Tuesday, September 6, 2011

KAZI NI KAZI TU !!!

Au jamani?

14 comments:

sam mbogo said...

Unasema kweli,Yasinta kazi nikazi bora mkono uende kinywani.pia kwa wenzetu huku ulaya msukuma mkokoteni,ana sabau kwanini anafanya hivyo,mfano,kama kazi yake ni kufagia barabara au kuzoa taka,hapo mkokoteni/tolori nisahihi kutmika. najaribu kuangalia,kazi hizihizi zinazo fanywa na watu wa ulaya/uk ,kama,kufagia,kuzoatakataka,kuleawazee,kubeba maboksi,kufanya kazi baa/pub,nk kwa uangalifu huohuo walionao wenzetu huku ulaya,nafikiri hata nyumbani Tanzania ingesaidia kidogo,kama siyo sana.tatizo tanzania tuna puuzia sana ,kufuata taratibu,hakiza watu kikazi,usalama wao wawapo kazini,na kuwa na utaratibu wa kueleweka ambao ni wazi katika kazi na ufanyaji wake.leo hii mwanafuzi akiwa likizo hana mahali pakufanya kazi kupiga( tempo),mfano kuna migahawa mingi tu bongo,vituo vingi tu vya mafuta,pub,hoteli,mahospitali ,nk hakuna haja ya kutoa ajira ya kudumu katika sehemu hizi nilizo taja,ajiri wakudumu wachache,wengine ,wakupita ,ila kwa kufuaata utaratibu wa kisheria,nahili ndo tatizo kubwa,haki ya mfanyakazi,haizingatiwi. kaka S

chib said...

Mradi iwe halali na inampatia mtu kipato!

Rachel Siwa said...

Na asiyefanya kazi na asile!!!!

John Fisher said...

Hakuna kitu chenye utamu kama kuwa na kazi. Utamu wa kazi yenyewe huwa ni ile ajira unayoipata kutokana na kazi yenyewe.
Hata Mola hufanya kazi nyingi juu ya maisha yetu sisi wanadamu.

Kweli mtu asipofanya kazi na asile.

John Fisher Kanene

John Fisher said...

Kazi ni kazi. Na kazi zote halali zina utamu wake maana bila kazi sijui ulimwengu ungekuwa wa aina gani. Hakuna kitu kizuri kuamuka kila asubuhi na kutarajia ile kazi uliyopanga kuifanya kwa siku hiyo.
Naa mwishowe je????? Utamu wake ni kupata mshahara au ajira yako...

KAZI TUFANYE TUACHE UZEMBE

John Fisher Kanene

Goodman Manyanya Phiri said...

Kweli kabisa, kazi vilevile ni tiba isiemtaka daktari. Mimi nawe wavivu tutakwenda kumuona daktari ili tupate vidonge vya usingizi pia vya hamu ya chakula na kuwashibisha wanandoa wenzetu.


... HUYO BWANA HATA KAMWE APATE MATATIZO YA AINA HIYO!

Unabisha?

Basi, mualike nyumbani kwako wiki nzima ili ugundue!

Anonymous said...

2 Wathesalonike 3:1-18

1 Mwishowe, akina ndugu, endeleeni kusali kwa ajili yetu, ili neno la Yehova liendelee kusonga haraka na kutukuzwa kama vile linavyofanya kwenu; 2 na ili tukombolewe kutoka kwa watu wenye madhara na waovu, kwa maana imani si mali ya watu wote. 3 Lakini Bwana ni mwaminifu, naye atawafanya ninyi kuwa imara na kuwaepusha na yule mwovu. 4 Zaidi ya hayo, tuna uhakika katika Bwana kuwahusu ninyi, kwamba mnafanya nanyi mtaendelea kufanya mambo tunayoagiza. 5 Bwana na aendelee kuielekeza mioyo yenu kwa mafanikio katika kumpenda Mungu na katika uvumilivu kwa ajili ya Kristo.

