Wednesday, February 26, 2014

LEO TUENDELEE UTAMADUNI HUU WA NYWELE..MTINDO WA NYWELE!!!!

Nimekumbuka leo mtindo huu wa nywele nadhani pia hakuna mdada/mwanamke asiyekumbuka mtindo huu wa nywele. Binafsi nakumbuka zaidi nilipokuwa shule ya msingi , ni mtindo huu tu ulikuwa unasukwa kwa wasichana kama hutaki basi kata nywele...Basi kila jumapili na jumatano ni kusuka ili nywele ziwe safi maana usiposuka mkasi unapita kichwani au wembe pia, kama vile msalaba. Nashukuru nilikuwa sina shida ya msusi, msusi wangu alikuwa mama  kama alikuwa amesafiri basi majirani walinisuka....Je? nawe ulikuwa unasuka msuko huu? na,  je? uliuitaje msuko huu? Mimi na rafiki zangu  tuliuita mtindo/msuko huu TWENDE KILIONI. SWALI JINGINE:- JE? ni kwa nini mtindo huu unaitwa Twende kilioni?.....

6 comments:

Emmanuel Mhagama said...

Ni kweli nakumbuka pia hata shuleni kwetu ni mtindo pekee uliokuwa unaruhusiwa kusukwa na wanafunzi. Labda la kuruhusu mtindo huu pekee ni kuepuka mashindano baina ya wanafunzi yanayoweza kuletwa na mitindo mbalimbali ya nywele. Hata hivyo kwa sasa hali tofauti sana hasa kwa shule za binafsi. Wanafunzi wanasuka mtindo wanaotaka na mapambo juu, kama vile vibanio kwa namna mbalimbali. Sina hakika na athari zinazoweza kuletwa na uhuru huu katika masomo ya wanafunzi.

Sina hakika kwa nini unaitwa twende kilioni, lakini nahisi ni kwa sababu mtindo huu ni wa kawaida mno (basic style) kati ya mitindi ya kusuka nywele.
Ni mtazamo wangu tu. SIKU NJEMA.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhagama! kwa asilimia 100% naakubaliana nawe ni kwamba ilikuwa hivyo na pia nashani kwa vile kuna sare basi ikawa ni lazima nywele pia ziwe mtindo mmoja. Ila juzi tu nimeona kwa sasa hakuna kusuka ni kuwa na nywele fupi sana wote sawa wavulana na wasichana...hii nilipenda sana ila nadhani zaidi ni vijijini sina uhakika maana mimi si wa mjini sana:-)
Pia kwa wazo langu nadhani jina hili ni kwa sababu watu wanapokwenda msibani na hasa kwenye mazishi wanakwenda mstari mmoja ...hivi ni nilivyowaza mimi..

Unknown said...

Tena ilikuwa mwisho nywele tano wenye ndefu wenye fup 8

Unknown said...

Tena ilikuwa mwisho nywele tano wenye ndefu wenye fup 8

Unknown said...

Tena ilikuwa mwisho nywele tano wenye ndefu wenye fup 8

Unknown said...

Tena ilikuwa mwisho nywele tano wenye ndefu wenye fup 8