Tuesday, February 22, 2011

SIKU AMBAYO SITAISAHAU

Restieli akiwa amejipumzisha nyumbani
kwao Njoro baada ya kutoka shuleni
Leo hii nimepokea waraka huu kutoka kwa binti Restieli Moses Mbwambo aishiye kule Moshi Kilimanjaro, waraka ambao umetumwa kwa msaada wa mdau wa BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO aliyeko kule MOSHI. Na mie bila kuongeza wala kupunguza neno nauweka kama ifuatavyo:

Ni siku ambayo niliungua na mafuta wakati nilipokuwa mdogo wa umri wa mwaka mmoja na nusu. Ukweli ni kwamba nilisimuliwa na wazazi wangu jinsi tukio hilo lilivyotokea kwa kuwa mri wangu ulikuwa ni mdogo. Walinisimulia kuwa tukio hilo lilitokea hapo mnamo tarehe 17 Julai 2002, siku ya Jumatano jioni.
Siku hiyo mama yangu alikwenda kurekodi nyimbo zao za kwaya huko Arusha na baba alikwenda kanisani kuhudhuria ibada ya jioni katika kanisa lao la Njoro SDA lililopo hapa mjini Moshi, hivyo akaniacha na jirani ili aniangalie.
Wakati baba ananiacha na jirani yao, alikuwa ndio kwanza anajiandaa kuchoma maandazi yake kwa kuwa alikuwa ni mfanyabiashara wa maandazi pale mtaani.
Kutokana na sijui udogo au utundu naambiwa kuwa nilikwenda kwenye kikango cha mafuta na kukishika ambapo kilipinduka na yale mafuta ambayo yalishakuwa yamepata moto yalinimwagikia mwili mzima na kunisababishia majeraha na maumivu makali.
Baba alijulishwa na aliporudi nyumbani akakuta nimeshapelekwa hospitali ya Mawenzi na baadae nikahamishiwa Hospitali ya KCMC kwa ajili ya matibabu.
Mama alirudi majira ya saa kumi na mbili jioni na kujulishwa juu ajali iliyonipata, akaja haraka hospitalini.
Kwa kweli niliungua sana kwa kuwa mafuta yalikuwa ni ya moto sana. Watu walitoka kanisani walipokuwa wakimuimbia mungu na kuja Hosptalini kuniona.
Siku ya Jumamosi ambayo ni siku a sabato ilitangazwa pale kanisani juu ya ajali iliyonipata hivyo waumini wote walipotoka kanisani walikuja moja kwa moja kuniona na walikuwa wengi sana.
Nikiwa ndio nimetimiza miaka kumi mwaka huu, nimelikumbuka sana tukio hili na ndio maana nikaamua kukaa chini na kuandika kumbukumbu hii na kumpa mama na baba yangu kama kumbukumbu ya tukio hilo la kusikitisha.
Namshukuru mungu sana kwa kunilinda mpaka sasa nimetimiza miaka kumi, jina la Bwana lipewe sifa.
Pia nawashukuru wazazi wangu, majirani na washirika wa kanisa la Njoro SDA kwa kuwa karibu na wazazi wangu katika kipindi chote cha madhila yangu.
Natoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini wanapokuwa au wanapoachiwa watoto wadogo kuwaangalia, kwa kuwa watoto hawajui vitu vya hatari, kama moto, visima, magari na kadhalika.
Tarehe 17 Julai 2002 ni siku ambayo sitaisahau
Ni mimi Restieli Moses Mbwambo wa Njoro Moshi.

17 comments:

Mija Shija Sayi said...

Aisee, Mungu ni mwema.

Je alipona kabisa na sasa hana kilema chochote?

Unknown said...

inasikitisha sana ila jambo la kushukuru amepona na kutukumbusha engine kujali watoto mahali penye hatari.

Simon Kitururu said...

Pole sana Restieli!

Na ni matumaini kwa kuliandika tukio hili unazidi kupona pia hata kisaikolojia hasa kwa kuwa matukio kama haya hayaumizi mtu kwa nje tu bali humuumiza mtu hata kisaikolojia.


Na pia kwa mdada wa miaka kumi kwa mtazamo wangu unajua sana kujieleza na kuandika vizuri!

Na labda hicho ni moja ya kipaji chako kwa hiyo usiache kuandika na kusimulia vitu kwa kuwa nahisi dunia hii inahitaji kukusikia.

Kwa mara nyingine ``POLE SANA!´´

Yasinta Ngonyani said...

Mija! Kwa maeleo niliyoyapata ni kwamba ana kovo usoni hata ukimwangalia sana utaona linaonekana, pia kifuani.

