Wednesday, February 13, 2019

UJUMBE WA LEO- TOFAUTI BAINA YA SHULE NA MAISHA.....

Shuleni unajifunza somo/masomo na baadaye unapata mtihani. LAKINI- Katika maisha , kuna mitihani ambayo tunajifunza masomo.
PANAPO MAJALIWA , Kapulya wenu!

Tuesday, February 12, 2019

KUMBUKUMBU: NI SHAIRI LA SIKU NYINGI SANA NILIIMBA NIKIWA DARASA LA NNENililiimba kipindi niko shule ya msingi ,nakumbuka ni darasa la nne na mpaka leo takribani miaka 30 zaidi bado nalikumbuka. Bila shaka shairi hili litakukumbusha yaliyo mema ya kipindi cha nyuma. Na cha kufurahisa zaidi kitabu hiki ambacho hili shairi lipo ninacho:-)

Monday, February 11, 2019

HIZI ZITAKUWA PICHA ZA MWZI HUU WA PILI

Nimeamka asubuhi ya leo na nikawa na hamu ya kula yai  kwa kawaida huwa napenda kula yai moja tu lakini lakini leo macho yangu yakakutana na maajabu haya katika yao moja nikaona ni mawili. Cha ajabu yao halikuwa kubwa kuliko kawaida....nimeyale yote :-)  Mara nikakumbuka kuna mtu alinitumia picha ....
...picha maajabu yaliyotokea mgomba mmoja umezaa mikungu minne ya ndizi. Hakika hii ni kali ya mwezi ..

Monday, February 4, 2019

TUANZE MWEZI HUU WA PILI KWA PICHA HII:-UMOJA NI NGUVU

 Kuna wengi watakumbuka hii kazi ya kutwanga  sio hapo zamani tu hadi sasa hasa vijijini bado wana enzi utamaduni huu. Lakini jamii ya sasa sijui kama kuna anayejua kinu   na mwichi ni nini...najivunia kuwa mmoja ninayeuenzi utamaduni huu pia hata kizazi changu. NAWATAKIENI MWEZI MPYA HUU UWE MWEMA.


Thursday, January 31, 2019

SI KILA MARA UNAPASWA KUUSIKILIZANi mara nyingi sana tumeshindwa kufika mahali tulipopaswa kufika kwa wakati. Ni mara nyingi pia labda tumefanya makosa makazini au kwenye shughuli zetu za kila siku,yote hii ni kwasababu ya kuusikiliza kila wakati. Tumeshindwa kuwa na sauti kwake,unatupelekesha sana....

Maisha yanakwenda kwa kasi kweli kweli. Kila siku shughuli na mahitaji yetu yanaongezeka. Muda wa kufanya kazi unaongezeka....

Kadiri muda wa kufanya kazi unavyoongezeka ndivyo muda wa kupumzika nao unapungua,mahitaji mapya yanaongezeka. Kadiri siku zinzavyokwenda ndivyo mahitaji mapya yanaibuka zaidi kila siku,vile tulivyo navyo leo  tunaviona havifai tena tunataka vipya....

Ni kweli miili yetu nayo inachoka sana na kuhitaji pumziko kwa mfano ili kukusanya nguvu mpya ya kuendelea kuwajibika. Lakini jambo moja kubwa pengine tusilolijuwa ni kwamba mwili haujawahi kuridhika na chochote,kila siku/saa utahitaji kitu kipya. Ukipumzika leo kesho mwili utataka kupumzika tena na kesho kutwa hivyo hivyo na siku inayofuata,hakuna mwisho....

Wengi tumeshapata hasara au pengine kushindwa kutimiza mambo fulani fulani katika maisha  kwasababu ya mwili. Tunashindwa au tulishindwa kwasababu ya kuusikiliza mwili na kuupa kila utakacho lakini bahati mbaya sana mwili unaendelea kuhitaji tu. Unatufurusha tu kila siku....

Wapendwa,kama nilivyosema huko juu,mwili nao una mahitaji yake lakini mwili huu huu hauridhiki,hakuna wakati utasema hapana,ukiupa kuku leo kesho utatamani Sato. Hautaishia hapo keshokutwa utataka dagaa wakavu,siku inayofuata utataka nyama ya kukaanga na mlolongo unakuwa mreefu sana,hakuna kukoma labda afya iwe na kasoro....

Mwili ni kama mtoto mdogo. Mtoto anapoamka anataka kitumbua hapo hapo atataka kwenda kucheza. Kuna wakati tunawazuia watoto kutenda mambo fulani kwasababu tunajuwa yanaweza kuwadhuru au hayana faida kwao. Miili yetu nayo ni hivyo hivyo,si kila utakachohitaji basi uhangaike kuupa....

