Monday, May 23, 2011

TUIANZE JUMATATU HII KWA MSEMO/ UJUMBE HUU!!!

Macho yangu yanameremeta, midomo yangu ina tabasamu,

Lakini huzuni ndani yangu hakuna awezaye kuona....

Jumatatu njema!!!!!

8 comments:

emu-three said...

Moyo wangu unadunda-dunda, ndilo la muhimu, usipodundadunda...oooh!
Jumatatu njema dada Yasinta!

Mustapha MaDish said...

Nimeupenda huo msemo maana kiukweli ndivyo ambavyo tunapaswa kuishi hasa kwa wakati huu,Maana hata ukionyesha mbele ya kadamnasi wengi wao watangung'ong'a tu kama si kukucheka..!!

Simon Kitururu said...

Jumatatu njema Yasinta!

Rachel Siwa said...

Asante da Yasinta kwa maneno mazuri na jumatatu njema kwako na familia pia.

Goodman Manyanya Phiri said...
This comment has been removed by the author.
Goodman Manyanya Phiri said...

Ukingojea furaha ili ucheke, basi labda utacheka huko mbinguni. Maana duniani ni huzuni mtupu; lakini dawa yake ni kulekule kucheka.

Wiki njema kwenu wote!

Penina Simon said...

Hv kweli waweza kuwa macho yana furaha na midomo lakini moyoni ukawa na huzuni?

Goodman Manyanya Phiri said...

@Penina

Hio ndiyo siri ya maisha, Penny! Pia ni uchamungu kabisa! Na wahenga wanathibitisha kwamba jino pembe. Hivi wewe kweli unafikiri wote wanaochekelea nawe mara wanakualikia michai na vitumbua wanakupenda kweli???



43 "Mmesika kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

44 "lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,


45 "ili mpate kuwa wana waBaba yenu aliye mbinguni; maana yeye uwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

46 "Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?

47 "Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?

48 "Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu."



JAMAANI, NAMI MANYANYA "YALIOOZA KABISA" NIMENUKUU HAPA:

Kitabu cha Mathayo Mtakatifu 5:43-48, The Holy Bible in Kiswahili, Union Version, Published as Biblia Maandiko Matakatifu: Bible Society of Tanzania, 1997; Bible Society of Kenya, 1997!