Friday, May 20, 2011

Changamoto ya ijumaa ya leo!!!

Nimetumiwa ujumbe huu kutoka kwa msomaji wa Maisha na Mafanikio ambaye ni mkazi wa Njombe. Pia naweza nikamwita kama kaka yangu kwa jina anaitwa Salehe Msanda. Sitaki kuwa mchoyo nimeona ni vema nikiweka hapa ili tusaidiane kwa pamoja kwani kwenye wengi ni pazuri. Pia umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Kaka Salehe alianza kama ifuatavyo:-
-------------------------------------------------------------------------------------

Dada Yasinta naomba tusaidiane katika suala hili lifuatalo

Kwanini tulio wengi tu wazito wa kuthubutu katika nyanga fulani za msingi na muhimu kwa ustawi wa mtu mmojammoja, familia na jamii kwa ujumla?. Mfano tu-wagumu wa kuwekeza kwa ajili ya kuweza kupata mahitaji yetu ya msingi katika maisha ya kila siku (chakula, mavazi, malazi na uhakika wa afya zetu) au kubadilika kutoka katika mazoea yanayohatarisha ustawi wa familia na jamii na familia, lakini tu wepesi wa kuthubutu na kutenda mambo yanayohatarisha maisha na ustawi wa mtu na jamii.

Nini kifanyike kuibadili hali hii hasa kwa sisi waTanzania? Maana nionavyo mimi katika hii dunia ya UFAHAMU NA MAARIFA, wakati wenzetu wanaendelea kugundua mambo mapya kila siku sisi tumejikita zaidi katika burudani na starehe.
Kuna umuhimu wa kukumbushana katika kuifuta lugha ongozi ya kipindi au zama hizi za ufahamu na maarifa ambayo ni kuwa na taarifa na maarifa kadiri ya uwezo wetu.
Ijumaa njema!!!!!!!

5 comments:

Simon Kitururu said...

Mie siamini kuwa WATANZANIA kiasilimia kubwa wamejikita zaidi kwenye BURUDANI na STAREHE hasa baada ya kupita nchi kedekede ambazo sio TANZANIA na zile ziiitwazo zimeendeea!

Karibu kila sehemu utakuta kuna mtu mmoja aliyebadili na ukifuatilia utastukia kuanzia aliyegundua UMEME , balbu ya UMEME trenin, jinsi HOLANDI wanavyoweza kugeuza BAHARI iwe nchi kavu, mpaka aliyegundua TAMPAX ambayo kikigunzi cha kuficha siku za mdadaau mpaka BAISKELI ,..
... mara nyingi ni mtu mmoja au wawili na sio NCHI wala watu wengi kitu kifanyacho kuwa,...
... labda dawa ya TANZANIA ni mtu mmoja!:-(
Nawaza tu kwa sauti!:-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hii ni nukuu kutoka katika kitabu kimojawapo cha Munga tehenan

emu-three said...

Kweli hoja ina mantiki...labda mimi nawaza kivingine, kuwa badala ya kufikiria kuwa na trni za umeme, barabara za chini na juu, bado tunafikiria kununua mapikipiki(bodaboda) ...maana utasafiri na ninikwenye mahandaki..
Badala ya kufikiri kuwa na umeme wa kudumu, tunafikiria kununua majenerator, maana hatuna uhakika wa umeme...umeme ni kama donda ndugu hapa kwetu.
Badala ya kufikiri kuwa na dawa , kinga..nk tunafikiria dawa za kuoteshwa....mmmh!
Bado mawazo yetu yapo kule kule...wapi arubaini na saba! Kila kitu mpaka `mfadhili'...hata kufagia, hata...nanihii...mbona nanihii hatufikirii mfadhili...NAWAZA TU DADA YANGU!

Ebou's said...

Kaka salehe Msanda Ni vema ukakumbuka kuwa, unapogundua juu ya jambo fulani ambalo limekosa mwenendo mzuri, basi utafute namna ya kuachana nalo.

Acha kurudia makosa yale yale kila mwaka na ujiulize ni kwa nini huweki akiba kutokana na kipato chako? Njia pekee ya kuepekuna na tabia hiyo ni kufuta mfululizo wa makosa hayo yenye tabia ya kujirudia na udhamirie kubadili maisha yako.


Baadhi ya watu huishi huku wakiendelea kurudia makosa katika sekta ya kiuchumi. Bila shaka hutakiwi kuwa mmoja wa watu wa aina hiyo, kaka saleh.!

Njia nzuri ya kumudu jambo hilo ni kuhakikisha unaorodhesha mahitaji yote ambayo hayalipwi kwa utaratibu wa ankara, mfano vinywaji, burudani mbalimbali, kuchangia sherehe miongoni na mengine mengi.

Baada ya kufanya hivyo hakikisha unatenga kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya dharura, mfano matengenezo ya gari iwapo umebarikiwa kuwa nalo, au hata pesa ambayo itakuwezesha kusafiri kwenda kuona mgonjwa au kuhudhuria msiba.

Watu wengi hudharau mahitaji ya aina hii na kuyaweka kando ya bajeti kwa sababu hayana umuhimu kwao.

Hata hivyo, mara yanapotokea, umuhimu wake huonekana na hapo ndio hutambua kuwa kumbe katika wakati wote kuna matumizi zaidi ya hanasa.

raynjau njau said...

Hiyo ndiyo hali halisi na hakuna la kushangaa kwa huo ndiyo mfumo wetu wa maisha ambao kwa nia njema tumeukubali.Huna sababu ya kuuliza kwanini kila nyumba mtaani kwako imewekeza katika biashara ya ulevi na siyo elimu na kila wikiendi ni bajeti ya mamilioni mangapi yanateketezwa kwa ajili sherehe za arusi na kwa nini siku hizi maziko na ghali kuliko matibabu?Kwa nini hushangai kuwa watu wapo tayari kupanda upepo huku wakijua kuwa watavuna tufani?
Wikiendi njema!!