Wakati wa kuamka asubuhi unaweza kufika lakini mwili unakataa huku unafahamu kabisa kuwa ni lazima uamke ili ukawajibike,ukiusikiliza mwili wako utaharibu kazi. Mwili unaweza kukuharibia malengo yako na zaidi maisha kwa ujumla wake....

Si kila unaomtamani mwanamke/mwanaume basi uupatie mwili unachokitaka. Haitatokea ukaridhika,ukiupa mwili utakacho leo kesho utataka tena kwa mwingine mwishowe utaharibu ndoa yako na familia kwa ujumla....

Si kila unapotamani bia basi unywe. Si kila unapotamani nguo basi ununue. Utaharibu bajeti za mambo mengine halafu mwili hautakoma kutaka vingine....

Tujifunze kuukatalia mwili na vurugu zake. Upatie mwili yale ya muhimu tu. Kama unahitaji kulala,lala kwa muda sahihi na baada ya hapo amka ukafanye kazi. Mwili utakutaka uendelee kulala tu,ukiusikiliza inakula kwako. Utaharibu kazi na matokeo yake utaishia kufukuzwa kwenye nyumba uliyopanga au utashindwa kuihudumia familia yako....

Uvivu ni matokeo ya kuusikiliza mwili. Karibia tabia zote hasi ni matokeo ya kusikiliza mwili kuliko pindukia. Tabia kama ulevi,umalaya,matumizi ya madawa ya kulevya n.k ni matokeo ya jambo hili....

Kuanzia leo sema hapana kwa mwili wako. Kataa kuwa mtumwa wa mwili wako leo na maisha yako yatabadilika kabisa....

Uwe na wakati mwema......

Chanzo:- nimetumiwa na rafiki nikaona sio vema kubaki na ujumbe mzuri wa burasa kama huu  peke yangu. Elimu ni kugawana.

Friday, January 25, 2019

HEBU LEO TUANGALIE BAADHI YA MANENO LA HEKIMA....!

1. Kila jambo na wakati wake
2. Aba na haba hujaza kibaba
3. Maji hayatoki yakishushwa kwa moto.
4. Siku njema huonekana asubuhi.
5. Dalili ya mvua ni mawingi
6. Dawa ya moto ni moto
7. Fimbo ya mbali haini nyoka
8. Asiyefunzwa na mamaye hafunzwa na ulimwengu
BASI  NIWATAKIENI IJUMAA NJEMA NA MWISHO MWEMA WA JUMA.

Thursday, January 24, 2019

KUMBUKUMBU .....ENZI HIZOOO! WATU TUMETOKA MBALI KWA KWELI

Aina za mafuta ya kupikia pa kupaka kwenye mkate nadhani PRIDE na SUPA-GHEE
Aina nyingine ni tan bond
Dada ana mzinga wa redio/ kaseti ili kupata pozi
Basi la Iringa enzi hizo

Tuesday, January 15, 2019

Thursday, January 10, 2019

VIFAA MBALIMBALI VYA KUTUNZIA MAJI/KWENDA KUCHOTA MAJI KISIMANI AU SEHEMU NYINGINE

 Hapa ni ndoo tena za aina tatu au nne hivi 
 Hapa ni VIBUYU
 MTUNGI
Hapa ni kabila la wamasai wao hubeba mgongoni na hutumia madumu/madungu .
Binafsi nimezoea tumia ndoo na mtungi na kubeba kichwani. Je wewe mwenzangu?

Wednesday, January 9, 2019

UJUMBE WA LEO : TUYAKUMBATIE MALENGO/MAWAZO MAPYA ILI KULETA UHALISIA ....

Ukikumbatia ulicho nacho utaona mafanikio yake. NAWATAKIENI SIKU HII YA JUMATANO IWE NJEMA SANA.  PAMOJA DAIMA. Ni mimi Kapulya wenu.

Saturday, January 5, 2019

LEO NI SIKU YANGU YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA

 Namshukuru  mwenyezi kwa kunipa afya njema mpaka leo nimeiona kumbukumbu  yangu ya kuzaliwa. Pia napenda kuwapa hongera kwa wote waliozaliwa mwezi  huu wa kwanza  na watakaozaliwa mwezi huu.
 Kwa vile nilikuwa mwema familia, ndugu na marafiki wamenipondeza kwa zawadi.HONGERA SANA KWA SIKU YA KUZALIWA MIMI.

