TUTAONANA TENA MAJALIWA NA KAMA BASI NIWATAKIENI MWISHO WA JUMA UWE MWEMA...
Showing posts with label Swali. Show all posts
Showing posts with label Swali. Show all posts
Thursday, September 22, 2016
Monday, June 20, 2016
SWALI KUTOKA KWA MSOMAJI WA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO
Habari za leo ndugu zanguni...nimetumiwa huu ujumbe kwa barua pepe yangu..nimeona ni kheri niweke hapa kibarazani ili tusaidiani maana kwenye wengi pana mengi. Karibu tumsaidie huyo dada................................................................
Habari, mimi ni dada ninayeishi Iringa nina umri wa miaka 18 kwa bahati mbaya mpenzi wangu amenipa mimba na kutokana namna alivyo baba yangu Naamini akifahamu kwamba nina mimba ataniua Kwani mimi ni mwanafunzi.
Nimeongea na mchumba wangu tumekubaliana tukaitoe.
Hata hivyo bado najiuliza kama kutoa mimba ni kitu sahihi? Na je, nifanyeje Kwani nipo kwenye njia panda.
Thursday, September 3, 2015
SWALI NILILOULIZWA NA MSOMAJI /MFUATILIAJI WA MAISHA NA MAFANIKIO:-
Swali lenyewe lipo hivi:- Hivi ni kitu gani akina mama/wanawake kinawafanya wampende mtoto fulani zaidi kati ya watoto wao wa kawazaa?
Akaendelea:- Utamkuta mama ana watoto wanne, lakini anampenda mmoja zaidi ya wengine? Hii inakuwaje kwa upande wako? akanipa hili swali mimi......akaendelea nakuuliza kwa kuwa nadhani una watoto.....halafu akaendelea kusema ....Pia nadhani utakuwa umeshawahi kuisikia hii au inatokea.
Jibu langu lilikuwa kama ifuatavyo:- Binafsi kama mama nawapenda wanangu sawasawa na sijawahi kufikiria KUWAPENDA TOFAUTI.
Baadaye nikakumbuka kwanini niwashirikishe ninyi wasomaji/ ndugu zangu. Maana naamini palipo na wengi pana mengi
Hata hivo nami nikajiwa na swali:- Je? Hiki kitu kipo? na kama kipo kwa akina mama/wanawake tu? na sio akina baba/wanaume? Maana nao pia ni wazazi. NAOMBA TUJADILI KWA PAMOJA......Kapulya wenu!
Akaendelea:- Utamkuta mama ana watoto wanne, lakini anampenda mmoja zaidi ya wengine? Hii inakuwaje kwa upande wako? akanipa hili swali mimi......akaendelea nakuuliza kwa kuwa nadhani una watoto.....halafu akaendelea kusema ....Pia nadhani utakuwa umeshawahi kuisikia hii au inatokea.
Jibu langu lilikuwa kama ifuatavyo:- Binafsi kama mama nawapenda wanangu sawasawa na sijawahi kufikiria KUWAPENDA TOFAUTI.
Baadaye nikakumbuka kwanini niwashirikishe ninyi wasomaji/ ndugu zangu. Maana naamini palipo na wengi pana mengi
Hata hivo nami nikajiwa na swali:- Je? Hiki kitu kipo? na kama kipo kwa akina mama/wanawake tu? na sio akina baba/wanaume? Maana nao pia ni wazazi. NAOMBA TUJADILI KWA PAMOJA......Kapulya wenu!
Friday, July 17, 2015
Thursday, April 23, 2015
DUH KAAAZI KWELIKWELI HAPA SIJUI MWALIMU ATAJIBU NINI???
Nimeipenda hii angalia mwal. jinsi jasho linavyomtoka kwa kutafuta jibu. Watoto huwa wakweli sana na hawaoni aibu kuuliza swali....KILA LA KHERI.
Wednesday, November 12, 2014
SWALI LA LEO KUTOKA MAISHA NA MAFANIKIO A.K.A KAPULYA....
N imekuwa nikijiuliza kila siku na sijapata jibu, sasa leo nimeona niliweke hapa kwani palipo na wengi hapaharibiki neno, Ni hili hapa swali lenyewe:- Hivi kwa nini pilipili inamfanya/tufanya tupige chafya? Najua mtasema mbona kuna vingi vyatufanya kupiga chafya, lakini mimi naona pilipili ni zaidi.....naomba tujadili kwa kupamoja. JUMATANO NJEMA!!!
Wednesday, August 13, 2014
SWALI /TAFAKARI LANGU/YANGU LA/YA LEO ....NAOMBA TUTAFAKATI PAMOJA
Swali langu la leo:- Hivi tusemapo NI MTU NA MJOMBA WAKE au Ni MTU NA SHANGAZI YAKE.