S&k! ni kweli inasikitisha sana na tuzidi kumshukuru Mungu kwa uweza wake. pia kumshuru binti Restieli kwa kutukumbusha swala la kuwajali watoto sehemu za hatari wakiwa bila maangalizi.

Simon! Nami pia naamini binti Restieli maendeleo yake ni mazuri na hakika sijawahi kuona binti kama yeye anaweza kuwa na kumbukumbu kwa kusimuliwa na kisha kuandika vizuri hivi. Hapo ndipo nilipokuja amini ni kweli hatakuja kusahau milele. POLE SANA najua unaendelea shuleni vizuri sana.

Rachel Siwa said...

Pole sana da Restieli!Mungu awenawe kwa kila jambo,pia Hongera kwa kutimiz miaka 10 na kuwa mtu wa shukrani,Ubarikiwe sana.

Chambi Chachage said...

Salaam. Imenigusa hii. Naiposti kwenye http://ufunuo.blogspot.com/ wana-SDA wenzake wengine waisome pia. Amen

Koero Mkundi said...

Chambi hata mie ni Msabato na nilitamani sana kiweka pale kwenye Blog yangu ya VUKANI, lakini kwa kuwa umeshanitangulia basi ngoja nikuachie maana najua kule hata waumini wa kanisa lam SDA Njoro wataisoma habari hii.

Kwa sasa niko jijini Arusha, kwa kweli nilitamani sana niende Moshi kuonana na Binti huyu mwenye upendo na shukrani, lakini kwa bahati mbaya muda umenitupa mkono.

nakutakia maisha marefu binti na ukue kwa umri na kimo ili uje kumpendeza Mungu.

emu-three said...

Pole sana kwa kisanaga hicho, kwani wanasema `ajali haina kinga' na yote ni mitihani ya maisha.

John Mwaipopo said...

hakika kisa kinasikitisha na ashukuriwe MUNGU kwa kumnusuru binti huyu.

Ila kwa nia ya kuweka kumbukumbu vizuri nanukuu "Ukweli ni kwamba nilisimuliwa na wazazi wangu jinsi tukio hilo lilivyotokea kwa kuwa mri wangu ulikuwa ni mdogo"

Nukuu yangu inashwawishi kuwa siku AMBAYO ANAIKUMBUKA NI ILE ALIYOSIMULIWA, na siyo ALIYOUNGUA, au?

pia kwa binti wa miaka 10, nadhani kasaidiwa kuandika, la sivyo we have a genius in making.

Kwa wamama na wababa hii stori inatukumbusha kwa mara nyingine KUWAWEKA WATOTO WA UMRI HUU MBALI NA MOTO WA AINA YOYOTE IWAYO. kuna rafiki yungu huwa hatumii maneno MTOTO KAUNGUA anatumia MTOTO KAUNGUZWA NA MAMA (BABA)YAKE

Goodman Manyanya Phiri said...

Restieli, you do rock, Baby! Keep it up with your forward-looking attitude. Mungu akujalie, Mwanangu!

Nimekufurahia kwa sababu umenitahadharisha nami niwe mwangalifu jinsi ninavyomlea Tamara Phiri ambae leo anamiezi 4 na siku 13 tu. Ni mtundu kama nini!!!

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii kwa kuwashukuruni wote kwa mchango wenu. Nakubaliana ni makala ambayo imewagusa wengi sana maana malezi ya watoto kwa kweli si mchezo kwa hiyo kama mzazi napenda kuwapa ushairi wazazi wanzangu usimwache mtoto/watoto peke yao hata kama ni sekunde watoto ni viumbe ambao wanapenda sana kujaribu jaribu kuona nini kitatakea. Kwa mara nyingine tena nakupa hongera sana kwa kuweza kugawa habari hii nasi. Mwenyezi Mungu na awe nawe Daima.Upendo Daima.

kwanjara said...

Pole sana Restieli. Tumshukuru Mungu kwa uponyaji na faraja. Mungu akubariki sana. Nimeguswa sana na ushuhuda wako. Kama mzazi mwenye binti wa umri wa mwaka mmoja, umenipatia kitu cha kufikiria na kutafakari.

Goodman Manyanya Phiri said...

Haya, basi, Binti Restieli Mbwambo! Juzi-juzi siku kama ile uliepatwa na mkasa wa fundisho kwetu sote, nami nimeongeza POST moja katika blogu yangu "Lengibatsandzako".

Nitembelee basi, Binti, uone nimeandika nini... kwa Kimombo lakini, samahani!

Bonyeza hapa http://ninaewapenda.blogspot.com/2011/07/tanzanian-young-heroine-fights-back-for.html

cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing obat cytotec

Unknown said...

Nam

Anonymous said...

What do you mean nam

Anonymous said...

God be the glory pole