machungwa...Basi nakuambieni baada ya shule unaaga nyumbani kwenda kuchota maji au kuokota kuni kumbe kula machungwa ya shule...shhhh.:-(.....Ila mmhhh ilikuwa ukikamatwa na mlinzi basi ni viboko tu ...Kaaazi kwelikweli:-) PAMOJA DAIIMA NA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA. Kapulya.

Wednesday, May 27, 2015

LEO NIMEAMKA NA HAMU YA EMBE KWELI...KWENDA DUKANI ETI EMBE MOJA BEI YAKE ...

Ni 2640, duh  nikakumbuka nyumbani Ruhuwiko nina miembe na mpaka kuna wakati natupa maembe au nalisha nguruwe...Mmmmmhhh maisha haya kaziiiii kwelikweli.... JUMATANO NJEMA KWA WOTE!!

Tuesday, April 14, 2015

VYAKULA TUNAVYOPASWA KULA ILI TUWE NA AFYA BORA!!

Tusipuuzie vyakula vya aina hii ili kulinda afya zetu... Mie hapo nimeutamani hasa  muwa huo:-) Tuzingatie ndugu zanguni. Basi mie niwatakieni siku njma sana.  NENO LA LEO:- Usiache kufanya kitu kwa sababu umechoka, acha kwa sababu umekimaliza,

Thursday, December 5, 2013

MATUNDA NI MUHIMU KATIKA AFYA ZETU TUZINGATIE...

Huu ni mlo wangu wa leo mchana mchanganyiko wa matunda mbalimbali. Kama ilivyo ni kwamba matunda ni muhimu katika afya zetu. Usisahau kula hata tunda moja tu  kwa siku....Kila la kheri kwa wote....

Tuesday, July 9, 2013

MATUNDA NA BEI YAKE..KAAAZI KWELIKWELI......

Jana nikawa na hamu kweli ya papai nikaenda dukani kuangalia bei mamaaa weeewewee kama muonavyo hapa 22kr ni sawa na 5000Tsh na kapapai ndo kama ngumi yangu...nikaanza kukumbuka mapapai yangu Ruhuwiko kwangu..nikaondoka na sikununua papai. Maisha haya kaaaaazi kwelikweli..

Monday, May 20, 2013

PALE INAPOKUWA EMBE MOJA KUGAWANA WATU WANNE....

 Leo tumetamani kweli EMBE ..lakini bei yake mmmh, embe moja shilingi 2300.. Basi tukaishia kununua moja ili angalao kupunguza hamu ya embe....
...na mwisho wake vikatokea vipande vinne..kila mtu akapunguza hamu ...iliishia kwenye ulimi tu hata shingoni haikufika..mweeeeeh maisha haya kaaaaziii kwelikweli..Nakumbuka januari nilikula embe mpaka kuziacha na pia kutupa sasa....mmmmhhh.

Monday, February 18, 2013

KULA MATUNDA NI MUHIMU KWA AFYA ZETU..TUSISAHAU

Matunda ya aina mbalimbali ni muhimu kwa afya zetu...tujaribu kuzingatia kula matunda ,,ikiwezekana kila baada ya mlo JUMATATU NJEMA KWA WOTE...

Saturday, September 1, 2012

MWEZI MPYA:- TUANZE HIVI TUSISAHAU KULA MATUNDA NI MUHIMU KWA MIILI YETU!!

Matunda, tusisahau kula matanda jamani....kwa kawaida inatakiwa tule angalao kila siku matunda kama matano hivi. Lakini kwa bahati mbaya si wengi tuna nafsi ya kula hata tunda moja kwa siku. Na pengine wale wanye nafasi hawali. Jambo hili la kutokula matunda huhatarisha miili yetu kuto jengeka yaani vile virutubisho vya kuujenga mwili na kuuimarisha. kikinga. Na ndio hapo tunapojikuta miili yetu haina kinga za kutosha.
Wote tunajua mwili uwapo dhaifu ni rahisi sana kushambuliwa/kupatwa na maradhi hatari. Kama vile saratani, pia mboga majani nazo husaidia tuzile kwa wingi nazo pia. Kuna wakati unaweza kushangaa, kuona mtu anamaliza mwezi mzima hajala hata tunda moja. Tuchukue ule msimu wa machungwa, unaingia mpaka unaisha hajala hata chungwa moja. Ukija msimu wa maembe nao ni hivyo hivyo. Halafu utakuta maembe yanadondoka tu chini na kuoza na pia wengine wanayaokota na kulisha nguruwe. Au wanyama wengine lakini yeye mwenyewe anajisahau.

