Showing posts with label salama. Show all posts
Showing posts with label salama. Show all posts

Monday, August 8, 2011

"KAPULYA" BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO:- INAPENDA KUMSHUKURU MUNGU KUWA TUMESAFIRI SALAMA...MENGINE YANAKUJA BAADAYE:-) NIMIRUDIIII





Nimefika jana jioni .Hapa ni Jumamosi ya tarehe 6/8 nikiwa Silver Sand Dar Es Salaam.......Kapulya huyooooooo!!

Friday, December 24, 2010

SALAMU ZA CHRISTMAS KUTOKA SWEDEN!!!

Katika familia yetu mimi siwezi kuwa karibu na mti wa Chritsmas. Bahati nzuri tuna hili ua kubwa kama mti ndani ya nyumba kwa hiyo tukaona tuupambe ili uwe mti wa Christmas na hapa unaona jinsi zawadi zilivyojaa najiuliza kama nimekuwa mtoto mzuri kustahili kupata zawadi leo ...Nitawajuza



Na hapa ndipo tutakapo kaa na kula mlo wetu wa christmas pamoja karibuni jjamani tujumuike!!

Na hapa ndio maakuli yenyewe kwa kutumia mikono yetu wenyewe. Ila pilau halikuwepo, labda kesho.

Na hapa sherehe imeanza , kama upo karibu unakaribishwa sana. Skål och GOD JUL ALLIHOPA!!!

Wednesday, May 26, 2010

Maji safi na salama ya kunywa kwa kutumia jua!!

Maji ni muhimu kwa kila binadamu, maji bila wadudu ni muhimu zaidi. Wengi kwa kuatapa Kupata maji salama tunahitaji kuchemsha. Lakini sasa unaweza kupata maji bila kutumia kuni au mkaa sio ndoto, kama unatumia "Solvatten". soma hapa

Thursday, February 26, 2009

NATAKA KUMSHUKURU MUNGU KUWA NIMESAFIRI SALAMA

Habari za siku chache wanablog na wasomaji wote napenda kuchukua nafasi hii na kusema ya kwamba, nimesafiri salama na nimerudi tena hapa kijiwe. Ili niweze kuwa nanyi pia napenda kuwashukuru woooote kwa sala na upendo wenu nakujua mlikuwa mnaniombe nisafiri salama. Ni hayo tu.

Wednesday, December 31, 2008

NIMEFIKA SALAMA

Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kunilinda mimi na familia yangu katika safari hii ndefu. Tumefika salama mpaka hapa Dar, safari bado inaendelea. Yaani mpaka Songea kama mnavyojua natoka Songea mngoni. Raha sana kuwa nyumbani joto, watu wachangamfu halafu nyumbani ni nyumbani. Leo sisemi kazi kweli kweli ila nasema raha kwelikweli.

Kwa hiyo napenda kuchukua nafasi hii kwa kuwatakieni wootee HERI SANA KWA MWAKA MPYA 2009. Ila mimi nafaidi zaidi kwa wale wote waliokuwa kwenye nchi za baridi. Ha, ha, haaaaa.