Tuesday, May 31, 2011

PAMOJA NA UBABE KUMBE HAWAJIAMINI!

Kwa utafiti wangu nilioufanya wanaume wengi hawajiamini katika nyanja za mapenzi na ni wakwepaji wakubwa wa kuwajibika fuatana nami ujue.
Ni wanaume wachache wanaoweza kuoa msichana aliyekwishazaa. Lakini pia ni wanaume haohao wanaowapa wachumba wao masharti ya kwamba mpaka ubebe mimba ndio nikuoe. Na wavulana pia hata kama yeye ni muhuni kupindukia atataka msichana atayemuoa asiwe na sifa ya kuchapa umalaya na hata akioa utasikia "usipoheshimu familia yangu tutakosana". Pamoja na mlolongo huo wote. Lakini kwa wanawake ni tofauti, wanawake wanajiamini sana katika mapenzi ndio maana pamoja na kuchagua wanaume watakaowaoa wao hujali zaidi, watathiminiwa kiasi gani? Mume awe ni mwizi, jambazi, mbeba zege au mfanya shughuli yoyote unayoiona ya hovyo. ATAMPENDA na KUMTHAMINI. JIFUNZE KUJIAMINI.

23 comments:

Rachel Siwa said...

Hehehehheheeh!!!Dada wa mimi Yasinta leo umechambua haswa!kumbe ni kutojiamini kunawafanya ohh watu watasemaje oohhh nitaonekana dume bwege! oohhh wazazi wangu! Ohhhh Kitururu na emu-3 watanibeza!!!!!!!!!baadae kidogo nitakuja kuchungulia hapa,ngoja nikalale!!.

Raymond Mkandawile said...

Message sent and delivery dada Yasinta...hahahahahaaaaa

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

na wanawake msitafute kuthaminiwa, jifunze kujithamini

Simon Kitururu said...

Yasinta unaongelea DUNIA ya SASA?

Kwa maana nasikia siku hizi ``UNAPESA kiasi gani´´ inachangia sana UHENDISAMU wako au UZURI wako kama SHUGA MAMA!

Nasikia siku hizi hata uwe na watoto wangapi kama unamshiko vijana wengi watakupenda uwalee kama SHUGA mama na mpaka kukuogesha watakuogesha ukitaka.

Mapenzi ya siku hizi nasikia watu wanacheki kwanza unanini cha kuofa na atakacho MDADA kinaweza kuwa kiko kwa Mpiga zege ambaye kwa kupiga zege ni ushahidi kwa mdada kuwa yuko ngangari na sio lainilaini mpaka chini ya blanketi kukiwa na giza mdada anashindwa kustukia yuko na kidume kisa kidume laini sana kisa mayai na kulia kivulini.


Kwa hiyo:
Ukweli ni kwamba WANAUME na WANAUME ni tofauti kuanzia KIBAOLOJIA kitu kifanyacho wawe tofauti hata KISAIKOLOJIA. Kumbuka maswala ya WANAUME kuwa viumbe yanasaidiwa na MAUMBILE pia ukizingatia kimaumbile WANAWAKE ni majuzijuzi tu wamejulia kuzuia hata kupata mimba kitu ambacho ilikuwa ni tatizo sana katika kusaidia wadada kufanikiwa kiumalaya bila kudakwa kama iwezekanavyo kwa wanaume.

Na ukizingatia ni wanawake wabebao mimba na wenye sehemu za siri ambazo ni rahisi kuathiriwa kuanzia kimchubuko mpaka kikuambukizwa hata Ukimwi kwa kuwa kiumbile ndicho kimwagiwacho uteute wa watoto wakubwa wa kiume,...
... huwezi kufananisha kirahisi hivyo YA WANAUME na YA WANAWAKE.

Na KUJIAMINI kwa MTU ni kitu BINAFSI uwe MWANAUME au MWANAMKE.

Na KUJIAMINI pia kunawezaathiriwa na MTU mmoja na sio mtu MWINGINE kitu kiwezacho kufanya AJIAMINIYE mbele za KIKWETE anaweza kujikuta hata ajuayo hajiamini nayo kama yuko mbele ya MANDELA ambaye anamshemu heshima zikaribiazo kuabudu halafu MANDELA ndiye awe mpinga HOJA!

