Showing posts with label kutokuwa na huruma. Show all posts
Showing posts with label kutokuwa na huruma. Show all posts

Wednesday, June 17, 2009

SAFARI YA SONGEA MWAKA 2009

Najua wengi mnakumbuka mwaka huu mwanzoni kabisa nilikuwa nyumbani Tanzania. Ni kwamba baada ya wiki moja, nilikwenda madukani kununua vyombo ilikuwa siku ya Ijumaa. Si mnajua Ijumaa ni siku ya watu kupita madukani kuomba. Songea ni hivyo sijui sehemu nyingine Tanzania pia. Basi nikiwa katika harakati za kulipa akaja mtu mmoja au niseme alikuwa (kijana)au pia naweza kusema alikuwa na "changamoto za kifikra" (mentaly challenged)?
Alivyoonekana alikuwa kichaa. Akamwambia mwenye duka naomba hela akamjibu leo hakuna.

Akageuka kwangu we dada je? naomba hela nami nikamwambia sina. Akanipiga kofi na akaondoka zake. Kwa kweli nilishikwa na mshangao sana. Nimeandika hii kufananisha na mambo anayofanya dada Koero ninavyoamini mimi angekuwa pale angeacha kununua vyombo na angempa yule mwombaji. Nimejifunza mengi sana katika mada zake dada Koero asiyesoma basi chukuni muda na someni. Koero Mkundi hasa hii mada ya ANITA NA MIKASA YA DUNIA .Nashukuru Mungu ametuumba tofauti. Ni hayo tu kwa leo ni mada fupi lakini ina ujumbe wake.