Wednesday, August 20, 2008

AGOSTI 20, 2008 MAISHA,UNYANYASAJI NA ELIMU

Wote tunajua maisha ni changamoto, maisha ni mawasiliano yanayotufundisha kukuabiliana na changamoto zote. Kwa hiyo inabidi tusimame imara. Kama nilivyosema hapo mwanzoni madawa ya kulevya, inaonekana ni kishawishi kikubwa kwa wengi, ambacho inabidi tukabiliane nacho. Maisha si rahisi wakati wote, wote tunatakiwa kuwa makini na hodari ili tuweza kukabiliana na mambo mbalimbali tunayotaka katika maisha yetu. Hakuna mwingine ayaongozayo maisha yetu zaidi ya sisi wenyewe au wewe mwenyewe. Kwa hiyo inabidi kuchagua na kuamua mambo fulani fulani maishani mwako/ mwetu. Tunatakiwa kuweka malengo yetu na KUKATAA vishawishi ambavyo tunajua vitayaharibu maisha yako/yetu. Tumbumbuke wahenga walisema utavuna ulichopanda.

Halafu kuna hili jambo la unyanyasaji:- Unyanyasaji, kuna ukatili mwingi sana hapa duniani ambao zaidi ni juu ya wanawake na watoto. Hao ndio wanaopata shida zaidi. Ukatiki ni kinyume na haki za binadamu na uko ukatili wa aina mbalimbali. Kuna vipigo, matusi, kulazimishwa kufanya mapenzi, kuna baadhi ya mila potofu kama vila ndoa za lazima, kuolewa ukiwa na umri mdogo, kurithi wajane, pia ni ukatili kutahiri wanawake.

Nisisahau jambo la elimu:- Wote tunajua ujuzi ni nguvu na elimu ni ufunguo wa maisha. Hii ndiyo sababu tunaenda shuleni, ili tuweze kupata elimu na kujua mambo. Kumbuka usipokuwa na elimu nzuri huwezi kupata kazi nzuri.

1 comment:

Simon Kitururu said...

Kijiwe poa sana hiki Dada!Asante pia kwa kupoitia kule kwangu.