Kama mnawakumbuka picha hii na tukio lake basi ni kwamba Dada mkubwa Mariana Kutoka nchini Angalo katika picha kushoto mwenye miwani katuacha ghafla leo . Ni masikitiko makubwa sana kwa familia yake marafiki na jamaa. Da Mariana alikuwa mtu mmoja ambaye ni mcheshi, makarimu na mwenye kupenda sana watu. Kwangu ni pigo kubwa sana, kwani yeye alikuwa mtu muhimu sana kwangu, zaidi ya rafiki...alikuwa hakosi kunifariji pale nilipokuwa na matatizo.. nimepatwa na mshtuko wa ajabu kwa kweli...hebu soma hapa. MWENYEZI MUNGU NA AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI...AMINA
Showing posts with label rafiki. Show all posts
Showing posts with label rafiki. Show all posts
Wednesday, March 20, 2013
Friday, March 1, 2013
CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KATIKA KUUANZA MWEZI HUU WA MACHI/TATU NA IJUMAA YA KWANZA YA MWEZI HUU NI:- WIMBO HUU WA DADA RAY-C UPO WAPI...
Tuanza mwezi huu kwa kujiulizani lini nimewasiliana na baba, mama, babu, bibi, shangazi, mjomba, kaka, dada, mama mdogo, baba mdogo, mtoto, rafiki, mpenzi wangu au hata jirani yako. Kwa hiyo chukua nafasi na mtafute yule mliopoteana na mpeana mawili matatu....NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA NA MWISHO MWEMA WA WIKI...
Tuesday, February 26, 2013
PALE MNAPOKUTANA NA MLIOFANYA NAO KAZI/MLIOSOMA NAO....
......Furaha inakuwa ni ya ajabu...hapa ni mwalimu mtaafu Eusebius Mlelwa na mwal. Klaesson walikuwa wanafanya kazi pamoja Wilima Secondary hapa walikutana mwaka huu mjini Songea. Hapa ni stendi kuu ya Songea
Sio wao tu walipata bahati ya kuonana ..la hasha Yasinta/kapulya naye alionana na rafiki yake ambaye walisoma chuo pamoja ni Pendo Mapunda. Nilifurahi sana kuonana na Penda miaka mingi tulipoteana. Hapa ni Lizabon Songea.....Raha eeeehhhh....
Tuesday, March 20, 2012
UMEWAHI KUFIKIRI KUWA HAKUNA KITU KIBAYA KAMA KUPOTEZA MAWASILIANO NA RAFIKI, MPENZI, MUME/MKE AU LABDA NISEME JAMII KWA UJUMLA?
Basi mwenzenu yamenikuta nimempoteza rafiki yangu mpenzi . Namtafuta kwa kila hali na mali lakini simpati. Na jinsi ukimya uzidivyo nazidi kukosa raha. NAMPENDA SANA RAFIKI YANGU HUYU. KAMA UMESOMA UJUMBE HUU TAFADHALI NTAFUTE SITAKI KUKUPOTEZA.....Dada Yasinta nifanye nini ili rafiki yangu aongee tena nami?
-------------------------------------------------------------------------------------------------Ujumbe huu nimetumiwa na mdau ambaye ni msomaji wa Maisha na Mafanikio...nikaona niweke hapa ili mnisaidie ni ushauri gani kumpa mwenzetu.
-------------------------------------------------------------------------------------------------Ujumbe huu nimetumiwa na mdau ambaye ni msomaji wa Maisha na Mafanikio...nikaona niweke hapa ili mnisaidie ni ushauri gani kumpa mwenzetu.
Friday, December 2, 2011
TUWE PAMOJA NA KAKA Addson Noel Omari ( Mfalme Mrope ) KWA MAOMBI YA MSIBA WA MAMA MZAZI HUKO NYUMBANI TANZANIA!!