Wengi huona ya kwamba matunda siyo sehemu ya vyakula muhimu. Tuache tabia hii tule matunda na tuepukane na maradhi. Ukitaka kulifaidi tunda, basi kula pale ambapo tumbo lipo tupo/kabla hujala kitu chochote tanguliza matunda kwanza na baada ya nusu saa au saa moja, ndiyo unashauriwa ule mlo wako kamili.
NAWATAKIENI JUMAMOSI HII YA KWANZA YA MWEZI HUU WA TISA IWE NJEMA SANA!!!

Monday, May 14, 2012

JUMATATU HII AU WIKI HII TUANZE NA:- DONGI DONGI EMBE!!!

Leo nimeona tuelekee Mbamba bay kula embe. Je mpo nami au? Yaani hapa nimetamani kweli hizi embe  ....Haya nawatakieni mwanzo wa juma mwema na  DONGI DONGI JE UNAKUMBUKA MCHEZO HUU UJIPATA KITU BASI NDIYO NDONGI DONGI!!!!

Wednesday, April 25, 2012

MAPAPAI :- UTAMU ,FAIDA NA MATUMIZI YAKE!!

Kama kawaida ni kile KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO MBALIMBALI YA MADA, PICHA NA VITU VINGINE MBALIMBALI. NA LEO TUANGALIE KUHUSU MAPAPAI. Hiii niliiweka hapa kibarazana lakini kama mnijuavyo huwa napenda kurudia kusoma kitu ili nielewe zaidi. kusoma maoni mazuri ya wasomaji gonga KAPULYA. Karibuni sana.


Hapa ni mti wa papai, leo nimekumbuka faida mbili za majani ya mipapai moja ni dawa ya tumbo hasa kama una tatizo la choo kubwa . Unachukua hayo majanai na unachemsha na halafu unakunywa yale maji yake. Pili ni sabuni unaweza au niseme mimi nimewahi kufulia nguo ila usifulie nguo nyeupe basi itakuwa kijana. Nguo nyingine zote sawa kabisa.


Na hapa ni tunda lenyewe nalo lina faida zake kwanza ni kwa ajili ya kula ni tamu sana na pia nalo kama una tatizo la choo kubwa ni nzuri. Halafu jambo jinginge papai ni kilainisho kizuri sana cha chama hasa nyama ya ngómbe. Toa hizo mbege weka kwenye chombo, pondaponda papai na uchanganya na hizo mbegu koroga taratibu katakata nyama vipande vidogovodogo weka humu kwenye mpondo na subiri masaa kadhaa. Hakika utaifaidi nyama yako mno itakuwa lainiiii. Ila kusema kweli nimetamani kweli papai ni muda sasa sijala:-). PANAPO MAJALIWA BASI TUONANE TENA KATIKA KIPENGELE HIKI JUMATANO IJAYO!!!!!!

Monday, March 12, 2012

JUMATATU HII TUANZA HIVI:- MATUNDA NA VIUNGO!!


Nadhani wote mnajua hapa ni mti wa malimao angalia jinsi yalivyo yaani nashindwa hata kuelezea hapa ni mwaka jana wakati nilipokuwa nyumbani na ni Matema beach kwa rafiki yetu....

....na hapa bila kiungo hiki kachumbali hainogi ni pilipili kichaa ...swali la kizushi hivi ukila hizi unakuwa kichaa kweli? na kwanini zinaitwa pilipili kicha?..


Bado tupo Matema Beach bonge la mkungu wa ndizi mpaka nikatamani nipata na unajua nini? niliupata:-)
..Hapa ni Mdunduwalo mti wa machungwa ...naipenda Afrika yangu kwa kweli matunda na chakula ni kutoka tu nje na kuchukua....JUMATATU NJEMA JAMANI ILA MWENZENU LEO NIMETAMANI kwelikweli nyumbani...




Wednesday, February 29, 2012

MADONGA/NATURAL TROPICAL FOREST FRUITS......



MADONGA/MATUNDA YA ASILI
Nimeamka nikiwa na hamu kweli ya matunda haya ya asili, nimekumbuka nilipokuwa mdogo ukienda mstuni kuokota kuni basi huko nyumbani wasahau maana chakula tayari kilikuwepo. Matunda haya yanakuwa kwanza kijana, na baadaye yanakuwa njano unapasua na ndani yake kuna mbegu. Mbegu hizo zina nyama nyingi tu basi unazimungúnyamungúnya kama vile pipi na mbegu unatema...weeeeeeeeeeeee ni matamu na sijayala miaka mingiiiiiiiiiiii nimetamani kwelikweli...kama vile LIKUNGU....Kuna mwingine amewahi kula matunda haya????

