Sunday, May 8, 2011

SWALI :- HIVI HIZI SIKU ZA MAMA DUNIANI ZIKO NGAPI?

Mama wa Maisha na Mafanikio (aka Kapulya)



Habari za leo ndugu zanguni!
Namshukuru Mungu nimeamka salama. Ndugu zangu leo nina swali ambali nimeona niwaulize wenzangu kwani nahisi kutoelewa kidogo hapa. Ni hivi nimeamka leo nimefunga blog ya Maisha na Mafanikio na nakutana na vichwa vingi vya habari kuwa leo 8/5 ni siku ya AKINA MAMA DUNIANI. Je? ni duniani au? Maana niliposoma hapa pia hapa nk nimeona ni tofauti. Nikakumbua kama mwezi hivi umepita nilisoma kwa mwanamke wa shoka kuwa ilikuwa siku kama hii huku Uingereza. Halafu sasa nazidi kuupata utata kwani hapa niishipo hii siku itakuwa mwezi huu baada ya wiki kama mbili hivi.


Kusema kweli nahitaji msaada swali langu ni kwamba HIVI HII DUNIA SIO DUNIA MOJA ? NA KWA NINI KUNA SIKU/TAREHE TOFAUTI KAMA HIZI ZA AKINA MAMA NA AKINA BABA ? NIELIMISHENI MWENZENU....Kapulya!!

5 comments:

Rachel Siwa said...

Hapa Uingereza ilishapita,nafikiri kila nchi wana tarehe yao ya kuadhimisha siku hii,Yote kheri nami niungane na kina mama wote,Hongera kwa siku ya MAMA.

Simon Kitururu said...

Siku ya akina mama na siku ya wanawake kwangu ni kila siku ya mwaka!

Na nikisikia tu watu wameweka kasiku fulani mie sikawii tu kupongeza kwa sauti pongezi kwa akina mama.

Mimi kwangu kesho ni siku tena ya akina mama , halafu kesho kutwa nadhani itakuwa tena siku ya wanawake,....nk.

Goodman Manyanya Phiri said...

Sio kwamba ninawivu, lakini idadi ya siku hizi inaweza kuwa kero tupu.

Mara "VALENTINE": lazima akinamama watambe hata huko licha kwamba huyo Valentine alikuwa mwanaume!

Mara "SIKU YA WANAWAKE" (hata "MWEZI WA WANAWAKE" jamaani!)


Mara (kama leo Mei 8) "Siku ya Mama".


Ukichunguza sana wote hawa waliotajwa juu ni mtu huyohuyo mmoja anayenufaika. Kisa na mkasa: KATUZAA!!!


(Nilitaka kusahau, hapa kwetu ipo ingine yenye jina "TAKE A GIRL CHILD TO YOUR WORKPLACE" au kitu kama hicho!) OF COURSE, YOU GUESSED RIGHT: A GIRL CHILD IS ANOTHER EUPHEMISM FOR THE SELF-SAME "WOMAN" (ONLY AT HER MOST YOUTHFUL, IF MOST VENOMOUS TOO)!


Sasa mimi mwaka huu nimegoma kabisa! Mama-mtoto aliniambia asubuhi sana..kunikumbusha kweli: "LEO NI SIKU YA MAMA"

Nikamchunguza! Baadaye nikachunguza mfuko wa suruali yangu... nimechacha!!

Ndipo nikachachamaa kabisa! Nikamjibu: "YOU ARE NOT MY MOTHER, REMEMBER?"

lol!

KUSEMA UKWELI NILIWAACHIA WAENDE ZAO JIJINI KUJICHANA HUKO KISHA BAADAYE NIKAPOKEA SHUKRANI ZANGU! Heshima kwa wanamama (hata akiwa binti wa mwaka mmoja) ni siri kubwa kwa mwanaume!

Anonymous said...

Kwa hapa Marekani, siku ya mama (mother's day) huwa ni jumapili ya pili ya mwezi Mei. ni siku ya kuwaenzi wamama(walio na watoto) na si kila mwanamke.

Anonymous said...

Sio Kila mwanamke anasifa zakuitwa mama wengi wanatoa mimba awataki kuitwa mama kwaiyo siku ya mwanamke inausisha wanawake wote atawale wanafunzi walioko mashuleni nasiku ya mama ni kwaajili ya wanawake walio zaa na wanalea wototo wao