Kaka Mrope pole sana kwa msiba wa mama yetu mzazi kwani naamini mama yako ni mama yetu.Katika pita pita zangu nimekutana na habari hii ya kusikitisha.-----------------------------------------------------------------------------------------------
TAARIFA YA MZIBA
Napenda kuwataarifu ndugu zangu na marafiki popote mlipo kuwa nimepatwa na msiba wa mama yangu mzazi Shamsa binti Hassan aliyefariki huko nyumbani Tanzania leo tarehe 2/12/2012. Habari za kisomo na dua zitawajia baadae. BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA...Kwa pole napatikana 301 222 7739.... nahitaji maombi yenu.Wenu, Addson Noel Omari ( Mfalme Mrope ) http://tustaarabike.blogspot.com/
Tuesday, October 25, 2011
KAKA SHABAN KALUSE APATWA NA AJALI YA GARI/DALADALA NA KUVUNJIKA MKONO WA KULIA!!!
Friday, October 7, 2011
IJUMAA NJEMA PIA MWISHO WA JUMA MWEMA!!!
Nikiwa natoka kazini kwenye baiskeli yangu ghfla nikajikuta naimba wimbo huu nikaona niuweke hapa ....TUPO PAMOJA!!!
Tuesday, April 27, 2010
HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA DA MIJA/MWANAMKE WA SHOKA!!
Ni furaha kuwa na rafiki kama Da Mija na leo ni siku tukufu kwako. Ni siku ambayo ulitokea hapa duniani . Napenda kukutakia yote mema, uishi miaka mingi uwe bibi kizee na wajukuu wengi uwe nao. Mija, kama wote tunavyomfahamu alizaliwa hapa dunuani ili awe mwanamke wa shoka nakuheshimu na pia nakupenda sana .HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA RAFIKI YANGU na MWANAMKE WA SHOKA WETU!!!!!!
Wednesday, November 18, 2009
+RAFIKI YANGU MPENDWA AGNESTA MAPUNDA+
Kutokana na sheria au sijui niseme mipango ya Tanzania kuwahamisha/shwa walimu:- Nakumbuka ilikuwa mwaka 1985 baba alipata uhamisho kutoka Lundo s/m kwenda kijiji kimoja chenye shule iitwayo Kingoli. Nilikuwa darasa la tano. Nilipofika pale shuleni nilikutana na wanafunzi wengi, lakini Agnesta alinipokea kwa namna yake.
Tulianza urafiki wetu, uarafiki ambao tulikuwa wakati wa jumamosi au jumapili tukitembeleana majumbani. Yaani, tulikuwa tukitembeleana, huku tunachuklua zawadi(ndundu) unga kwenye jamanda na kuku. Na ukifika kwake unachinjiwa kuku pia.
Nliachana mwaka 1988 na rafiki yangu Agnesta. Mwaka 2007 nilikuwa nyumbani TZ. Siku moja nilikuwa mjini – Songea, katika pitapita ghafla mtu akanishika bega na kunisalimia dada Yasinta shikamoo! Nikashtuka na kugeuka alikuwa mdogo wake Agnesta. Nikasema moyoni AHSANTE Mungu. Kwa kufurahi kupata habari za rafiki yangu Agnesta. . Lakini habari nilizozipata hazikuwa nzuri Agnesta rafiki yangu alikuwa hayupo tena nami alishafariki muda mrefu labda miaka mitatu iliyopita. Sikuamini masikio yangu, nilisikitika sana , kwani alikuwa rafiki yangu mpendwa. Na leo naona amenishukia nkwani nimemkumbuka sana ndio maana kisa cha kuandika hapa. Mwenyezi Mungu Aiweke Roho yako PEPONI AMINA..
Tulianza urafiki wetu, uarafiki ambao tulikuwa wakati wa jumamosi au jumapili tukitembeleana majumbani. Yaani, tulikuwa tukitembeleana, huku tunachuklua zawadi(ndundu) unga kwenye jamanda na kuku. Na ukifika kwake unachinjiwa kuku pia.
