Saturday, August 2, 2008
AUGOSTI 2, 2008 UTANI
Kuna watu wengi wanapenda sana mambo ya utani kiasi kwamba yule anayempa ule utani anaami ni au anaweza mpaka kuchanganyikiwa. Mimi mwenyewe ni moja wa watu hao, napenda sana utani laki ni sio kwamba nataka kuwatesa au kuwachanganya la hasha. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kama ule utani umepita mipaka na unakaribia kuwapoteza marafiki zako wote utafanyaje. Kwani hilo swali nimepata leo kwa rafiki mmoja amemdanganya rafiki yake kwamba wakutane sehemu furani lakini kumbe ni uwongo je afanyeje ili wawaze kuwa marafiki tena. Kwani anajisikia vibaya pia anaona aibu kwa kuwa mwongo. Hataki kumpoteza rafiki yake kwani ni mabest. Pia anasema kwa vile wako mbalimbali kama ingekuwa karibu angejaribu kuongea naye na kuomba radhi. Kwa yeye aliona kama ni mchezo. Wasomaji naomba mnisaidia nimwambieje huyo ili amwambie rafiki yake wa mbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Utani ni mzuri sana kwani hufanya tufurahi na kucheka kitendo ambacho ni afya.
Pia utani una mipaka yake sasa kama mtu anakudanganya then anasema anatania hapo inabidi awe makini. Kwa uzoefu wangu kuna watu huwa hawataniwi kamwe. Na pia kuna wengine wao ni mabingwa wa kutaniwa ingawa wenyewe huwa hawataniwi.
Muhimu kusoma saikolojia ya mtu kwanza ndo fanya utani.
Binafsi napenda sana utani
Yasinta sasa utaua watu!kumbe unatania hadi jamaa wanachanganyikiwa hivyo?Hivi kwanini uliamua kumtania ua kuna mtu alikuwa nafanya utani ambao jamaa akajua ni kweli? aah mwambie hakuna lililojema kama kutaniana na marafaiki lakini pamoja na hayo nimkumbushe msomo wa Rais kikwete kwamba "i will be wearing a smile but firm on issues' kazi kwako utapaoteza marafiki
Post a Comment