Jana nikawa na hamu kweli ya papai nikaenda dukani kuangalia bei mamaaa weeewewee kama muonavyo hapa 22kr ni sawa na 5000Tsh na kapapai ndo kama ngumi yangu...nikaanza kukumbuka mapapai yangu Ruhuwiko kwangu..nikaondoka na sikununua papai. Maisha haya kaaaaazi kwelikweli..
8 comments:
Mmh pole huku Mia 5 papai kibao
kweli kbs, ugenini tunapata shida sana ya bei za vitu ambavyo nyumbani viko chini!pole kwa hilo ila ishi maisha yalivyo ili kuepuka ugonjwa uitwao "kiu ya kweli!"
Mhhhhhhhh;nyumbani eeeeeeeeeh,nyumbani ni nyumbani japo hakuliwi!!!
Nancy! Ahsante aisee....na hongera
Kaka justin ! Umeona hiyo eeeh yaani hapa nipo hoi....
Kaka wa mimi Ray ....wewe acha tu..
Sasa hii ni fursa yako da Yasinta. Unaweza kuimport mapapai toka TZ na ukapata faida zaidi ya 500%. Ramadan Kareem to all. By Salumu.
Dada Yasinta nilikuwahi kukupa siri ya matunda nje, usilinganishe bei na kukumbuka ya shambani kwako mana ni ya bure, ukiwa na kiu ya tunda nunua tu kula ukimaliza ndio uanze kulinganisha bei na kukumbuka ya nyumbani! Ila pia licha ya bei hayana utamu kama wa ya nyumbani. Hongera kwa kuyatazama na kutonunua. Sasa huwa unapendelea matunda yapi ambayo bei yake ni nzuri kwa huko ulipo?
Bahati nzuri ni kwamba kila sehemu matumizi huendana na mapato..
Haya kaka Salumu ni wazo nzuri ahsante.
Usiye na jina nimekupata.
Dada mkuu msaidizi ahsante.
Post a Comment