Mmasai kakamatwa kwa kosa la kukojoa hadharani, akafikishwa mahakamani. Aliposomewa shtaka akubali, akahukumiwa miezi sita au kulipa faini ya sh. elfu hamsini,mmasai akamuuliza hakimu, muheshimiwa huko jela nalala bure na iko chakula ya bure? Hakimu akamjibu, ndio. Akauliza tena na masiwa ya bure iko? Akajibiwa, ndio, Mmasai akamwambia hakimu, basi ongesa miaka tano na iambie mama yeyo(yaani mkewe)ije na watoto yangu yote maana huko iko na raha . Hakimu na watu pale mahakamani wakavunjika mbavu kwa kucheka….. Basi nawe nadhani umeungana nao kuvunja mbavu….
Habari hii nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio na nikaona si Vibaya nicheke Nanyi
9 comments:
nimecheka kweli, Mmasai akaona kaupatia vya dezo dezo kumbe.................
Kama sikosei wanaita kujimba dawa!
Ili kuenda na wakati nadhani mabasi yaendayo masafa yanapaswa kuwa na maliwato ili watu waweze kujichana na kuburudika wapendavyo.
Mabasi ya kisasa siku hizi yamekuwa yakitoa motisha kama vile soda n.k Sasa unategemea abiria akipata haja atafanyeje?
abiria wengine wanapenda kunywa bia kwa raha zao, ni ukweli usiopingika kuwa alcohol huwa zina tend to depress Antidiuretic hormone or vasopressin na hivyo kufanya reabsorption ya maji kwenda kwenda kwenye damu kuwa kidogo na hivyo figo kurusu maji kutiririka kwa kasi katika mfumo wa mkojo na hivyo kusabibisha kitu kinachoitwa Diuresis. Sasa nani alaumiwe hapa!
Wenzetu ulaya wamefanikiwa kwa hili la kuwa na maliwato kwenye mabasi ya masafa. Kila motisha lazima uwe na outomce. Ukitoa soda kwa abiria kama motisha basi utegemee mkojo na hivyo lazima kwa wahusika wa mabasi kujiandaa na mazingira ambayo yanaweza kujitokeza hapo.
Sahihisho: kuchimba dawa
Jamani mie nimeamua kutokucheka!!
Kwani mzaha huu unanipa taswira ya baadhi ya watu, wanaangalia kitu kidogo cha bure bila kujua madhara ya huo ubure :-(
Hahaaa Mmasai Hajatulia huyu,eti na mama yeyo na watoto nao waende jela lol...
watu wendawazimu jamani
Mh!! huyo Mmasai naye jama!!!
mmmh!
Hii balaa tupu!!
Post a Comment