Showing posts with label kujiamini. Show all posts
Showing posts with label kujiamini. Show all posts

Tuesday, February 11, 2014

MKE ANAPOMJALI NA KUMKUBALI MUME HUMUONGEZEA KUJIAMINI…

Mke anapomjali na kumkubali mume humuongezea kujiamini…
Mahusiano kati ya mume na mke nyumbani huweza kumfanya mume afanikiwe kwenye shughuli zake au aanguke. Kwa nini? Ni kwamba, mtu ambaye anakataliwa na mtu au watu wanaomhusu huwa anakosa kujiamini, huwa anafikia mahali ambapo hujichukia hata yeye mwenyewe.
Mke anapomkosoa mume, anapomlalamikia kila mara na kuwa na ghubu, bila kujali kama mume huyo amekosa au hapana, mume hufikia mahali huanza kujitilia mashaka kama kweli ana uwezo wa kufanya mambo, kama kweli ana thamani anayodhani kuwa anayo. Kujiuliza huku mara nyingi kuna maana ya mwanaume kuanza kupoteza kujiamini na hata kuanza kuwa na uhusiano mbaya na watu anaohusiana nao mahali pengine kama kazini. Unaweza kumgundua mtu ambaye ana mke mlalamikaji, mkosoaji na mwenye ghubu kwa kuangalia jinsi anavyojitathmini. Kama mke ni mkosoaji na mwenye ghubu kwa mumewe ni lazima mume atakosa kujiamini katika kufanya mambo yake mengi, ni lazima ataanza kuwa na uhusiano mmbaya na watu wengine kutokana na hukohuko kutojiamini kwake ambako kumesababishwa na ghubu na kukosoa kwengi kwa mkewe. Mwanaume ambaye ana mke mkosoaji na mwenye ghubu hutokea kutowapenda watu wengine na kukosoa wengine inatokea kuwa sehemu muhimu kwa maisha yake, anatokea kuwa na hasira za karibukaribu na ni vigumu sana kwa mtu wa aina hii kuelewana na watu.
Baadhi ya makampuni huko Marekani, kabla hayajampandisha mtumishi wake cheo, humchunguza mke wa mtumishi. Hawachunguzi kama ni mzuri wa sura au kama anajua mapenzi au kupika vizuri. Mara zote huchunguza kama mwanamke huwa anampa mumewe moyo, kama hamkosoi na kumlalamikia na kama hana ghubu. Wanapogundua kwamba mke wa mtumishi siyo mkosoaji
wala mwenye kulalamika-lalamika humpa cheo mtumshi kwa imani kwamba atakuwa ni mtu mwenye kujiamini. Lakini wanapogundua kwamba mke ni mwenye kukosoa, mwenye ghubu na
mlalamikaji, kamwe hawampi mtumishi cheo, kwa sababu wanaamini kwamba, mtumishi huyo hawezi kuwa makini, atakuwa hajiamini.
.......................................................................................................................................................
Swali langu hapa je hii ni pale tu mwanamke anapomjali mume na ndio iwe hivi? Je? mwanamke astahili kujaliwa na kukubaliwa ili kuongeza kujiamini?..au ndo kusema mwanamke anajiamini sana kuliko mwanamume?..swali kutoka kwa KAPULYA...
Habari/mada hii nimetumiwa na mkereketwa/msomaji wa Maisha na Mafanikio kwa kutaka tu mimi nisome lakini mimi nimeona ina mafundisho ndani yake nikaona ni bora niiweke hapa ili wengine wafaidike na ELIMU hii.

Thursday, October 11, 2012

TUNATHAMINI MCHANGO WA MWANAMKE??

Mama mjasiriamali tayari hapa kumekucha na kuwajibika ndiyo kama kawaida...na kama kawaida mara nyingi watoto wa kike hujifunza karibu kila kitu kupitia mama. Basi hapa tunaona binti huyu hayupo nyuma naye yupo mbele katika kujifunza maisha...hapa unadhani wanatoka kuuza au wanakwenda? 

Tuesday, May 31, 2011

PAMOJA NA UBABE KUMBE HAWAJIAMINI!

Kwa utafiti wangu nilioufanya wanaume wengi hawajiamini katika nyanja za mapenzi na ni wakwepaji wakubwa wa kuwajibika fuatana nami ujue.
Ni wanaume wachache wanaoweza kuoa msichana aliyekwishazaa. Lakini pia ni wanaume haohao wanaowapa wachumba wao masharti ya kwamba mpaka ubebe mimba ndio nikuoe. Na wavulana pia hata kama yeye ni muhuni kupindukia atataka msichana atayemuoa asiwe na sifa ya kuchapa umalaya na hata akioa utasikia "usipoheshimu familia yangu tutakosana". Pamoja na mlolongo huo wote. Lakini kwa wanawake ni tofauti, wanawake wanajiamini sana katika mapenzi ndio maana pamoja na kuchagua wanaume watakaowaoa wao hujali zaidi, watathiminiwa kiasi gani? Mume awe ni mwizi, jambazi, mbeba zege au mfanya shughuli yoyote unayoiona ya hovyo. ATAMPENDA na KUMTHAMINI. JIFUNZE KUJIAMINI.

Tuesday, September 30, 2008

KAZI+USAFIRI NA KUJITEGEMEA

Bila kuvuka hapa basi hafiki nyumbani ,ila ningekuwa mimi sijui kwani nahisi kuna mamba hapa.
Kusafirisha cementi kwa mkokoteni. Umoja ni nguvu unyonge ni uzaifu. Kwani angalia wanavyoshiriana hivi ndivyo inavyotakiwa watu wote wawe.


Hapa ni mto Ruhuhu, Kufika ktika kijiji cha Lituhi ni lazima wavuke hapa na hapo wanasafirisha cementi mifuko 216. Watu wana imani sana.


Hakuna kulala kazi na mtu, hapa wanachonga mtumbwa kwa kutumia mti wa mwembe. Kwa hiyo mti wa mwembe sio kupata embe tu hapana mitumbwi pia.