Mvulana mmoja maskini alikuwa akiangalia gari la bwana mmoja ambaye alikuwa tajiri, tajiri alimchukua yule mvulani na kumwendesha katika lile gari. Mvulani akasema una gari nzuri sana. Je? hili gari si ghali sana? Tajiri akamjibu, ndiyo ni ghali sana ila mimi nilipewa na kaka yangu kama zawadi.
Mvulana akawa anafikiri. Tajiri akamuuliza unawaza nini? Ebu ngoja, nawe unataka kuwa na gari kama hili eehh? Mvulana akamjibu HAPANA....NATAKA KUWA KAMA KAKAYAKO!!!
Showing posts with label mawazo. Show all posts
Showing posts with label mawazo. Show all posts
Tuesday, July 21, 2015
Wednesday, December 11, 2013
TUSISOME MAWAZO YA WENGINE!
Ni hatari kwa mtu kudhani kwamba, anajua kila ambacho kinaendelea kwenye mawazo au hisia za mpenzi wake. Kuna uwezekano mkubwa hisia zako zinaweza zisiwe sahihi, kama ambavyo mara nyingi imekuwa ikitokea. Kuna migogoro mingi ambayo chanzo chake ni hisia potofu, hisia zitokanazo na mtu kujaribu kuingia kwenye mawazo au hisia za mwenzake.
Hebu fikiria, umeingia ndani mwako kutoka huko utokako. Unamkuta mumeo/mkeo akiwa amekunja uso. Kabla hujamuuliza chochote unaanza kufikiria kwamba, amekasirika kwa sababu leo umechelewa kurudi nyumbani kwa nusu saa tu. Unaanza kuwaza kwa kulaani kwamba, mumeo/mkeo siyo mtu wa maana kwa sababu ya wivu. Unaweza kufikiria kwamba, usiku huo utamwambia ukweli na kama ni kugombana ni afadhali iwe hivyo, halafu unamuuliza "Vipi mbona uko hivyo, nini tena?"
Mumeo/mkeo anakujibu "Hapana, nina taarifa mbaya, nimesimamishwa kazi kutokana na tuhuma fulani...." Unabaki ukiwa umepanua mdomo, kwa sababu uliingia kwenye mawazo yake na ukawa umekosea sana. Mfano huu ni wa jambo dogo, kuna wakati tunaweza kuingiza mawazoni mwetu fikra kwamba, wenzetu hawatupendi kwa kudhani kwetu kwamba tunaweza kujua yale yanayoenda mawazoni mwao. Kutokana na kufikiri kwetu hivi, tunaweza kuanza kufanya mambo ambayo sasa ndiyo yatapelekea wapenzi wetu kuacha kutupenda.
HABARI HII NIMEITOA KWENYE KITABU CA MAISHA NA MAFANIKIO KILICHOANDIKWA NA MUNGA TEHENAN...JITAMBUE
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Hii huwa inatokea mara nyingi sana na watu wengi wamepoteza marafiki zao kwa hili jambo la kusoma mawazo...ni bora kuuliza....

Thursday, November 28, 2013
MAISHA YA NDOA:- NIMEULIZWA SWALI HILI NA RAFIKI/MFANYAKAZI MWENZANGU!!!!