Ni mtazamo wangu tu!

@Rachel: :-)

Yasinta Ngonyani said...

Rachel! Ahsante. una bwebbwe wewe haya rudi sasa uchungulie...
Raymond!Ahsante kwa kunitembelea tembelea.
Kamala! wanawake tunajithamini na pia tunachoomba kwa wanaume ni kuthaminiwa pia.

Simon! nitanukuu hapa "Yasinta unaongelea DUNIA ya SASA?

Kwa maana nasikia siku hizi ``UNAPESA kiasi gani´´ inachangia sana UHENDISAMU wako au UZURI wako kama SHUGA MAMA!" mwisho wa kunukuu:- Hawa au afanyaye hivi basi ujue HAKUNA PENZI LA DHATI. maana kama kweli unampenda mtu kwa DHATI HASA hutajali kama yupoje na anaishi vipi. ni mtimzamo wangu.

emu-three said...

Kuna usemi usemao `kila mwamba ngoma huvutia kwake..' nikawaza sana, kwanini hata kama shati langu limechafuka kwa tope sikubali kuambiwa nina uchafu...ooh, utadai kuwa ni pambo, au sio.
Wanaume wamezaliwa kuwa waume, na wanawake wamezaliwa kuwa wake, lakini sio kila mwanaume na `mume' kitabia na kimatendo, na sio kila mwanamke ni `mke' kitabia na kimatendo...lakini mwisho wa siku wote ni wanaume au wanawake...na ni watoto wa Adamu.
Kasoro za kimaumbile,tabia nk,zipo katika kundi. Lakini uhalisia wake kama mume au mke upo pale pale, mengine ni udhaifu wa kibinadamu...au sio.
Kujiamini, hutokana na nini, akili au mwili au umbile au jinsia?
Huenda tukilijibu hili kitaalamu tutapata muafaka wa mjadala huu, Nani atusaidie kwa hili?

Simon Kitururu said...

@Yasinta: Kwani PENZI la DHATI ni lipi?

Hasa ukizingatia kuwa inasemekana PENZI sio kitu STATIC aka KITU KILICHOGANDA na ndio maana ni MTU yuleyule yasemekana awezaye kuhusishwa na KUFUKUZIA mtu , KUOA au KUOLEWA mtu kisa KAPENDA na KUMUACHA mtu/KUDIVOSI kisa tu ni siku mbali mbali na yote kitendo ndani ya mtu huyohuyo yanauhusiano na PENZI?

Kwani si inasemekana siku ya kwanza na hata ya NNE katika watu wawili kwenye uhusiano hata kama kipimo ni PENZI ukichunguza utastukia tofauti?

Na je Kati ya ajisikiavyo mtu siku ya kwanza na ya mia kipenzi kama ni tofauti ni lini hisia zake ndio zilikuwa PENZI la DHATI?

Na si penzi la DHATI mtu akika vizuri kihoja anaweza kutetea kuwa ni lile la KUMUEPUKA mtu ili ambngalau UMFIKIRIAVYO ibakie vilevile bila kuharibu kwa kuwa naye karibu na kuharibu hiyo DHATI?

Tukiachana na hilo :
Kwani DHATI ni nini?

Nawaza tu kwa sauti!:-(

Yasinta Ngonyani said...

em-3 ulichosema ni sahihi kabisa hapa na kuhusu nani atatusaidia kujibu hapa labda kaka Kaluse au kutatokea tu mmoja na kutusaidia.

Simon! kumpenda mtu kwa dhati:- ni kumpenda mtu kama alivyo YEYE sio kwa uzuri, mali nk. YAANI KAMA ALIVYO:-) NI MIMI NIWAZAVYO

Simon Kitururu said...

@Yasinta:Kumpenda mtu kama alivyo yeye ,...
...uzuri,mali , nk haiwezekani ikawa imo humohumo katika ALIVYO MTU?