Tuesday, January 31, 2012

ULIKUWA UNAJUA MATUNDA HAYA YANAITWA MABUNGO?.....

......na yanapatikana ZANZIBAR. Je? kuna anayejua kama yanapatikana sehmu nyingine? kuna dada mmoja alikuwa huko na alionja na akayapenda. Binafsi sijawahi kuonja. Natumaini nitapata jibu kwani nimeulizwa swali hilo na nimeshindwa kujibu na nikaona hapa nitapata tu jibu..Natanguliza shukrani....

Thursday, January 19, 2012

NI MSIMU WA MAEMBE/NINA HAMU YA KULA EMBE!!

Nimekaa hapa nikawa nawaza kuwa sasa ni msimu wa maembe, mmhhh nikapata hamu. Natamani kweli embe. Maana msimu huu huwa maembe yanakuwa mengi mpaka wengine wanalisha nguruwe...Je wewe una tamani matunda gani? au chakula gani?


Tuesday, February 15, 2011

MAPAPAI :- UTAMU ,FAIDA NA MATUMIZI YAKE!!

Hapa ni mti wa papai, leo nimekumbuka faida mbili za majani ya mipapai moja ni dawa ya tumbo hasa kama una tatizo la choo kubwa . Unachukua hayo majanai na unachemsha na halafu unakunywa yale maji yake. Pili ni sabuni unaweza au niseme mimi nimewahi kufulia nguo ila usifulie nguo nyeupe basi itakuwa kijana. Nguo nyingine zote sawa kabisa.
Na hapa ni tunda lenyewe nalo lina faida zake kwanza ni kwa ajili ya kula ni tamu sana na pia nalo kama una tatizo la choo kubwa ni nzuri. Halafu jambo jinginge papai ni kilainisho kizuri sana cha chama hasa nyama ya ngómbe. Toa hizo mbege weka kwenye chombo, pondaponda papai na uchanganya na hizo mbegu koroga taratibu katakata nyama vipande vidogovodogo weka humu kwenye mpondo na subiri masaa kadhaa. Hakika utaifaidi nyama yako mno itakuwa lainiiii. Ila kusema kweli nimetamani kweli papai ni muda sasa sijala:-)

Friday, October 8, 2010

Ngoja Ijumaa ya leo tuache ugimbi na tule matunda!!


Kula matunda uwe na afya bora poa kujikinga na magonjwa!! IJUMAA NJEMA SANA KWA WOTE!!

Wednesday, February 3, 2010

Mapotopoto: Matunda pori yenye sifa tatu

mti wa masuku/mapotopoto
matunda kwenye mti (masuku) mapotopoto


Habari hii imenikumbusha nilipokuwa mtoto magauni yalikuwa yanachanika mpaka mama alikuwa anachukia kweli. Maana ukienda porini ukirudi mapotopoto kibao kwenye gauni. Sielewi kwa nini nilikuwa sichukui kapu. Haya ungana nami tusome:-)

*Utamu wake wamithilishwa na asali
*Miti yake yadaiwa kutibu malaria
*Magamba yake ni mbolea maridhawa