AKIWA MAWAZONI
Habari za leo Yasinta, ni siku nyingi hatujaonana. U- hali gani? Vipi familia ni wazima wa afya? Nikamjibu, salama tu na familia wote wazima. Sijui wewe na familia yako? Akaguna...mmmhhh! Sina uhakika, sijisikii vizuri niko katika mawazo mengi. Sijisikii raha kabisa kuwa na mume wangu. Lakini ni ajabu kwa kuwa huwa hawi nyumbani muda wote. Anafanyia kazi zake mbali kidogo anaweza akawa hayupo nasi wiki moja au mbili. Kwa hiyo ilibidi nimfurahie/tufurahiane arudipo lakini ni kinyume. Yasinta, mimi bado kijana..38 na yeye 35, nipo njia panda, sifurahii maisha niliyo nayo. Pia mwenzangu naye haonyeshi kama ananijali. Nifanye nini? Nisaidie?Duh! Hapo Kapulya akabaki hoi maana ushauri wangu.....si wa kiataalamu wa mambo ya ndoa. Nikakumbuka Maisha na Mafanikio, kuwa nikiweka hapa kwa pamoja tutaweza kumsaidia rafiki yangu. Na ndio maana nawaombeni tujadili kwa pamoja. Kwani kesho laweza kukupata wewe au mimi au yule n.k. Nawatakieni kila la kheri na mjadala mwema. SIKU IWE NJEMA......Kapulya
Wednesday, August 21, 2013
BINADAMU NA MAZINGIRA:- KUFANYA UAMUZI NI MUHIMU KATIKA MAISHA
Nimeamka na kama kawaida nikiwa na mawazo mengi kichwani, mmmhhh nikaona ngoja niende kukimbia ili kuweza kufanya takafari. Unajua unapokimbia au tembea mstuni unaweza kuchanganua mawazo vizuri sana maana kupo tulivu. Basi nikaanza kuaendelea kuwaza hili ambalo ni muda sasa nilikuwa nikiliwaza.:- Linahusu jinsi ilivyo muhimu kufanya uamuzi...Hivi ndivyo nilivyowaza:-
Nikaanza hivi, Maish huenda bila kuamua? na nikajipa jibu mmmh:- Maishahayaendi hivyo na hata siku moja haijatokea mtu asiyejue anataka nini maishani kufanikiwa au kutulia. Kama mtu ameamua kufanya biashara kwa mfano ya genge basi inabidi ajizatiti sana na biashara hiyo na aipange mipango yote ya kuikuza.
Na nikajiuliza je kama mtu anataka kusoma afanyeje? Kama mtu ameamua kusoma masomo fulani au kufanya kazi aina fulani, basi inabidi azingatie hilo na wala asiyumbe.
Kila siku huwa tunasikia watu wakisema , "yule jamaa alianza kuuza chapati na vitumbua tu, lakini angalia sasa alivyotajirika ana mabasi na maduka mji mzima". Au mfano mwingine utasikia wakisema "yule jamaa alianza masomo yake kwa njia ya posta tu lakini sasa yupo chuo kikuu". Hizi kauli huwa zinatamkwa sana lakini bila shaka hatujawahi kujiuliza inakuwaje hadi mtu kama huyu kufikia juu kiasi hicho kutoka alipoanzia ambako wengi wanadhalau na kukata tamaa?
Kwa hiyo hapa nikagundua kwamba:- Tukianza kujiuliza sasa tutajua kwamba sababu kubwa ni mpango inayotokana na kujua kwamba anataka kitu gani maishani mwao. Kwa sababu wanajua wanakokwenda wanachokitafuta, hata mambo yakienda kombo watangángánia tu kufanya shughuli zao. Wale wasiojua wakiyumba kidogo tu huacha kile wakifanyacho na kukimbilia kingine.
UJUMBE:- Ninachotaka kusema hapa katika maisha mtu unatakiwa kuwa malengo hata kama malengo hayo utafanikiwa baada ya miaka kumi. Kwa kuwa ni malengo ndiyo ambapo utaweza kwanza kutulia na baadaye kufika kule unakokutaka
KAMA HUJAWEKA MALENGO KWA UNAYOTAKA KUYAFANYA KATIKA MAISHA FANYA SASA.
NAWATAKIENI KILA LA KHERI NA TUSIWE NA TABIA YA KUKATA TAMAA: KAPULYA

Tuesday, June 4, 2013
MILA NA DESTURI:- NI WAZO LA LEO KUTOKA KWA DIARY YANGU....EBU SOMA HAPA CHINI!!!
Katika pitapita zangu kila siku nakutana na mengi sana katika blog nyingi na hivi karibuni nilikuwa nimepita hapa na nikakutana na WAZO la mwanablog mwenzetu nimelipenda wazo lake nami nikaona si mbaya kama nikaleweka hapa ili kueneza wazo lake.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
WAZO LA LEO: Mila na desturi zipo, na tumezikuta kwa
wazee wetu, zipo nyingi, na nyingi hatuzijui tena kwa vile huenda hazikuwezekana
kutekelezeka. Lakini kuna mambo mengi mazuri tumeyapuuzia, na kwa kufanya hivyo
tumejikuta tukipata taabu sana,…nachukia kwa mfano wa kutafuta mchumba, kabla
mtu hajaoa au kuolewa, wazee wetu walikuwa wakihakikisha kuwa mke au mume wa
kuoa au kuolewa anatafutwa kwa kufanyika uchunguzi wa kina kwenye familia
anayotoka…ni ni hekima yake, ni kuwa kwa kumpata mume au mke bora ni kwa ajili
ya kizai bora, na matokeo yake ni kuwa na familia bora na hili litaweza kujenga
taifa lenye amani, hili tumelipuuza, na matokea yake ndio haya..