Naendelea kuwaza tu kwa sauti!:-(

Yasinta Ngonyani said...

Ndiyo Simon! lakini mimi nitakachojali ni kumpenda YEYE SIO MALI ZAKE, SIO UZURI ISIPOKUWA NARUDIA TENA NITAMUHUSUDI YEYE KAMA YEYE KWA VILE NDICHO NIKITAKACHO.

Simon Kitururu said...

@Yasinta:

Asante kwa SHULE!

Yasinta Ngonyani said...

Simon! Ahsante wewe pia kwani nami nimejifunza ...ila unaruhusiwa kuwa katika mjadala zaidi kwani haujafungwa-...

Unknown said...

Emu three, naona nimehusishwa na mada hii kama mtego vile!
Ha ha ha aaaa, ngoja na mie nipige tiralila zangu hapa.

Ni hivi, kwa mtazamo wangu mada hii imekaa mkao wa kiujumla mno, na kama nikisema nijibu swali lako naweza kusema “SIJUI” lakini hata hivyo kama ukisoma mada hii na kuiangalia kwa jicho la tatu, yes I mean jicho la tatu, kuna jambo moja hapa nadhani tunaweza kujifunza wote.

Nionanvyo mie kama Shaban, ni kwamba kama tutalipima jambo hilo kwa mizania kuna ukweli kwamba huenda mzani ukalalia upande ule uitwao mfumo dume.

Ki vipi- Kwa silka tulizo nazo sie wanaume ( Ki-mfumo dume) Mada hiyo ina ukweli kwa kiasi cha kutosha, kwa sababu hayo yaliyosemwa mara nyingi ndiyo yanayotamkwa na vinywa wale wanaoamini kuwa Mwanaume ndiye kichwa cha nyumba sio ki-ushauri na kuweka uwiano wa mawazo bali kwa maamuzi ya kibabe yasiyo na busara.

Ngoja nishereheshe:

Nina maana kwamba kama mwanaume ndani ya kichwa chake ana amini kwamba mwanamke hana maamuzi wala mamlaka ya kutoa ushauri katika mambo yahusuyo familia, kauli hizo ni za kutarajiwa sana.

Kwa kujibu swali lako Bwaba Emuthree, ni kwamba Swala la kujiamini halitokani na akili, mwili, umbile au jinsia, bali linategemeana na uelewa wa mtu katika kupambanua mambo na uwezo mzuri wa kufikiri.

Nimalizie kwa kusema kwamba masuala ya uhusiano yana falsafa ndefu na ngumu sana, na ndio maana kupitia vyomba vya habari na hata Blog zetu hizi huwa tunapata habari zihusuzo jinsia hizi mbili kila upande ukishangaza kwa namna yake.

Wakati nikiandikia Gazeti la Jitambue kabla halijasamama kuchapishwa, nilikuwa nikiandika ushuhuda wa watu mbali mbali. Miongoni mwao walikuwepo wanandoa. Kuna wakati nilikuwa naweza kuzungumza na mwanandoa mwanaume akanieleza mateso anayofanyiwa na mkewe nikabaki mdomo wazi, wapo wanaume waliowahi kukiri hata kupigwa na wake zao.

Lakini upande wa pili nao naweza kukutana na mwanamke naye akawa analalamikia hali hiyo hiyo, mada kuu ikawa ni ndoa ya mateso, kupigwa kudharauliwa na wengine kuachiwa vilema vya maisha. Je tunaweza kusimama na kutuhumu kuwa upande mmoja unaukandamiza upande mwingine?

La hasha………. Tutakuwa hatuutendei upande mwingine haki…………

Haya nimemaliza longo longo zangu, ngoja niwapishe na wengine waseme yakwao.

@Ambiere Kitururu-Ulilonena nalo neno..........!

John Mwaipopo said...

kama naangalia movie vile

chib said...

Mwaipopo ha ha haaa, Kitururu, nafikiri umenena.
Na mimi je nasemaje..... Labda mkosaji huwa hakosi sababu. Kila mtu ana utafiti wake, hata kuna wanaosema pombe ni mbaya kiafya na wanatoa sababu, lakini wapo wanaokuja na tafiti zikisema pombe ni nzuri kiafya

EDNA said...

