Habari hii nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio nami nimeipenda na nimeona nisiwe mchonyo pia ni vema kujadili kwa pamoja...pamoja daima...
---------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kwanini nasema hivyo:- Nasema hivi nikiwa na maana yake, ni kwamba zamani maisha yalikuwa mazuri na mepesi na yenye khekima kwa wakubwa na wadogo. Vyakula vilikuwa vingi pesa ilikuwa ina thamani. Ikiwa na maana watu waliishi kwa mapenzi mema tena sana. Watoto wakike walifundishwa jinsi ya usafi, kupika, kujiepusha na vitu vya anasa na kadhalika. Na pia wazee waliwapenda wajukuu wao. Wakati wa jioni walikaa nao wakiota moto wakiwa wanawasimulia hadithi nzuri ambazo zilikuwa na mafunzo na pia watoto waliburudika sana. Pamoja na kuwa palikuwa na uhaba wa huduma za jamii ila watu waliishi kwa kula vyakula asilia, na kutumia dawa za miti shamba....,,, Namalizia kusema MAISHA YA ZAMANI YALIKUWA NI BORA KULIKO YA SASA!!! Napenda kusema tena:- Maisha ya kisasa ni tofauti na zamani kwanini nasema hivyo. Maana yake siku hizi watu sio vijana sio wazee wanapenda mambo ya kisasa NA PIA YA KUIGA. Utakuta wanavaa mavazi tofauti na zamani, wanapenda anasa sana kuliko vitu vinginne, hawapendi kukaa na watoto wao kama wazee wa zamani, hawapendi vitu asilia....! Je? Kuna ukweli kuwa maisha ya zamani ni bora? KILA LA KHERI!!!!


