Saturday, May 23, 2009

KARIBUNI TUJUMUIKE (CHAKULA NI UHAI) + MAISHA


Chakula ni muhimu hapa ni ugali, kisamu, kachumbali na samaki karibuni sana!!!!

7 comments:

Anonymous said...

asante sana kwa karibu ya chakula, tunakula kwa macho. mhh hao ni samaki aina gani? vituvi, mbelele, hangu, makambali, magege? chisambu chinoga kifuku wakati wa ligela, mm napendelea zaidi pitiku!!

Mzee wa Changamoto said...

Hapa umenipa MENU ya lunch yangu. Nilikuwa nawaza "combo" ya kujipikilisha ili nile mchana, lakini nimeiona hii, naiiga na naamini changu kitanoga kama hiki.
Wacha nianze kuchemsha kisamvu maana nacho kinachukua muda kwelikweli. Lol
Asante kwa ukarimu na tukiweza tutakaribia (japo kwa fikra)
Blessings

Mwanasosholojia said...

Woww! Shukrani da Yasinta, msosi wa nyumbani haswaaaa! Tatizo huku bwana mambo hayo adimu...machakula yao hayana ladha, huwa tunatafuta samaki vibua siku moja moja na kupika ugali wa nyumbani na bamia. Nimemiss vitu hivi ila si kitu, nina siku kama mbili tu, jumatatu nakwenda home bongo kwa likizo..so nitakula saaaaana!

ahsante tena kwa kunidondosha mate ya uchu!

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina umenikumbusha na kunidondesha mate kusikia hilo neno PITIKU nakalilya kila siku patawili kunyumba si umanyile chawili chifuku. Na hiyo samaki ni mbufu :-)

Mubelwa asante ila nakuomba ukishapika usinisahau kwani mimi ugali na samaki na halafu kisamvu huwa sishibi kabisa. Lol

Kaka mwananasosholojia, ni kweli kabisa ila mimi hapa nilipo nina bahati kidogo huwa nanunua samaki wa kutaka Asia kama vile redsnaper nk. na pia nilichukua dagaa nyasa na unga wakati nafika yaani hii juzi pia nilichukua mbegu za mchicha na mamboga kwa hiyo hapa nilipo nimeziotesha. Kwa hiyo anayetaka anakaribishwa kuja kusaidia kulima bustani-

Umeniumiza sana roho uliposema jtatu untakuwa nyumbani kwani nakuonea wivi kweli. maana vyakula vya huko kazi kwelikweli. Ok Basi nakutakia safari njema kakangu.

Koero Mkundi said...

UMENITAMANISHA KWELI DADA YASINTA....

Yasinta Ngonyani said...

Mdogo wango Koero! mbona sasa kinyume we iko huko nyumbani ndio kwenye vyakula hivyo. Basi nipikie nakuja. Kama umetamani basi najua utaenda kwa Bibi Koero na atakupikia au?

SERENGETI GRILL said...

Mubelwa nyie huko mna bahati sana mnapata kisamvu!!!, mimi kisamvu nanacho wauzia mpaka kitoke thailand na matayarisho yake si kama ya nyumbani, kisamvu cha thailand wenyewe wanakichuma halafu wanakianika kikikauka ndipo kinafungwa kwa ajili ya export, si kama cha kwetu tunachemsha kwanza yaani hapo ukitaka kiwe na test at least kidogo kama ya nyumbani kinahitaji vikolombwezo zaidi