Monday, December 31, 2018

UJUMBE WA MWISHO WA MWAKA 2018 KUTOKA KWANGU KUJA KWENU

UJUMBE :-
HATA SURA NZURI ITAZEEKA, NA MWILI MZURI UTACHOKA, ILA ROHO NZURI HUBAKI  KUWA NZURI MILELE NA MILELE.
NACHUKUA NAFASI HII KUWASHUKURUNI SANA KWA MWAKA HUU 2018 KWA USHIRIKIANO WENU. AHSANTE SANA SANA . NI MIMI KAPULYA WENU.

Wednesday, December 26, 2018

MWOKOZI YESU AMEZALIWA


NI MATEGEMEO YANGU KUWA SIKUKUU HII YA KUZALIWA MWOKOZI WETU IMEKUWA NJEMA KWA WENGI WETU. NAMI NACHUKUA NAFASI HII NA KUSEMA NAWATAKIENI  WOTE NOELI NJEMA

Monday, December 17, 2018

LEO NIMEKUMBUKA MITINDO YA ZAMANI JINSI WATU WALIVYOKUWA WAKIPEANA HISIA ZAO

Hapa itakuwa anaenda kisimani ndoo kaficha sehemu, hivi unafikiri kwa nini hawaangaliani?
Hapa yaonekana mdada anaenda kutafuta kuni

...na mtindo huu ni kiboko wote wanaonekana kuwa na aibu ...


....hii ni  baadhi ya mitindo ya hapo kale.  Au pia watu walikuwa wakiandika barua au kumtuma mtu. Siku hizi eti mtu anatuma sms ya kawaida au WhatsApp

Thursday, December 13, 2018

TAREHE HII HAPA LEO NI SIKUKU YA MTAKATIFU LUCIA...

Kwa hiyo mimi nimeona itapendeza zaidi kama nikiitumia mikono yangu kwa kutengeneza aina hii maalumu ya mikate(LUSSEKATTER)  ili kujumuika ndugu, marafiki pia majirani kwa kusherehea siku hii....


.....pia aina hii ya biskuti (pepparkaka) GINGERBREAD


Na hapa ni maagizo  jinsi inavyokuwa. Nakumbuka binti yetu aliwahi kuigiza duh! niliogopa sana maana hiyo mishumaa inawaka kwa ukweli ......ila walijiandaa na ndoo za maji...

Monday, December 10, 2018

HAPO KALE KARIAKOO YETU ILIVYOKUWA........

NAWATAKIENI WOTE JUMATATU NJEMA SANA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!

Wednesday, December 5, 2018

NIMEYATAMANI SANA HAYA MATUNDA...............


Hapa ni mbula au sisi wangoni twasema  mabuni ni matamu sana pia juisi yake ni tamu mno.
Na hapa ni masuku, sasa ndio msimu wake 

Tuesday, December 4, 2018

NI MWEZI MPYA TENA ...TUANZE NA MSEMO HUU KUUANZA MWEZI HUU WA KUMI NA MBILI!

Msemo/ujumbe wa leo:-
Njia bora ya kuacha kuwaza ni jinsi gani unafikiri ya kwamba unajifahamu/jijua ni kuzingatia kile unachokijua, unajua.
TUKUTANE TENA PANAPO MAJALIWA!

Wednesday, November 28, 2018

BADO TUPO SONGEA KWETU

Karika pilika za kununua ngua Songea mjini

Tuesday, November 27, 2018

NAIPENDA SONGEA YANGU PIA CHAI HASA BILA SUKARI!

Kikombe hiki nimekipenda sana  hasa kwa kunywea chai na zaidi haya maneno ya naipenda SONGEA

Thursday, November 22, 2018

USIACHE KWENDA KANISANI

 


Mshiriki wa Kanisa, ambaye hapo nyuma amekuwa akihudhuria ibada kila juma,
 aliacha kwenda Kanisani. 
Baada ya wiki kadhaa kupita, Mchungaji aliamua kumtembelea nyumbani kwake.
Ilikuwa jioni ya baridi. Mchungaji alimkuta ndugu yule nyumbani peke yake akiwa
amekaa mbele ya jiko akiota moto
dhidi ya baridi. Akiwa anajaribu kutambua sababu ya  Mchungaji kumtembelea,
alimkaribisha na kumpatia kiti ili 
waote moto pamoja na kusubiri kitakachoendelea.
Mchungaji aliketi, lakini hakusema chochote, alikuwa kimya. Katikati ya ukimya ule,
aliutazama ule moto na mkaa 
uliokuwa ukiwaka jikoni. 
Baada ya dakika kadhaa, Mchungaji akachukua kibanio cha mkaa,
kwa makini akachukua kaa moja lililokuwa 
linawaka zaidi na akaliweka chini peke yake na kisha akakaa tena kwenye kiti chake kimyakimya.