Pia wazee wetu walikuwa wakiangalia kuwa huyo anayeolewa au
kuoa, hana matatizo yoyote ya kiafya au ya kurithi, au tabia za kishirikina, au
tabia zozote mbaya…haya yalikuwepo na ukiyachunguza kwa makini utayaona kuwa
yalikuwa na faida zake, lakini huenda haya na mengine mengi hayapo tena
tumeyapuuza.Wazo langu la leo. Zipo mila nzuri, tuzifuate, na kama zipo mila potofu, tuziache, au tuziboreshe ziwe bora zaidi, lakini tusisahau kabisa mila na desturi zetu zenye hekima ndani, na kukimbilia mila na desturi za wenzetu,….kwanini tupuuze mila zetu, ….huo ndio utamaduni wetu na anayeacha utamduni wake ni mtumwa.
NIWATAKIENI JUMANNE NJEMA NA KILA MTAKALOTENDA LIWE NJEMA...UJUMBE TUPENDANE....KAPULYA WENU
Thursday, May 23, 2013
UJUMBE/FIKRA WA/ZA LEO!!!
Katika dunia huwezi kuishi maisha bora kama una akili/mawazo hasi/finyu.
NAWATAKIENI WOTE SIKU NA KAZI NJEMA!!!
NAWATAKIENI WOTE SIKU NA KAZI NJEMA!!!
Wednesday, May 8, 2013
UJUMBE WA LEO NI HUU:- MAISHA NI ZAWADI!!
Leo kabla ya kusema neno baya, mfikiria mtu ambaye hawezi kusema.
Kabla ya kulalamika kuhusu ladha ya chakula, fikiria mtu ambaye hana kitu cha kula. Kabla ya kulalamika kuhusu mume wako au mke wako, fikiria mtu ambaye amliliaye Mungu kwa ajili ampe rafiki. Leo kabla ya kulalamika kuhusu maisha. Fikiria mtu ambaye alikwenda mbinguni mapema mno amekufa mapema mno. Kabla ya kunung'unika kuhusu umbali gani unaendesha gari lako, fikiria mtu ambaye anatembea umbali huo kwa miguu yake. Na wakati wewe ni mchovu na ulalamikapo kuhusu kazi yako, fikiria wale wasio na ajira, walemavu, na wale ambao wanataka wangekuwa na kazi kama yako . Na wakati mawazo yanakutawala na kukufanya uwe na huzuni, tabasamu na ufikiri. Wewe ni hai na bado upo.
TUWE NA UHAKIKA NA TUFIKIRI/TUWAZE KWA UHAKIKA!!!! SIKU NJEMA KWA WOTE MTAKAOPITA HAPA.

Thursday, August 9, 2012
FIKRA/WAZO LA LEO:- UTOFAUTI WA BINADAMU JINSI ULIVYO!!
Halafu hii ya kuwa na HASIRA ZA HARAKA ambazo watu wengi inakuwa ngumu kusamehe hata kitu kiwe kidogo kwako kinakuwa kikubwa. Sababu kubwa wanakuwa wameumizwa sana na yule aliyemuumiza mwenzake anaona si umizo/maumivu. Lakini kuna wengine ni wepesi sana kusamehe hata iweje sasa sijui wanasamehe kweli au?
SWALI LANGU ambalo nimekuwa nikijiuliza kila siku:- Je? kama wote tungekuwa hivyo dunia hii ingekuwa? Na Je? kundi lipi ni jema?
Tuesday, July 3, 2012
UJUMBE WA LEO NI HUU:- MAISHA NI ZAWADI!!
Leo kabla ya kusema neno baya, mfikiria mtu ambaye hanawezi kusema.