JE? kati ya hao MTU NI NANI NA MJOMBA/SHANGAZI NI YUPI?
HAYA KILA LA KHERI TUPO PAMOJA.....Kapulya wenu.
Monday, November 25, 2013
TUANZA JUMATATU HII NA SWALI HILI KUTOKA KWA KAKA BWAYA ...KUHUSU MAISHA NA FURAHA!!!
Kama mnakumbuka mwezi uliopita niliweka picha hii hapa kibarazani na baadaye kulitokea na maoni. Na baadhi ya maoni aliyotoa msomaji mmoja ambaye ni kaka Bwaya ambaye alikuwa ameadimika kwa muda mrefu na sasa yupo nasi tena. Nachukua nafasi hii kumkaribisha Kaka Bwaya......Haya na maoni yenyewe yalisomeka hivi;-
Bwayasaid...
Tafiti zinaonyesha kuwa watu waishio katika maisha yanayoonekana kuwa duni, ndio wenye furaha zaidi. Mfano ni hawa. Swali: kwa nini? Naomba tusaidiane kujadili swali hili kwa pamoja....JUMATATU NJEMA!!!
Bwayasaid...
Tuesday, September 17, 2013
UJUMBE /SWALI WA/LA LEO!!!
Kama huwezi kujisamehe mwenyewe na uliyoyafanya, utawezaje kuwasamehe wengine?
NAWATAKIENI WOTE JUMANNE NJEMA SANA NA KUMBUKENI TUPO PAMOJA DAIMA!!!Kapulya!
NAWATAKIENI WOTE JUMANNE NJEMA SANA NA KUMBUKENI TUPO PAMOJA DAIMA!!!Kapulya!
Thursday, August 15, 2013
NAOMBA TAFSIRI YA NENO KIONGOZI/VIONGOZI...MAANA LINANIKERA MNO.......!!!
Nimeamka leo nikiwaza hili neno KIONGOZI/VIONGOZI nikashindwa kuliwazua nikaamua kuchukua KAMUSI SANIFU YA KISWAHILI CHETU. Nayo ikaniambia hivi:-KIONGOZI/VIONGOZI.....
1. mtangulizi wa jambo fulani au wa kikundi cha watu, mkubwa anayesimamaia shughuli maalumu kwa kueleza au kuelekeza. AU...
2. Kitu kinachosaidia kuonyesha au kuelekeza......
Je? hawa viongozi wanaongoza kweli au wanajiongoza? Naomba tutafakari au jadili kwa pamoja.
Ndimi Kapulya wenu:-)
1. mtangulizi wa jambo fulani au wa kikundi cha watu, mkubwa anayesimamaia shughuli maalumu kwa kueleza au kuelekeza. AU...
2. Kitu kinachosaidia kuonyesha au kuelekeza......
Je? hawa viongozi wanaongoza kweli au wanajiongoza? Naomba tutafakari au jadili kwa pamoja.
Ndimi Kapulya wenu:-)
Tuesday, July 23, 2013
SWALI LILILONISUMBUA SIKU YA LEO...!!!!
Nimeamka asubuhi hii na nimemshukuru Mungu kwa kunilinda. Nikaona ngoja ninyooshe viungo:- Yaani nikaende nje kama kawaida yangu kukimbia, nimekimbia, nimekimbia mara nikakutana na mkimbaji mwingine naye kawaza kama mimi anakimbia. Sasa hapa kitu kilichonipa swali ni kwamba mdada huyu alikuwa akikimbia na mbwa wake ambaye amemfunga kamba shingoni. Swali likanijia huyu dada ana uhakika kama huyu mbwa/kambwa anataka kukimbia? Maana niliona kama mbwa mwenyewe hata hakufurahia. Nikataka kusimama na kumuuliza.....lakini nikaacha. Muda wote nilipokuwa nakimbia swali lilizidi kunisumbua hivi kweli yule mbwa alipenda kukimbia? Na pia nikazidi kuwaza....Nikaona niwape na wenzangu haka kakisa....TUSITENGANE TUWA TUNAKUMBUKANA. PAMOJA DAIMA SIKU NJEMA. KAPULYA!!
Tuesday, October 16, 2012
KWANINI KUNA MAHINDI YA NJANO NA MAUPE?
MAHINDI YA NJANO....
Na hapa ni mahindi MEUPE ambayo mimi binafsi nimeyazoea tangu nilipokuwa katoto kadogo. Ndiyo, nimewahi kuona mahindi mekundi meusi au mchanganyiko lakini hayo ya njano sijawahi kuona Tanzania yetu. Je? kwanini?
Tuesday, June 5, 2012
KWANINI PILIPILI MBUZI INAITWA HIVYO? NA JE KWA NINI HIKI CHOMBO ZA KUKUNIA NAZI PIA CHAITWA MBUZI?
