Wednesday, September 28, 2011

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA YANGU SHABAN KALUSE!!!

Shaban Kaluse atimiza miaka 40 leo!



Napenda kuchukua nafasi na KUMPONGEZA KAKA YANGU WA HIARI SHABAN KALUSE kwa siku yake ya kuzaliwa. Shaban Kaluse ni kaka mmoja ambaye ni mshauri mzuri sana , msikilizaji, sio mbinafsi. nk. Nikuambieni kitu kimoja? Ni hivi mimi au pia watu wengine wanafikiri kaka, dada au ndugu ni yule uliyezaliwa naye tumbo moja yaani mama mmoja na baba mmoja. LA HASHA. Kaka huyu amekuwa KAKA kweli na amekuwa mwema sana katika familia ya akina NGONYANI. HONGERA SANA KWA KUTIMIZA MIAKA 40 NI MIAKA MINGI MWENYEZI MUNGU AKULINDE NA AKUJALIE AFYA NJEMA!!!

5 comments:

Koero Mkundi said...

Hongera kaka Shaban Kaluse kwa kutimiza miaka..........
Miaka 40! sio mchezo kaka....
Mungu aki=upe maisha marefu na afya njema wewe na familia yako.

Nimeadimika kidogo niko huku TANGA, kwa dada yangu, nitarudi wiki ijayo kuendeleza libeneke hapo VUKANI.

ray njau said...

"URAFIKI WAZIDI UNDUGU;UNDUGU NI KUFAANA NA SIYO KUFANANA NA AKUFAAYE WAKATI WA DHIKI NDIYE RAFIKI WA KWELI".
-----------------------------------
"Kuendako hisani hakurudi nuksani bali shukrani."
-----------------------------------
1 Wakorintho 13:1-7

1 Nikisema kwa lugha za wanadamu na za malaika lakini sina upendo, nimekuwa chombo cha shaba nyeupe kinachovuma au toazi linalolia. 2 Na ikiwa nina zawadi ya kutoa unabii nami nazijua siri takatifu zote na ujuzi wote, na ikiwa nina imani yote kuweza kuhamisha milima, lakini sina upendo, mimi si kitu. 3 Nami nikitoa mali zangu zote ili kuwalisha wengine, nami nikiutoa mwili wangu, ili nijisifu, lakini sina upendo, sipati faida hata kidogo.

4 Upendo ni wenye ustahimilivu na wenye fadhili. Upendo hauna wivu, haujigambi, haujivuni, 5 haujiendeshi bila adabu, hautafuti faida zake wenyewe, hauchokozeki. Hauweki hesabu ya ubaya. 6 Haushangilii juu ya ukosefu wa uadilifu, bali hushangilia pamoja na kweli. 7 Huhimili mambo yote, huamini mambo yote, hutumaini mambo yote, huvumilia mambo yote.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

uuuuuuuuuuuuuuwwwwwwwwwwwwwwwiiiiiiiiiiiiiii bahati nzuri najua kuwa huyu bwana haogopi kifo

Simon Kitururu said...

Nimechelewa kidogo,...
HAPPY BIRTHDAY ambiere!

MARKUS MPANGALA said...

ni ukubwa kweli,
miaka iliyojaa heri,
naamini mola yu pamoja nawe na familia yako pia.