Kabla ya kulalamika kuhusu ladha ya chakula, fikiria mtu ambaye hana kitu cha kula. Kabla ya kulalamika kuhusu mume wako au mke wako, fikiria mtu ambaye amliliaye Mungu kwa ajili ampe rafiki. Leo kabla ya kulalamika kuhusu maisha. Fikiria mtu ambaye alikwenda mbinguni mapema mno amekufa mapema mno. Kabla ya kunung'unika kuhusu umbali gani unaendesha gari lako, fikiria mtu ambaye anatembea umbali huo kwa miguu yake. Na wakati wewe ni mchovu na ulalamikapo kuhusu kazi yako, fikiria wale wasio na ajira, walemavu, na wale ambao wanataka wangekuwa na kazi kama yako yako. Na wakati mawazo yanakutawala na kukufanya uwe na huzuni, tabasamu na ufikiri. Wewe ni hai na bado upo.
TUWE NA UHAKIKA NA TUFIKIRI/TUWAZE KWA UHAKIKA!!!!
TUWE NA UHAKIKA NA TUFIKIRI/TUWAZE KWA UHAKIKA!!!!
Tuesday, February 28, 2012
UJUMBE WA LEO!/AU NISEME NI WAZO!!
Ndo ndo ndo si chu ru ru; Ni kwamba ukiwa mwenye ndo ndo ndo au chu ru ru, si jambo la busara kubughudhi au kujigamba mbele ya wenzako. Kwa sababu hayo yote yanategemea uwezo wa Mungu. Na ndiyo tofauti iliyoko katika maisha
Saturday, February 18, 2012
FIKRA/WAZO LA JIONI YA JUMAMOSI HII!!!
1. Je?Kuna mtu yeyote amewahi kukuambia ni jinsi gani una umuhimu kwa wengine?
2. Unajua ya kwamba kuna mtu/watu wanatabasamu kwa upendo wako wa kweli?
3. Je kuna mtu yeyote amewahi kukueleza ni kiasi gani anakupenda? Basi, leo rafiki yangu nakuambia. Naamini ya kwamba bila kuwa na rafiki utakosa mengi. Uwe na jioni/siku njema , nina furaha ya kuwa sisi ni marafiki. URAFIKI UENDELEE NATUMAINI SIKU YAKO ITAKUWA/IMEKUWA NJEMA..NA ITAENDELEA KUWA NJEMA. KAPULYA.!!!

Thursday, February 9, 2012
HIVI KWANINI WANAPOJENGA/TENGENEZA HIZI BARABARA HAWATENGENEZI NA BARARA ZA BAISKELI.....
Thursday, November 17, 2011
UJUMBE WA LEO NI HUU:- MAISHA NI ZAWADI!!
Kabla ya kulalamika kuhusu ladha ya chakula, fikiria mtu ambaye hana kitu cha kula. Kabla ya kulalamika kuhusu mume wako au mke wako, fikiria mtu amnbaye amliliaye Mungu kwa ajili ampe rafiki. Leo kabla ya kulalamika kuhusu maisha. Fikiria mtu ambaye alikwenda mbinguni mapema mnoamekufa mapema mno. Kabla ya kunung'unika kuhusu umbali gani unaendfesha garilako, fikiria mtu ambaye anatembea umbali huo kwa miguu yake. Na wakati wewe ni uchovu na ulalamikapo kuhusu kazi yako, fikiria wale wasio na ajira, walemavu, na wale ambao wanataka wangekuwa na kazi kama yako yako. Na wakati mawazo yanakutawala na kukufanya uwe na huzuni, tabasamu na ufikiri. Wewe ni hai na bado upo.
TUWE NA UHAKIKA NA TUFIKIRI/TUWAZE KWA UHAKIKA!!!!
TUWE NA UHAKIKA NA TUFIKIRI/TUWAZE KWA UHAKIKA!!!!
Thursday, October 6, 2011
FIKRA/WAZO LA JIONI HII!!!
1. Je?Kuna mtu yeyote amewahi kukuambia ni jinsi gani una umuhimu kwa wengine?
2. Unajua ya kwamba kuna mtu/watu wanatabasamu kwa upendo wako wa kweli?
3. Je kuna mtu yeyote amewahi kukueleza ni kiasi gani anakupenda? Basi, leo rafiki yangu nakuambia.
Naamini ya kwamba bila kuwa na rafiki utakosa mengi.
Uwe na jioni/siku njema , nina furaha ya kuwa sisi ni marafiki.
URAFIKI UENDELEE NATUMAINI SIKU YAKO ITAKUWA/IMEKUWA NJEMA..NA ITAENDELEA KUWA NJEMA.

