Wednesday, August 7, 2013

WAKATI WA KUVUNA UMEFIKA SASA YAANI MPAKA RAHA NI KUTOKA TU NJE NA KUCHUMA/KUCHUKUA NA KULA:-)

Mnaona raha ya kulima nyanya zimeanza kuiva kwa hiyo hakuna kununua nyanya kwa muda sasa. Halafu ni tamu sana..Si mnaona zilivyofungamana kwa hiyo nawakaribisha tujumuike ...
Hapa ni njegere nazo zimezaa kweli ..
Maboga nayo hayoooo  :-)
 
Vitunguu navyo havipo nyuma, kwa hiyo hakuna kununui vitunguu kwa muda. Mliopo jirani karibuni na wote wengine. Nipo kwenye mkakati wa kupanda ile vigiri nitawaonyesha hivi karibuni ni vipi kuwadhibiti wale viwavi...Nitajaribu

10 comments:

Unknown said...

Dah cjui ntafanyaje, natamania kweli. Hongera Da yasinta.

Unknown said...

Dah cjui ntafanyaje, natamania kweli. Hongera Da yasinta.

Rachel Siwa said...

Shambani Shambani. Mazao bora shambaaaaani. ..Hongera sana kadala wa mimi.

Anonymous said...

Hongera da Yasinta. Tunakuombea mafanikio zaidi.Natumaini tutakula na mapapai pia. By Salumu

Yasinta Ngonyani said...

Nancy! Njoo ndugu yangu...karibu sana
Kachiki...ahsante Alo kawimbo katamu ako
Salumu ! Ahsante kakangu...hahahaaaaa umenichekesha kuhusu mapapai labda nanasi

ray njau said...

Honera sana Yasinta kwa kuthibisha kuwa wewe ni mkulima bora sana.Karibu sana kwenye sikukuu ya wakulima ya nane hapa Tanzania.

Anonymous said...

Hongera sana Yasinta. Duh nadhani sasa itabidi nije kwa kweli hali ni ngumu kuvumilia hayo mazao ya shambani kwako. Tutajumuika wote karibuni ila naukiulizia vipi vile viazi mviringo vipo au vimeisha? Siku njema.

Anonymous said...

Da Yasinta yani bustani imependeza sana sana! hongera kwa kilimo kwanza mana unakipa kipaumbelea kilimo hadi raha, ukizingatia kuwa unaishi ulaya.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! Ahsante kwa kunitia moyo.

Usiye na jina wa 4.44 pm karibu sana sana. Viazii mviringo bado vipo ila wahi.

Na usiye na jina wa 4.46pm ahsante nazidi kupata moyo

Bennet said...

Dada Yasinta hongera sana ila kama ungepunguzia matawi nyanya zako zingekuwa kubwa zaidi, mbolea yako imeliwa na matawi usiyoyahitaji next time you will do your best