Mjadala umenoga,nimejifunza kitu kutoka kwa wachangiaji...Asante dada kwa kuiliibua hili.

Unknown said...

Ni kweli EDNA, licha ya mada, pia watu hujifunza kupitia maoni ya wachangiaji........

Goodman Manyanya Phiri said...

@Simon

Udhaifu wa sisi wanaume katika mapenzi naukubali nikiwa na kubaliana naye Dada Yasinta. Lakini baadaye namwacha yeye Da' Yasinta kwenye mataa ya stendi ya basi na kusonga mbele nawe Simon.


Mapenzi ni mali (A MATERIAL THING), hata Dada Yasinta akitaka kusema mapenzi ya dhati yapo...hamna kitu kama hicho kwani naye alipo anampenda mume wake ndiyo na tunakubali, lakini hakukutana naye jalalani akiwa mume huyo anaokota na kula uchafu wa pipa la taka, wala!


Kumpenda mtu kama ni wazo, basi tayari wanasayansi wameonyesha katika maabara wazo (au mapenzi) ni mali au MATERIAL THING.


Waliwachukua funza wa aina fulani na kuwamulikia tochi kwa kila nusu sekunde mara kwa mara; kisha wakawakausha na kuwasaga kama chakula cha funza wenzie.


Kuwamulikia tochi funza walaji, hakuna kilochotokea. (Kifupi: hamna kitu kipya au chenye mafunzo kilieliwa na funza walaji)


Baadaye wakachukua kundi jipya la funza na kuwamulikia tochi kila walipowafanya wasikie uchungu kwa matumizi ya umeme. Baada ya mara ya kumi, funza hao walikuwa wameshajifunza kwamba mwanga wa tochi unakwenda sambamba na uchungu wa umeme na walikuwa wanajikunja KILA TOCHI IKILETA MWANGA HATA KAMA UMEME HAWUKUWEPO!!!


Wanasayansi basi wakawakausha na kuwasaga funza wale wenye kujifunza na wakapewa kama chakula kwa funza wepya kabisa wasiejuwa umeme wala mwanga wa tochi.

Lakini walishangaa pia na kushangalia wanasayansi kugundua kwamba KILA TOCHI LIKIMULIKWA, funza hao walaji NAO WALIJIKUNJA MITHILI YA WALE WALIEJIFUNZA KWA JASHO LA UMEME!

Ni hivyo walivyopruvi wanasayansi kwamba mawazo, vilevile kumpenda mtu (kama wazo) ni mali tu OR A MATTER OF MATERIAL THINGS!

(Mke wake marehemu wa nchi fulani sitataja nikimwambia leo 'nampenda' ataniona kichaa, wacha lakini nikiwa dume jipya la nchi yangu, atanirukia kama ninavyosikia amewarukia wengi hata Zimbabwe huko kabla ya kumpata mteja wake wa sasa huku bondeni!)

Ebou's said...

Hiyo ni kweli dada Yasinta ila suali la kuowa mwana mke mwenye watoto kama wawili tuna sema BUY 1 GET TOW FREE. Inakuwa ni kazi na Mwana mkee ameumbwa kwa kujiamini sana Hata ukiangalia Hadithi ya Adam na Hawa pia alifanya mambo kwa kujiamini. kwasababu wanawake wingi tegemeo lao ni kwa wanaume. kwa sababu mama anajuaa baba ndio mwenyenyumba.. hii itafundisha vijana ksiri ya mafanikio ni kujiamini iwajee unakaa Ghetto na mwanamme mwezako ushindwe kuowaa bana.. hinayo imependeza dada Yasinta na mimi bakaribisha wasua kwenyee swahilivilla kwa maoni yenu kuhusu hii Video it's so funny http://swahilivilla.blogspot.com/2011/05/only-in-america-make-sure-kiddies-are.html?showComment=1306895830144#c1159396037327574167

Koero Mkundi said...