Thursday, June 23, 2011
MIAKA NANE YA NDOA, LAKINI HAYA MAUZA UZA NINAYOYASHUHUDIA NABAKI KUJIULIZA, TATIZO NI MALEZI AU NI WAPAMBE?
Ndio, leo hii natimiza miaka nane ya ndoa, lakini nikiwa peke yangu.Sio kwamba mwenzangu katangulia mbele ya haki, au amesafiri, la hasha,
yupo, tena hapa hapa mjini, yu buheri wa afya kabisa.
Siku kama ya leo, ilikuwa ni furaha isiyo kifani mimi na mume wangu
tulikuwa tumesimama madhabahuni tukila kiapo cha ndoa mbele ya wazazi
wetu, ndugu, jamaa na marafiki. Nakumbuka nilikuwa nimemuangalia mume
wangu usoni wakati alipokuwa akitamka yale maneno ya mwisho ya kiapo
yasemayo, “mpaka kifo kitakapotutenganisha” Alikuwa akionekana dhahiri yale maneno yalitoka katika moyo wake ambao
ulijaa upendo wa hali ya juu, upendo ambao kwangu mimi niliuona
dhahiri ni maalum kwa ajili yangu. Nilimuamini sana mume wangu tangu
aliponitamkia miezi kumi na nane iliyopita kwamba ananipenda na
angependa tuoane.
Naikumbuka vizuri sana siku nilipokutana na mume wangu, ni siku ambayo
kamwe sitakuja kuisahau katika maisha yangu, sijui nisemeje lakini
ninachoweza kukushirikisha wewe msomaji ni kwamba, huyu alikuwa ndiye
mwanaume wa kwanza kukutana naye na moyo wangu kulipuka katika penzi
zito lisilo na mfano.
Mwanzoni mwa maisha yetu ya ndoa, nilianza kuhisi jambo, kwani
nilianza kushuhudia ndugu wa mume wangu wakiwa ndio washauri wakuu wa
mume wangu. Nilijikuta kila mara nikiwa nimeachwa nje kwa kila jambo,
yaani nilikuwa sishirikishwi kabisa katika mambo muhimu ya kifamilia
jambo ambalo lilikuwa linaniuma sana.
Kwa kuwa mume wangu ana uwezo kifedha kwa kiasi fulani, amejikuta
akiwa amezungukwa na ndugu kiasi kwamba wao ndio wamekuwa wakimtegemea
kwa kila kitu mpaka kusomeshewa watoto, na wanahisi labda ndugu yao
angeweza kuwasaidia zaidi, kama sio uwepo wangu yaani kuolewa kwangu.
Nadhani hapo nyuma alikuwa akiwapa misaada mingi sana na huenda tangu
anioe kumetokea upungufu wa misaada tofauti na zamani kwa sababu ya
majukumu ya kifamilia ambayo hakuwa nayo hapo nyuma.
Katika kila ndoa kama mnavyojua kuna kutofautiana kimitizamo na
kukwaruzana kwa hapa na pale kitu ambacho hakiepukiki. Ila kitu
kilichokua kina ni sikitisha ni pale tu mwenzangu anapokua hajali
ushauri wangu na kufata ule wa ndugu zake.
Nilipokuwa najaribu kumshauri mwenzangu, anakuwa ni mkali kupindukia,
ilifika mahali nikajiona kama mtumishi wa ndani.
JUU YA KIDONDA UKAWEKWA MSUMARI WA MOTO
Nikiwa bado nasakamwa na yeye mwenyewe pamoja
na ndugu zake, na kama hiyo haitoshi mnamo Januari mwaka
huu nikampoteza baba yangu.
Ulikuwa ni msiba mzito sana kwangu, kwani, baba yangu alikua kama
ndiye baba wa mume wangu, ametusaidia sana walau kufikia hapa
tulipofika. Alikuwa ni baba mwenye busara sana na mwenye upeo wa hali
ya juu katika masuala ya kifamilia. Alikua akitatua matatizo yetu
mengi sana pale tunapokwaruzana na kutaka kusawazishwa ili maisha
yapate kuendelea.
wakati tunajiandaa na kumaliza 40 tangu baba yangu afariki, siku moja
akaja dada yangu kwa baba mkubwa ambaye ameolewa na mjomba wa
mume wangu. Dada yangu ambaye nilitarajia angekuwa upande wangu, alinitamkia bila kutafuna maneno kuwa wanafamilia ya mume wangu wamefurahi sana na pia
kufanya sherehe baada ya Baba yangu kufariki kwani sasa matakwa yao ya
mimi kuachika yatatimia, hakuishia hapo alitoa maneno mengi ya
kashfa dhidi yangu. Wakati wote mie nilibaki kimya nikiwa siamini kile
kinachotokea mbele yangu.