Pilipili mbuzi zikiwa kwenye mti jee unajua kwanini zina itwa Pilipili Mbuzi? ni kwa kuwa zina faa sana kwenye supu ya Nyama ya Mbuzi au?
N ahap ni mbuzi mwenyewe , sioni kama kuna mfanano hapa...
...na hapa sasa ni kifaa cha kukunia nazi nacho kinaitwa MBUZI . Mara chache nimesikia wengine wakisema kikunio au je kuna jina jingine ambalo mimi sijawahi kulisikia...naamini kwa pamoja tutafika pahala pazuri. Mchana,jioni au sijui usiku mwema....KAPULYAMonday, May 21, 2012
BAADA YA MAPUMZIKO NIMEONA TUANZA JUMATATU HII KIHIVI!!!
Ni matumaini yangu kuwa wengi wetu twnajua/twakumbuka hapa ni wapi. Labda tu niuliza Je? unajua hapa ni wapi?...Nawatakieni mwanzo wa juma hili uwe mwema.
Tuesday, April 24, 2012
SWALI HILI LIMENIKERA SANA:- MAJINA YA SAMAKI YANATOKA WAPI???
HAPA NI SAMAKI AINA YA MAGEGE
Ni muda mrefu sana nimekuwa nikijiuliza kuhusu majina ya samaki. Juzijuzi nilikuwa nikiangalia habari/pragramu kuhusu ziwa Nyasa, ziwa Viktoria na Tanganyika. Nikakumbuka majina ya samaki kama vile :- Kambale, Mbofu, Mbelele/sengefu, Magege, Vitui, Vindogo, Mbasa nk. Nikawa najuiliza hivi ni maeneo ya ziwa nyasa tu tunawaita hawa samaki hivi au? Na kama ni hivi nani aliwapa samaki hawa haya majini? Sikupata jibu...nikaona niliweke hapa kibarazani hili swali. Kama nisemavyo/nijuavyo palipo na wengi hapaharibiki kitu. Tuwe pamoja katika kamjadala haka
Friday, March 30, 2012
SWALI LA WIKI HII!!!!
Umewahi kufanya maamuzi magumu sana kwenye maisha yako? ilikuwa ni kuhusu nini?haya funguka sasa!
NAWATAKIENI WOTE KILA LA KHERI NA MUWE NA MUDA MZURI NDANI YA MWISHO WA JUMA HILI LA MWISHO WA MWEZI HUU WA TATU.UPENDO DAIMA.
NAWATAKIENI WOTE KILA LA KHERI NA MUWE NA MUDA MZURI NDANI YA MWISHO WA JUMA HILI LA MWISHO WA MWEZI HUU WA TATU.UPENDO DAIMA.
Tuesday, January 31, 2012
ULIKUWA UNAJUA MATUNDA HAYA YANAITWA MABUNGO?.....
Monday, January 23, 2012
TUANZE JUMATUTA KIHIVI:-JE? NI PICHA GANI AMBAYO IMEVUNJA REKODI MWAKA 2011 KATIKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO?
Saturday, January 7, 2012
NIMEULIZWA SWALI HILI NA BINTI YANGU....
Ilikuwa mwaka jana siku ya Noeli ...Binti yangu Camilla akaniuliza:- Mama, hivi kwa nini Yesu alizaliwa tarehe 25/12..Lakini, kipindi cha Pasaka huwa tuna sema kuwa Yesu anakufa, kwa nini ile tarehe ya kufa huwa haiwi ileile kila mara? Je kuna Yesu wangapi?...Mmmhhh!! hapa nikawa natafakari na sijapata jibu na leo nimeona niombe msaada hapa kibarazani kwani palipo na wengi huwa hakiharibiki kitu....
Tuesday, December 13, 2011
HATA MIGUU NAYO HUPENDEZESHWA!!!! SWALI JE NI VIBAYA?

Vikuku ni urembo au?
KUNA mtu kanitumia hiyo picha anauliza hizo shanga za miguuni zinavaliwa kujiremba au zina maana nyingine?Kwa mujibu wa maelezo yake, amewahi kusikia kwamba, shanga hizo a.k.a vikuku zina maana yake hivyo anaomba kufahamu kama ni kweli. Anasema, kaelezwa kwamba, kikuku kikivaliwa mguu wa kulia ina maana yake, na kikivaliwa kushoto kinakuwa na maana nyingine, ni kweli?Kama kila mguu una maana yake, vikivaliwa miguu yote inamaanisha nini?
Pia nimesikia nchi kama Ivory Cost ukivaa mguu wa kulia basi inaonyesha kuwa wewe ni msagaji /shoga. Je ni kweli?
Subscribe to:
Posts (Atom)