Mada kama hizi, huwa wanaume hawazipendi. Unajua ni kwa nini? Ni kwa sababu umegusa Mtima wao.

Mtu kama Kitururu, ukisoma maoni yake utajua kabisa kuwa ndio wale wale....... Yaani hakunjui kabisa kwa mdada.

Ni kweli Yasinta, hili lina ukweli kabisa, wanaume hawajiamini hasa katika Mapenzi... na ndio maana wanaposhindwa ligwaride kisha mdada akaaamua kuwa muwazi na kudai zaidi kwa kuwa hajatosheka, hiyo ni sababu tosha kwa mwanaume huyo kumpiga kibuti na kama akiulizwa sababu hatasita kusema kuwa mdada yule ni Malaya.

Wanaume wana silka ya ubabe na ujuaji, ni vigumu sana mwanaume kukiri mbele ya mkewe kuwa jambo fulani haliwezi, na ndio maana visa vingi vya wanaume kujitoa roho, kuwekwa ngeu aua hata kufungwa gerezani utakuta sabaabu kubwa ni wanawake, huwa hawakubali kushindwa wala kuwajibika kwa makosa yao.

Kwa mfano, inawezekana mdada asiwe na makuu, lakini akisikia kuna kidume mwenye uwezo kumzidi anamsalandia mdada, hapo ndipo utakapoona vijimambo.

Ni jambo la kutarajiwa sana kwa mwanaume kuhatarisha maisha yake ili kujionesha kuwa na yeye anauwezo wa kuwapata warembo.

KISA: Kuna mdada alidumu na jamaa katika ndoa kwa takriban miaka 8 bila kupata mtoto, visa mateso na manyanyaso kutoka mumewe na ndugu zake vilimshinda, akaamua kujiondokea.
Mungu sio Kitururu.... akampata akachumbiwa na kuolewa na jamaa mwingine, haikuchukua raundi jamaa akam-mimbisha, na hivi ninanvyoandika maoni haya anao watoto watatu na yuko katika ndoa ni mwaka wa tano sasa.

Mjamaa aliyeachwa ana kazi ya kubadilisha wanawake kila uchao na hataki kukiri kuwa ni yeye mwenye shida ya kutomudu kutia mimba!

Mara nyingi shabaha dhaifu kwa wanaume ni wanawake, na ndio maana kama mwanamke hashiki mimba mtu wa kwanza kunyooshewa kidole ni mwanamke......(Jamani tunaonewa sisi!)

Mwanasosholojia said...

Mengi yameshaongeleka, naonekana kama nimechelewa...anyway, shukrani Da'Yasinta kwa mada hii ya moto...ndiyo ni ya moto kwa kuwa inagusa "maslahi" ya kundi fulani...lakini zaidi inabainisha udhaifu...kutokujiamini...hasa katika suala la mapenzi. Nakubaliana na hoja nyingi, lakini nasisitiza kama wengine, sio wanaume wote wenye silika hiyo...na labda ukiniuliza kwa nini walio hivyo wanafanya hivyo nitakujibu tu sababu zipo nyingi lakini asilimia kubwa ya sababu inaibukia kwenye malezi hasa socialization na taasisi zake...hii inamfinyanga mtu tofauti na mwingine kadiri anavyokua..na inasawiri mtazamo wa mtu huyo dhidi ya jinsia nyingine...ni mchango wangu kwa sasa.

Simon Kitururu said...

@KOERO: Kiletacho maana kwa ASHURA labda sio kweli kina maana ile ile kwa KHADIJA!

Na apatavyo MAANA mtu MWINGINE katika kumuelewa mtu MWINGINE aongeaye kiuzoefu wake katika SWALA,...
... uzoefu wao utofautiana unaweza kuwa HAUSHABIHIANI katika hata kufananisha staili zao za kubishia JAMBO .

NI hilo TU!

Goodman Manyanya Phiri said...

@Koero

Nimefurahi kukuona kumbe wewe ni mpana na mrefu. Mungu akujalie zaidi kiakili (maana yake Wanamama wa Kiafrika wakielimika taifa ndipo litapata uhuru kamili).