Hivi ni vile viazi angalia hapa na jana jioni ndiyo ikafikia muda wa kuangalia kama vyaweza kuliwa na matokeo yako yakawa kweli vyaweza kwa hiyo jana jioni tumekula viazi vya kulima Nangonyani.......kama
....uonavyo kwenye sahani hapa ni viazi , broccoli, nyanya kidogo, limao na samaki aina ya salmon(kiswahili ) nisaidieni ......kilikuwa kitamu mno....nawashauri wote mlio na nafasi ya kulima bustani kulima viazi mviringo....NAWATAKIENI ALHAMIS NJEMA NA MWANZO MWEMA WA MWEZI AGOSTI:-)
5 comments:
Da Yasinta! yaani mwezi umoja tuu toka ulime hizo viazi na ndio imezaa kwa wingi. kweli weye mtoto ya mkulima. By Salumu.
Mkulima na jembe lake na mazao yake na mlo wake.
Duuhh Hongera sana sana KADALA wa mimi..
yani mlo unaonekana ulikuwa mtamu hatari.... mimi mginjwa sana wa mbogamboga, hapa nishatokwa na udenda hatari. nachungliaga bustani ya dada Yasinta...nikiangalia majani ya maboga nawaza mlenda (bamia, majani ya maboga yamechanganywa pamoja yakawekwa magadi, kijaniiiiiiiii..tupia na nyanya chungu kidogo...then upate kitu kama nyama au huyo samaki wako da Yasinta, na ugali...acha kabisa...hongera.
Mlo ulikuwa kabambe sana, hongera kwa kula viazi ulivyolima mwenyewe. Nimekula kwa macho dada. Siku nyingine nishtue mapema ili nishiriki mlo pamoja nawe.
Post a Comment