RUVUMA ni mkoa uliojaliwa neema nyingi. Una aina mbalimbali za madini na inaelezwa kwamba utafiti wa kina ukifanyika unaweza kuwa na migodi mikubwa hivyo kuinua uchumi na ajira.
Katika sekta nyingine, Ruvuma ina misitu mikubwa iliyosheheni miti ya aina mbalimbali. Pia una Ziwa Nyasa lenye samaki watamu na dagaa wazuri kuliko dagaa wowote nchini.
Vile vile Mkoa wa Ruvuma una mito mingi, Mngaka, Ruhuhu na Ruvuma, kutaja michache, inavutia na inatoa samaki watamu kama mbasa, mbufu, mbelele na wengineo. Ruvuma ni moja ya mito mikubwa nchini na ambao unatenganisha Tanzania na Msumbiji.
Mkoa huo una milima ya kuvutia ambayo kama ikifanyiwa kazi inaweza kuwa moja ya vivutio vya kitalii na kuliingizia taifa na vijiji vinavyoizunguka kipato.
Milima Mara kwa mfano, uliopo Kata ya Magagura, unaweza kuwa kivutio kutokana na urefu na mandhari yake. Pia ipo Milima ya Litenga iliyotegwa na maji ambayo inalisha vijiji zaidi ya saba kwa miaka zaidi ya 30 sasa. Kuna safu ya Milima ya Livingstone, kuna Jiwe la Mungu huko Mbinga.
Pamoja na sifa hizo nilizotangulia kuzitaja, Mkoa wa Ruvuma una sifa nyingine kubwa inayotambulika zaidi hata kwa wanafunzi wa shule ya msingi, kilimo.
Mkoa huu ni moja ya mikoa minne 'the Big four' inayolisha chakula Tanzania na nchi za jirani. Pamoja na kuwa kilimo cha mahindi kinacholimwa zaidi Wilaya ya Songea, Ruvuma inazalisha kwa wingi mpunga, ulezi, ufuta, mtama, mihogo na soya.
Mbali ya mazao hayo ya chakula, kuna mazao ya biashara kama vile kahawa inayolimwa na kustawi zaidi wilayani Mbinga, na korosho inayolimwa zaidi Tunduru.
Sambamba na mazao ya chakula na biashara Ruvuma pia ina aina mbalimbali za matunda, ya kupandwa na yapo pia ya asili yanayopatikana kwa wingi misituni. Matunda pori haya yanajulikana kama mapotopoto, pia huitwa masuku.
Matunda mengine yanayostawi kwa wingi katika hasa katika Wilaya za Songea na Mbinga ni yake yanayojulikana kama Matunda Mungu.
Katika matunda yote hayo, mapotopoto yanaongoza kwa sifa. Wenyewe wanayafananisha na asali kwa utamu. Tunda lake lina mbegu nne ndani yake zinazozungukwa na utando wenye rojorojo ambao ndio hasa unaonywewa. Msimu wake wa mavuno ni kila robo ya mwisho wa mwaka.
Matunda haya yamekuwa chanzo kizuri cha ajira kwa akina mama wengi kwani wakati wa msimu, huenda porini na kwenda kuyauza katika maeneo mbalimbali kama vile kwenye vituo vya mabasi, sokoni, na wengine wakitembeza mitaani.
MMoja wa wachuuzi wa matunda hayo, Flora Mhagama anasema wakati mwingine huuza ndoo nzima kwa siku lakini kutokana na wingi wake porini, watu wengi huyafuata hivyo kufanya bei yake kuwa ndogo.

Anasema kwa ndoo hiyo moja anaweza kuingiza kati ya Sh1,000 na 1,500. Anauza kwa kupanga mafungu na kila fungu huuza kwa Sh50... “Yanatusaidia kupata fedha ya chumvi na sabuni.”
Wenyeji pia wanaamini kwamba miti inayotoa matunda hayo huweza kutoa dawa ya kutibu malaria inapokuwa michanga. Hii ni changamoto kwa watafiti wa dawa za tiba kubainisha ukweli huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Songea Vijijini Rogatus Haule anasema amewahi kusikia fununu hizo.
“Nimewahi kusikia kuwa miti michanga huweza kuwa dawa ya malaria ila siwezi kuthibitisha kama ni kweli au la. Ni ni wakati muafaka kwa taasisi za serikali na binafsi zinazojihusisha na utafiti wa dawa kutopuuzia fununu hizi na kuifanyia utafiti mimea hiyo,” anasema.
Inaelezwa pia kwamba masalia ya maganda ya matunda hayo ni rutuba nzuri kwa zao la uyoga. Hiyo inathibitishwa na ukweli kwamba katika misitu ambayo mapotopoto huzaliana kwa wingi, uyoga pia huota na kustawi.
Tatizo lililopo katika biashara ya matunda hayo kama ilivyo kwa mazao mengi mengine ni soko. Kwa mfano, Mkoa wa Dar es Salaam ambao hauna msimu wa matunda haujawahi kupelekewa mapotopoto.

Tatizo la kutopanua soko na kuangalia uwezakano wa kuyasindika matunda hayo ni moja ya changamoto ambazo zinawakabiliwa wadau wa kilimo wa Mkoa wa Ruvuma.

Na Jacob Malihoja kutoka gazeti la mwananchi

Sunday, June 28, 2009

MATUNDA NI MUHIMU KATIKA MWILI LAKINI BEI MBAYA MNO!!!!


Mti wa matunda damu. Matunda haya hapa Sweden moja unalipa 12kronor ni sawa na 2000Tsh
Halafu kula embe hapa embe moja inauzwa 9.90kronor ni sawa na 1584Tsh, pia papai bei yake ni kama 20,000Tsh. kwa hiyo ndio maana watu wengi wakija Afrika wanakula sana matunda kutokana na bei kuwa nafuu.