Showing posts with label ugimbi. Show all posts
Showing posts with label ugimbi. Show all posts

Friday, October 1, 2010

Ni Ijumaa mpja ya mwezi, kula kwanza halafu kunywa!!

Napenda kuwatakieni IJUMAA njema na mpya /ya kwanza ya mwezi huu wa kumi. Kila mtu leo atasema sasa nimemaliza kazi ngoja nipumzika na nipate moja baridi!ugimbi. Ni sawa lakini kumbuka kula kwanza ni MUHIMU sana. IJUMAA NJEMA!!!

Wednesday, July 21, 2010

Mlevi anapolewa chakari na kuanza kuongea!!!!

"Mlevi anapolewa chakari na kuanza kuongea unapaswa kumsikiliza kwani wengi wao huongea yale yaliyoko mioyoni mwao. Uhusiano wa pombe na ufanyaji kazi wa ubongo husababisha mlevi kunena yale yaliyoko moyoni mwake bila ya simile"- Mwalimu Malekela, Tabora Boys 1994.
Swali ni kwamba, je utafaidikaje na uvumbuzi huu? Nadhani ni kwa kuchagua yale yatokayo kwenye kinywa cha mlevi kwani si yote yatakuwa ni yenye kujenga. Mengi yatokayo kwenye kinywa cha mlevi hutokana na migogoro iliyoko ndani ya mioyo yao. Mara nyingi migogoro hii inakuwa ni ile isubiriyo suluhisho.
Katika jamii yangu mara nyingi nimeshuhudia tabia ya baadhi ya watu pale inapotokea kutokuelewana na wenzao, basi huenda kunywa pombe na kisha kurejea kwa mabishano zaidi. Je kuhusu wale wanaume wanaopenda kupiga wake zao pindi wanapolewa? Je hii nayo inasababishwa na migogoro au inakuwa ni tabia ya kuzoea? Au pale daktari au mwalimu anapohitaji glasi mbili au tatu ili waweze kufanya kazi zao? Hii inakuwaje?? Je kuna uhusiano kati ya unywaji pombe na ufanisi katika kazi? Je umepata kusikia kuhusu yule daktari bingwa wa upasuaji ambaye ni lazima apate kinywaji kwanza ili aweze kutenda kazi yake vema?
Habari hii nimetumiwa na msomaji wa blog ya Masha na Mafanikio na kuniomba niiweka hapa kibarazani ili tujadili kwa pamoja. Haya wapendwa karibuni na tujadili. Umoja ni nguvu .....