Monday, November 21, 2016


Leo nimetumiwa huu ujumbe na RAFIKI nami nikaona ni ujumbe mzuri nisiwe mchoyo nikaona niuweka hapa kibarazani kwetu...ukipata wasaa basi soma...

Bwana mmoja maskini sana aliishi na mkewe. Mkewe alikuwa na nywele ndefu za kuvutia. Siku moja mkewe akamwambia bwana huyu akamnununulie chanuo la nywele zake ili azichane zirefuke na kunawili vizuri. Bwana huyu alijibu hana pesa kabisa hata ya kutengenezea saa yake iliyokuwa imevunjika. Mwanamke huyu hakuendelea tena kusisitiza ombi lake. Kesho ilipofika bwana yule akiwa anarejea nyumbani alipitia dukani akaiuza ile saa yake na kununua chanuo kwa ajili ya mke wake. Alipofika nyumbani akiwa na lengo la kumshangaza mkewe  akastaajabu kumkuta mkewe kanyoa. Mke naye kumbe alizinyoa nywele zake na kuziuza kisha akamnunulia mumewe saa mpya. Wote walikuwa na furaha  ya kupendana na kujitoa kwa mwenzie wakajikuta wanalia kwa furaha.
UJUMBE:- KUMBUKA KUPENDA SIO KITU  ILA KITU NI KUPENDA . ILA KUPENDANA NI ZAIDI YA KITU. MPENDE AKUPENDAYE!

2 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nakubaliana na hoja kuwa hapa kuna upendo ingawa naweza kuongeza kuwa hapa ninachoona cha mno ni ueleewa, kujitoa, kuaminiana na kuthaminiana. Maana bi mkubwa angekuwa si mwelewa angedhani mumewe hamjali ukiachia mbali kuona kama haelewi thamani ya kitana. Vinginevyo angekuwa mchumiatumbo angeshamwita mumewe mume suruali. Ndoa inahitaji subira na kusomana tabia,kuelewan, kuvumiliana na yote katika yote kupendana na kuvaliana viatu yaani kujiweka kwenye viatu vya mwenzio wakati wa matatizo ili utoa hukumu au uamuzi mzuri.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango! ulichosema ni kweli maana kila mtu hakuona uthamani wa alichoanacho na hilo ndio PENDO LA DHATI LA KUALIANA NA KUTHIMIANA.. NDOA SIO LELEMAMA.