6 Sasa tunawapa ninyi maagizo, akina ndugu, katika jina la Bwana Yesu Kristo, mjiepushe na kila ndugu anayetembea bila utaratibu na si kulingana na pokeo mlilopokea kutoka kwetu. 7 Kwa maana ninyi wenyewe mnajua njia mnayopaswa kutuiga, kwa sababu hatukujiendesha bila utaratibu katikati yenu 8 wala hatukula chakula kwa yeyote bure. Kinyume cha hilo, kwa kazi ya jasho na kutaabika usiku na mchana tulikuwa tukifanya kazi ili tusimtwike yeyote kati yenu mzigo wenye gharama. 9 Si kwamba hatuna mamlaka, bali ili tujitoe kuwa kielelezo kwenu ili mtuige sisi. 10 Kwa kweli, pia, tulipokuwa pamoja nanyi, tulikuwa tukiwapa ninyi agizo hili: “Ikiwa yeyote hataki kufanya kazi, basi na asile chakula.” 11 Kwa maana tunasikia watu fulani wanatembea bila utaratibu katikati yenu, hawafanyi kazi hata kidogo bali wanajiingiza katika mambo yasiyowahusu wao. 12 Kwa watu wa namna hiyo tunawapa agizo na kuwahimiza katika Bwana Yesu Kristo kwamba kwa kufanya kazi kwa utulivu wale chakula ambacho wao wenyewe wanafanyia kazi.

13 Kwa upande wenu, akina ndugu, msiache kutenda yaliyo sawa. 14 Lakini ikiwa yeyote hatii neno letu kupitia barua hii, mtieni alama mtu huyo, acheni kushirikiana naye, ili aone aibu. 15 Na bado msimwone yeye kuwa adui, bali endeleeni kumwonya kama ndugu.

16 Sasa Bwana wa amani mwenyewe na awape ninyi amani daima katika kila njia. Bwana na awe pamoja nanyi nyote.

17 Hii ni salamu yangu, ya Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe, ambayo ni ishara katika kila barua; hivi ndivyo mimi huandika.

18 Fadhili zisizostahiliwa za Bwana wetu Yesu Kristo na ziwe pamoja nanyi nyote.
-----------------------
R.Njau

Simon Kitururu said...

Kazi sio KAZI tu!

Kwa kuwa kuna kazi nyingine hazifanyiki aisee!


Si kazi nyingine ni DHAMBI?:-(

Yasinta Ngonyani said...

Simon! kai gani ambazo ni dhambi?

Rachel Siwa said...

Ubarikiwe R.Njau!!!@kaka wa mimi Simon wa Kitururu kwikwiwki!!! nami nipo pembeni kwa da' Yasinta kupata elimu ya kazi zenye dhambi.

Simon Kitururu said...

@Da Yasinta na DA Rachel: DHAMBI ni kitu cha ajabu kwa kuwa inategemea na funzo la `` NINI ni DHAMBI´´.

Kwa waliofunzwa ``USIHUKUMU na ni MUNGU PEKEE ahukumuye !´´ hata kuwa HAKIMU kikazi hapa duniani wa nani kadokoa mboga na aadhibiwe vipikuna wadaio ni DHAMBI .

...na tukienda mpaka kwenye kazi wafanyazo MALAYA katika kujenga TAIFA la waliotulia baada ya kushughulikiwa na MALAYA kwa kuwa labda hata majumbani kwao hawalishwi wakashiba chakula cha usiku,...
.... unaweza ukastukia ni jinsi gani labda kazi nyingine ni DHAMBI!:-(

Yasinta Ngonyani said...

Simon nimekuelewa kakangu...lakini Je sasa hapo mwenye dhambi ni yupi?

Simon Kitururu said...

@Yasinta: Naogopa kuingia dhambi ya kuhukumu!:-(

Rachel Siwa said...

kakake Simon wa Kitururu nami pioa nimekumanya!!!!!!!hahahaaha unaogopa dhambi ya kuhukumu.