Saturday, October 16, 2010

Chagua CCM chagua mahitaji haya............................

TUKO HIVYO, Hatuoni,Hatusikii.
Tunadanganyika kirahisi Tunafuata mkumbo BAADAE TUNALALAMIKA Chagua CCM



OFISI ZETU

MAKAZI YETU

SHULE ZETU


DARASANI WATOTO WETU



HUKO VIJIJINI-DISPENSARY

WAO WAKICHAGULIWA........................

Ubalozi wa Tanzania Wasington

Ofisi zetuBunge
Kuna cha kuongeza?

Sasa tucheze na hesabu 6,900,000/= kwa mbunge mmoja,zidisha mara miezi 12 then zidisha kwa miaka 5 = 414,000,000/= jumlisha 50,000,000/= anayopewa mara baada ya kumaliza miaka 5 = 464,000,000/= kwa mbunge mmoja.

464,000,000/= siko tayari kuzidisha fedha hii mara wabunge wote kwa miaka 5,calculator yangu itachanganyikiwa alafu niingie gharama ya kununua nyingine.

9 comments:

Michael said...

Kwa wapiga kura wengi sasa mnaonekana mna dhamani na wanasiasa, cha msingi ni kila mtanzania mwenye mapenzi mena na hili taifa kuwa makini na hawa wanasiasa wabinafsi na wanopenda kula kwa migongo ya maskini wa watanzania

Taifa lina karibia kuwa na mika 50 lakini kuna maeneo mengine
1)- Hakuna maji safi ya kunjwa
2)-Hakuna huduma za awali za afya
3)-Hakuna barabara na miondombinu mingine
4- Elimu ndio kila kukicha inazidi kuwa duni

nchi ina rasilimali nyingi kushinda hata mataifa makubwa yaliyoendelea, tulichokosa ni viongozi wazalendo, wenye malengo, ubunifu na kujituma

Ni aibu kwa mkuu wa nchi kusimama na kuwatetea wahujumu maendeleo ya taifa hili( MRAMBA;CHENGE;ROSTAM;KARAMAGI)watu wameiba/wamezembea badala ya kuwajibishwa wanatetewa,,,ni vema wananchi tukachukua hatua madhubuti kuhakikisha tunachagua viongozi watakao lipeleka hili taifa letu kwnye nji ya Ahadi

ni vema kila mtanzania kwa uwezo alionao akahamasisha jamii ili tuamke

MARKUS MPANGALA said...

YANAUMA SANA lakini naomba niende NJE YA MADA HII

nimevutiwa na hicho kitanda cha TEREMKA..................
Maana enzi za ambazo Mama Mchungaji Koero anaita Ubaruubaru; niliwahi kuingia faragha kwa mchumba a.k.a limupenzi la muda mfupi NIKAKUTANA na hilo likitanda mweeeeeeeeeeeeeeeeeeee SITANIII mcharukooooo haki ya nani,,,,, lakini yale mambo mweeeee poaaaa tu hakuna kujali KITANDA cha teremka niku......... ha ha ha ha ha

Anonymous said...

Sina la kusema lakini ukitazama ikiwa CCM au chama chochote kile kingine kitashika hakitafanya zaidi ya hivi ni maofisi, shule na mahospitali yatabaki kama yalivyo, hamna tofauti sisi watanzania au hata waafrika wote ni sawa kila mmoja anafikiria maslahi yake.

Anonymous said...

Maisha yalivyo,yanashabihiana na namna ambavyo huamua kuwachagua viongozi waTAKAVITU ndani ya mioyo yao badala ya kuwachagua viongozi waTAKATIFU mioyoni mwao,hughilibika kwa khanga,tihseti na kofia bila kujali aina ya maisha yao yalivyo,wakija huwashangilia kwa tija ya bakuli la komoni,wanasahau shida na matatizo lukuki wanayoyapata kwa miaka mitano,hebu basi na ajaribu siku moja kiongozi huyo akalala katika kitanda kama hicho japo nusu ya usku mmoja tu seuze alale usiku kucha,bali wanapaswa kufahamu kuwa wapiga kura hao hayo ndio maisha yao dumu daima!!!! Eee Mungu wazindue wapiga kura hawa mwaka huuu!!!! mweee shida hizi balaa tupu na hayaa ndiyo maisha ambayo nyanya yangu kule kijijini kwetu anaishi,humwelezi chochote kuhusu chama TWAWALA!!!!

Simon Kitururu said...

Mmmmmh!

emu-three said...

Sijui, mimi napenda kutolea mfano wa mitandao yetu ya simu iliyopo hapa nchini, mnaionaje? kila siku wanaboresha huduma zao, na kila siku watumiaji mnanufaika, kweli si kweli?
Sasa huo ni mfano halisi wa `ushindani wa kibishara' na ushindani huo unawezekana kabisa katika siasa. Leo huyu akiboronga mweke mwingine uone atakavyofanya, akiboronga mweke mwingine, na mwisho wa siku hali inatengamaa...lakini hayo hatuyaoni? Kura yako, ndiyo pekee inayoweza kuleta mabadiliko, usikae pembeni na kulalamika, wakati sasa umeshikilia mpini, tarehe ikifika ukizubaa, makali yanaelekezwa kwako, utamlilia nani wakati umeyataka mwenyewe!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kigumu chama cha

Salehe Msanda said...

Asante kwa sms hizo
Zina shule ndani yake.
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuwajibika japo kwa asilimia 60% katika nyanjazote ndipo tutaona matokeo mazuri ya kuwepo kwetu hapa duniani

Tuna deni la kuonyesha kwa vitendo n i si kuishia kulalamika na kulaumu wengine.
Swali la msingi ni kujiuliza wewe kwa nafasi yako unawawezeshaje wengine kusikia nafuu japo si furaha ya wao kuwepo hapa duniani na uwepo wako na hicho unakijua kinawasaidiaje wengine? na si kuwaongezea maumivu/

Kila lakheri

Anonymous said...

Markus....LOL

Koero