Tuesday, February 25, 2014

VAZI LA KANGA NI MUHIMU KWETU TUSISAHAU VAZI HILI NA TULIKOTOKA: KANGA!!

 Kanga ya kwanza imetegenezwa mwaka 1870 na mwanamke kutoka kisiwa cha Zanzibar.

Kanga ni kitambaa chenye umbo la mstatili na rangi mbalimbali. Kipimo chake cha upana ni 44 inchi hivi na kipimo chake cha urefu ni inchi 60 hivi.
Kwa watu wa Afrika ya Mashariki, hasa wanawake, kanga ni  nguo muhimu sana. Mara kwa mara, wanawake wanavaa kanga wakati wa kupika, kusafisha nyumba, kuteka maji, na kadhalika.
Tena, kanga zinavaliwa na wanawake kwenye arusi, kwenye msiba, nk. Kanga si nguo tu. Matumizi ya kanga ni mengi. 
Kama kanga hii isemavyo TUSISAHAU KWETU...!!

3 comments:

Rachel Siwa said...

Asante sana KADALA..Jee unamfundisha binti yetu Kufunga/kuvaa kanga?

Pia kuna wanaume wengine wanavaa/funga KANGA..jee Shemeji wa mimi ana Vaa/Funga?......

Yasinta Ngonyani said...

KACHIKI..Yaani kama ulikuwepo Binti yetu anavyopenda kanga yaani basi tu..Shemeji wa wewe mmmhh si kanga labda kanzu:-)

Nicky Mwangoka said...

Dah safi sana. Khanga ni vazi zuri na la heshima hasa kwa mwanamke mtanzania. Ningefurahi jadi hiyo ingedumishwa.