Mwenyeji alitizama chote kilichokuwa kikiendelea akijaribu kujifunza kimyakimya.
Kadri lile kaa lililowekwa pembeni 
lilivyokuwa likiishiwa muwako wake, taratibu majivu yakaanza kulishika na hatimaye likazimika kabisa. 
Likawa baridi likazima kabisa.

Hakuna hata neno lililozungumzwa tangu waliposalimiana.
Mchungaji aliutazama ule mkaa ulozimika 
na akaona kwamba huu ni wakati sasa wa kuondoka.
Alisimama taratibu akauokota ule mkaa ulozimika na
 kuurudisha katikati ya makaa mengine yaliyokuwa yakiwaka moto.
Papohapo likashika moto likaanza kuwaka 
kama makaa mengine.
Mchungaji akaanza kuondoka. Alipofika mlangoni,
mwenyeji akiwa anabubujikwa na machozi shavuni, 
akasema "Mchungaji,
 ahsante sana kwa kunitembelea na hasa kwa hubiri lako hili la mkaa. 
Nimelielewa somo na kuanzia juma lijalo, nitaanza tena kuja kanisani"
**MWISHO WA SIMULIZI*

Nini tunajifunza hapa? Katika siku hizi za mwisho,
mwovu atatumia kila mbinu kuwafanya wanadamu 
wasihudhurie makanisani kwa kuwapatia sababu mbalimbali.
Lakini ushauri wangu, usiache kwenda kwenye ibada
kwa kisingizio kisicho na mashiko.
Kuwa Kanisani na kujichanganya na waamini wenzako kuna faida kubwa na 
kunatia joto la kiroho. Ukijitenga na washiriki wenzako,
utazimika kiroho na hatimaye utakufa kabisa kiroho.

Usiache kwenda kanisani kisa eti kule hawakujali,
usiache kwenda kanisani kisa eti Mchungaji/Askofu anapenda 
sadaka sana, usiache kwenda kanisani kisa huna sadaka,
usiache kwenda kanisani kisa uko katika hisia, 
usiache kwenda kanisani kisa unahofia kurudia nguo uliyovaa juma lililopita,
 usiache kwenda kanisani kisa 
unahofia kuna mtu mmekwazana kule,
usiache kwenda kanisani kisa hujisikii, usiache kwenda kanisani kisa 
wamekuudhi.
Ukiacha kwenda kanisani utazimika kama lile kaa moja,
ni kanisani ndiko MUNGU huachilia baraka ya kutufanya 
tuwe moto mkali, tunapojitenga na kanisa,
baridi ya dunia hii itatupiga na hatimaye tutazimika kabisa. 
Tafadhali usiache kwenda kanisani na Mungu akujalie upate hamasa mpya.

_*Nimeikuta simulizi hii mahali:
Pengine yaweza kutusaidia tuhudhurie ibada ikibidi mpaka katikati ya wiki.*_

Monday, November 19, 2018

PALE UNAPOOTA NDOTO YA KUWA NA SEHEMU KAMA HII

umekaa hapa na kuangalia uumbaji wa Mungu 
Hapa ni sehemu ya kupumzikia/kula
Jiko la kuchomea piza

Sunday, November 18, 2018

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA JIONI HII YA JUMAPILI YA LEO IWE TULIVU NA YENYE AMANI

Nawatakieni jioni hii ya jumapili ya leo iwe tulivu, yenye furaha na amani ya kutosha. KILA LA KHERI!...Kapulya wenu.

Monday, November 12, 2018

HII NI KAZI YA MIKONO YA KAKANGU HUKO MBINGA...MTOTO UMLEAVYO NDIYO AKUAVYOO

 Ukijishughulisha hakika njaa hutaiona......
Tujifunze kujishughulisha na hapo tutaona mafanikio yake

Tuesday, November 6, 2018

MBOGA ZA ASILI ZINA MANUFAA/FAIDA NA UTAMU WAKE

UYOGA PORI
Ni chakula nikipendacho sana na ni hodari sana kuutafuta huko mstuni. Maana ukiwa huko mstuni inakuwa kama ni kupoteza mawazo na pia unapata mazoezi na kIkubwa zaidi unapata mboga tena ya bureee. 
Mlenda bamia na mboga majani ya maboga au  mlenda wa porini na karanga. Binafsi nitachagua bamia na mboga maboga au mlenda pori usiotiwa karanga.