Nliachana mwaka 1988 na rafiki yangu Agnesta. Mwaka 2007 nilikuwa nyumbani TZ. Siku moja nilikuwa mjini – Songea, katika pitapita ghafla mtu akanishika bega na kunisalimia dada Yasinta shikamoo! Nikashtuka na kugeuka alikuwa mdogo wake Agnesta. Nikasema moyoni AHSANTE Mungu. Kwa kufurahi kupata habari za rafiki yangu Agnesta. . Lakini habari nilizozipata hazikuwa nzuri Agnesta rafiki yangu alikuwa hayupo tena nami alishafariki muda mrefu labda miaka mitatu iliyopita. Sikuamini masikio yangu, nilisikitika sana , kwani alikuwa rafiki yangu mpendwa. Na leo naona amenishukia nkwani nimemkumbuka sana ndio maana kisa cha kuandika hapa. Mwenyezi Mungu Aiweke Roho yako PEPONI AMINA..
Monday, October 12, 2009
HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA DA SUBI!!

Ni furaha kuwa na rafiki kama Da Subi na leo ni siku tukufu kwako. Ni siku ambayo ulitokea hapa duniani . Napenda kukutakia yote mema, uishi miaka mingi uwe bibi kizee na wajukuu wengi uwe nao. Subi ni mtu mtukutu sana kwa hilo nakuheshimu na pia nakupenda sana .HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA RAFIKI YANGU!!!!!!
Thursday, August 27, 2009
JE, UPWEKE NI UGONJWA?
Kabla na baada ya kuja huku niliko nilikuwa na marafiki wengi kifani. Lakini baada ya kuishi mwaka mmoja hap nililetewa barua toka kwa marafiki zangu na kuniomba niwatafutie wachumba au kazi. Na nilipowajibu kuwa mimi nilikuwa mgeni, pia binafsi sikuwa na kazi wala sikujua lugha walikata mawasiliano nami.Nikawa nashangaa kwa nini? je? hawa kweli walikuwa marafiki wa kweli yani wale ambao wanasema hufaana kwa penye furaha na taabu. Kwa hiyo nikabaki mpweke bila rafiki wa karibu isipokuwa nilikuwa na rafiki yangu wa karibu sana ambaye ni mume wangu na baadaye wanangu. Na baadaye yaani kama mwaka mmoja uliopita nilianza kublog na hapo nikapata marafiki wengi tena. Na natumaini ninyi rafiki nilowapata hamtanikimbia. Hii ndio sababu nimeuliza je? upweke ni ugonjwa? kwasababu mimi nilikosa sana raha nilipokuwa mpweke.
Saturday, August 2, 2008
AUGOSTI 2, 2008 UTANI
Kuna watu wengi wanapenda sana mambo ya utani kiasi kwamba yule anayempa ule utani anaami ni au anaweza mpaka kuchanganyikiwa. Mimi mwenyewe ni moja wa watu hao, napenda sana utani laki ni sio kwamba nataka kuwatesa au kuwachanganya la hasha. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kama ule utani umepita mipaka na unakaribia kuwapoteza marafiki zako wote utafanyaje. Kwani hilo swali nimepata leo kwa rafiki mmoja amemdanganya rafiki yake kwamba wakutane sehemu furani lakini kumbe ni uwongo je afanyeje ili wawaze kuwa marafiki tena. Kwani anajisikia vibaya pia anaona aibu kwa kuwa mwongo. Hataki kumpoteza rafiki yake kwani ni mabest. Pia anasema kwa vile wako mbalimbali kama ingekuwa karibu angejaribu kuongea naye na kuomba radhi. Kwa yeye aliona kama ni mchezo. Wasomaji naomba mnisaidia nimwambieje huyo ili amwambie rafiki yake wa mbali.
Subscribe to:
Posts (Atom)