Baada kusema yale aliyosema na roho yake kuridhika aliondoka huku
akiendelea kunipiga vijembe. Nilibaki pale kwenye kiti kama
walivyonikuta nikitafakari juu ya kadhia ile….. Naam baada a
kutafakari mtiririko wa matukio yaliyopita kati yangu na mume wangu
tangu baba yangu afariki nilianza kuamini maneno ya ndugu zake. Kwani
tangu baba yangu afariki nilianza kuona mwenzangu anabadilika,
hanijali tena na alikuwa na majibu ya ovyo ovyo hata kama namuuliza
jambo la msingi. Nadhani alikuwa ananiheshimu japo kwa kiasi kidogo
kwa sababu ya kumuogopa baba, na kwa kuwa baba ameshafariki, sasa ni
nani nitamkimbilia ili kutaka kusawazishwa pale tutakapokuwa
tunatofautiana………..Nikajua sasa nimekwisha, nilijikuta nikitamka
maneno hayo kwa sauti, nilishtuliwa na sauti yake akinijibu, “ni bora
umelifahamu hilo mapema” hata sikujua aliingia pale ndani saa ngapi?
Hata sikumjibu, nilibaki kumwangalia tu kisha nikaguna, niliingia
chumbani na kujitupa kitandani, ambapo nilipitiwa na usingizi mzito.
Nilishtuliwa na mwenetu pekee wa kiume ambaye ndio alikuwa ametimiza
miaka 6, alikuwa amerudi kutoka shule. Niliamka na kumkumbatia
mwanangu huku machozi yakinitoka. Mwananu alishtuka na kuniuliza,
“mama unalia?” Nilimdanganya kuwa nimemkumbuka babu yake, yaani baba
yangu, mwanangu aliniambia pole na nilimuona dhahiri na yeye akiwa
amegubikwa na uso wa huzuni.
Sikujua kwamba ule ulikuwa ndio mwanzo wa Segere, kwani baada ya
kumaliza 40 ya baba siku kama ya 5 hivi, nakumbuka ilikuwa ni Februari
18, 2011, ulizuka ubishani kati yangu na mume wangu ambao ulizua mzozo
mkubwa tu. Nilijikuta nikapandwa na hasira na kumbwatukia yale maneno
yote niliyoambiwa na ndugu zake.
Mwenzangu katika hali ya taharuki alikasirika sana na nilishangaa
kumuona akichukua baadhi ya nguo zake chache na vyeti vyake akatia
kwenye gari na kuondoka zake, kwa kuwa ilikua usiku wa manane
nikampigia mama mkwe simu kumueleza, maana lolote laweza tokea. Kwa
ufupi mama hakuchukua hatua yeyote ile, na wala hakuja kwangu kujua
sababu ya mume wangu kuondoka katika mazingira ya kutatanisha.
Hata hivyo nililala nikijipa moyo kuwa huenda atarudi kwani alikuwa
amekunywa pombe kidogo, na labda kutokana na hasira na ndio maana
akaamua kuondoka, ingawa jambo lile kwa kweli lilinishtua kwa sababu
tangu tumeoana haijawahi kutokea tukatofautiana kiasi cha mume wangu
kuikimbia nyumba yake. Ndugu msomaji labda unaweza ukashangaa
nikikueleza kwamba mpaka leo hii ambapo ndoa yetu inatimiza miaka 8
sijamtia machoni mume wangu.
Juhudi za kumsihi mama mkwe atusuluhishe zimegonga mwamba kwani
alinitamkia waziwazi kwamba amemchukua mtoto wake na anaishi naye
nyumbani kwake mpaka hasira zitakapo muisha! Alienda mbali zaidi na
kudai kwamba haoni sababu ya kukaa kikao maana hakuna mtu katika ukoo
wangu ambaye wanaweza kumuita na kuongea naye!
