Nimeamka leo nikiwaza hili neno KIONGOZI/VIONGOZI nikashindwa kuliwazua nikaamua kuchukua KAMUSI SANIFU YA KISWAHILI CHETU. Nayo ikaniambia hivi:-KIONGOZI/VIONGOZI.....
1. mtangulizi wa jambo fulani au wa kikundi cha watu, mkubwa anayesimamaia shughuli maalumu kwa kueleza au kuelekeza. AU...
2. Kitu kinachosaidia kuonyesha au kuelekeza......
Je? hawa viongozi wanaongoza kweli au wanajiongoza? Naomba tutafakari au jadili kwa pamoja.
Ndimi Kapulya wenu:-)
3 comments:
Kiongozi bora au bora Kiongozi.hapa kuna maana mbili. Kiongozi bora ni yule anaefanikisha kwa kiwango kikubwa matarajio ya wale anaowaongoza. Bora kiongozi ni yupo yupo tuu lakini hakuna matumaini yoyote kwa wale anaowaongoza,unaweza ukasema nchi inajiendesha kwa remote control aka kwa rehema za Mwenyezi Mungu. By Salumu.
Yeah upo right kwa tafsiri ya kiongozi, lakini pia kiongozi ni mtu anaeangalia kama wale anaowaongoza wanaridhika, akubali kupokea maoni yao na kuyafanyia kazi.
Kiongozi ni mtu aliyekabidhiwa jukumu la kuongoza au kusimamia kikundi cha watu katika kufikia malengo kilichojiwekea kikundi. Kiongozi anaweza kuwa bora au vinginevyo kulingana na anavyosimamia na kukidhi malengo tarajiwa. Kuna haja ya kuonya kidogo. Kuna tofauti kati ya kiongozi na mtawala. Mtawala hutawala lakini haongozi. Na kiongozi huongoza ila hatawali. Kwa ufupi kiongozi ni mtu anayekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza, kuhami,kufanikisha na hata kupanga namna ya kufikia malengo yaliyolengwa na kundi analoongoza au kusimami.
Post a Comment