Thursday, May 12, 2011

TAARIFA:- BLOGU YA MAISHA NA MAFANIKIO NA KIPENGELE KIPYA KILA JUMATANO!!



Blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwataarifu kuwa, kuanzia wiki ijayo itakuwa na KIPENGELE kipya ambacho kitakuwa ni kipengele cha MARUDIO YA MADA/MAKALA mbalimbali. Zitakuwa ni mada/makala zangu na pia za bloggers wengine. (kama wamiliki wa blogu nyingine wapo radhi nifanye hivyo) .Kwani katika kuwaza na kuwazua nimeona mtu kama unarudia kusoma/kufanya kitu mara nyingi huwa kinabaki kichwani. Nikiwa na maana ya kwamba unakuwa ndio unaelewa kwa urahisi na kumbukumbu inabaki kwa muda au milele. Pia kuna mada/makala nyingine hazijasoma na wasomaji wote. Kwa hiyo kila JUMATANO KIPENGELE HIKI KITACHUKUA NAFASI YAKE. AHSANTENI!!

8 comments:

Simon Kitururu said...

Aksante kwa taarifa Binti Ngonyani!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ni wazo zuri Da' Yasinta....

Christian Sikapundwa said...

Tunayasubili Dada Yasinta.

Unknown said...

Hongera kwa wazo hilo.

Mwanasosholojia said...

Heko, wazo zuri!

Raymond Mkandawile said...

Mie nakupongeza dada Yasinta a.k.a Kapulya kwa wazo lako zuri sana na kwa upande wangu mlango uko wazi kabisa mda wowote iwapo lipo ambalo wataka kuikumbusha jamii....good luck

Mija Shija Sayi said...

Safi sana Yasinta, wazo lako tumelipokea kwa kwa mikono miwili dada, binafsi ruksa kuchukua mada zangu wakati wowote.

Pia asante kwa kutukumbusha tabia ya kurudia rudia kusoma kwani kwa njia hii vitu hubakia kichwani, na si kubakia tu kichwani bali hata unaweza kugundua jambo ambalo uliposoma mara ya kwanza hukuligundua.

Keep it up.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mchari! Ahsante kwa kulipokea wazo langu.

Kaka Mathew! Heko nawe pia kwa kuona ni wazo zuri...
Raymond! nazipokea pongezi zako kwa mikono miwili pia nasema ahsante sana kwa ruksa katika hizi blog hakikosekani kitu cha kusoma na cha kuelimisha.

Ndugu yangu Mija.Ahsante sana kwanza kwa kuona ni wazo sasfi, pia kwa kulipokea kwa mikono miwili. Bila kusahau kwa ruksa kuchukua mada zazko.
Na mwisho ulilosema ni kweli kabisa kwani kuna wakati mtu una kuwa na haraka na unasoma kwa haraka unadhani umeelewa na unaporudia tena unaelewa tofauti...Ahsante kwa kuafikiana nami..PAMOJA DAIMA.