Kauli hiyo iliniuma sana. Nilijiuliza, hivi ina maana mimi kufiwa na
wazazi wangu hakuna ndugu yangu anayestahili kuthaminiwa na ndugu wa
mume wangu? Je ina maana hata yale maneno waliyonieleza kuwa
wamefurahia baba yangu kufariki ni kweli?
NAJIULIZA!
Je nifanyaje? Nianze mchakato wa kudai talaka ili niwe huru? Kwa kweli
sina uhakika hata kama tukisuluhishwa sidhani kama tutaweza kuishi kwa
amani, maana kuishi na mtu huku ukiwa unajiuliza je tukigombana
ataondoka tena? na hiyo kama ataondoka nitakuwa na hali gani? mgonjwa?
sina kazi? sina uwezo wa kutunza mtoto? Maswali ni mengi kwa kweli.
Jambo hili linaniumiza sana maana nilijua nimekwisha pata asilimia
kubwa ya vitu ambavyo nilikua navihitaji katika maisha kwa mfano
tayari nimeshapata mume, mtoto, kazi nzuri kwa hiyo nilichokua nawaza
ni maisha ya kiroho, lakini sasa imenilazimu nirudi tena kujipanga
upya.
Dada Yasinta nimeona nikutumie mkasa wangu huu ili kuwashirikisha
wadau wa kibaraza chako cha MAISHA NA MAFANIKIO, kibaraza ambacho mimi
ni msomaji mzuri na nimekuwa nikifuatilia mijadala mingi unayoiweka
hapo ambayo inawavutia wasomaji wengi ambapo maoni na michango
inayotolewa ni darasa tosha.
Ni imani yangu wasomaji wa kibaraza hiki watatumia busara zao na kutoa
maoni na mitizamo yao kwa uhuru na haki bila kupendelea upande wowote.
Sikueleza hayo hapo juu ili kujidhalilisha, bali kutaka kupata
suluhisho ya kile ambacho nakabiliana nacho nikiamini kwamba sisi kama
binaadamu kuna wakati tunahitahi ushauri kutoka kwa wenzetu ili tumudu
kukabiliana na changamoto za maisha.
Natanguliza shukrani zangu za pekee kwako na kwa wadau wote wa Blog
popote pale Duniani.
Ni mimi msomaji wako.
Dada Gly
Monday, May 23, 2011
Saturday, January 1, 2011
UJUMBE/WOSIA KUTOKA KWA BABA YANGU WA KWA MWAKA MPYA 2011
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda toka mwaka jana mpaka mwaka huu mpya. Bado ninawaza kama nilivyowaza nilipokuwa mwaka mmoja . Kwa nini hakubadiliki rangi kama ni mwaka mpya?Nachotaka kusema ni kwamba: Nina ujumbe ambao nimepewa na baba yangu leo katika kuuanza mwaka huu 2011. Kwanza aliniuliza Kama najua Mungu ameiumba kwa kusudi gani?
Nikashindwa kumjibu na yeye akasema atanisaidfia kujubu.na majibu yaka ni haya:-
1. Kujua yeye ni muumba wetu.
2. Tumpende kuliko vitu vyote.
3. Tumtumikie kadiri ya wito wetu.
4. Na mwisho ni kwamba ili tuweze kufuka mbinguni.
Halafu akaendelea kunieleza ni kwamba Mungu anajua kama unamtendea kama unamtendea wema na si lazima uende kanisani ndo kumtendea Mungu mema hapana . Ni kwamba unaweza kumtendea jirani yako kitu na hapa ndipo utakuwa umetenda jema, kumwona mtu kama alivyoo, kumwalika/tembela mtu asiye na uwezo.nk nk. maneno haya yamenipa tafakari sana na nimeona niweka hapa ili mnisaidie kutafakari ujumbe huu.
Sunday, March 22, 2009
NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA WOTE
Anayekataa kufundishwa anajidharau mwenyewe,
Bali anayekubali maonyo hupata busara.
Aendeye kwa unyofu huenda salama,
Bali apotoshaye njia zake atajulikana.
Malezi bora ya watoto wetu ndio msingi imara wa taifa la kesho.
NA PIA
Binadamu tunapanga mipango yetu,
Lakini kauli ya mwisho ni yake Mwenyezi Mungu.
Ana heri mtu yule amsikilizaye,
Akisubiri siku zote mlangoni pangu,
Akingoja penye vizingiti vya milango

Subscribe to:
Posts (Atom)