Kama ukimuuliza au ukiwauliza watu wanaooana, kwamba kwa nini wanaoana au ni kwa nini wako kwenye ndoa? Utapata majibu tofauti tofauti kulingana na namna watu hao wanavyotafsiri neno ndoa. Mimi sitajibu swali hilo lakini labda kile ninachokusudia kukiandika hapa huenda kikakusaidia kupata jibu la kwa nini watu wanaoana.
Kuna ukweli kwamba binadamu wamefanya kuoana kama jambo la kimaumbile, na wakilifunganisha na tendo la ndoa. Mtu anajikuta akioa au kuolewa tu. Hana haja ya kujiuliza ni kwa nini anaoa au kuolewa, kwa sababu anaona watu wanoa na kuolewa na akiangalia umri wake anaona kwamba amefikia umri wa kuoa au kuolewa hana haja ya kutaka kujua sababu. Hivi ni nani aliyepanga umri wa kuoa au kuolewa? Na umri wa kuoa au kuolewa umapangwa kwa kuzingatia vigezo gani? Je kupitisha umri huo kuna athari gani?
Ipo sababu nyingine inayotajwa kuwa watu wanoana kwa sababu wamependana, upendo ninaouona hapa ni wa mtu kumtamani mwenzie awe mwanamke au mwanaume, kwani kwetu sisi tunaamini kuwa kutamani ndio kupenda.
Hivi kam watu wanoana kwa sababu ya kupendana kungekuwa na talaka kweli? Naamini kama kungekuwa na talaka basi zingekuwa ni chache sana, na wanaoachana wasingeachana kwa ugomvi na visasi, bali wangeachana kwa upendo na wangeendelea kupendana na kuheshimiana, kwa sababau upendo ni tofauti na kutamani, upendo upo na utaendelea kuwepo na si vinginevyo.
Utakuta wanandoa wanasema “sisi tumeoana kwa sababu tunapendana” lakini baada ya mwaka wanandoa hao hawaelewani na wanakuwa na ugomvi wa mara kwa mara mpaka kufikia mmoja kumuua mwenzie, huu ndio upendo wa aina gani?
Ndoa za namna hii, hazikuwa ni za upendo bali watu kutamaniana au mtu kutamani mwili wa mwenzie, lakini kulikuwa hakuna upendo miongoni mwao.
Wengi wameoana kwa kufuata mnyororo ule ule wa kuoana kwa kufuata dhana iliyowekwa na jamii kuwa ni lazima watu waoana bila kutafuta tafsiri ya kufanya jambo hilo. Na mara waingiapo katika ndoa huona kama wamejitwisha mzigo mzito wasioweza kuubeba. Kuna zile kauli zinazotolewa ambazo wengi huita usia kwa wanandoa kwamba ndoa ni kuvumialiana, lakini watu hawajiulizi ni nini maana ya kuambiwa ndoa ni kuvumiliana, kuvumiliana kwa lipi? Kuna kitu gani katika ndoa kinachohitaji watu kuvumiliana?
Haya maswali inapaswa watu wajiulize kabla hawajaingia katika ndoa maana kuna mambo mengine hayafai kuvumilia, sasa itakuwaje nikishindwa kuvumilia? Na kuvumilia huko ni mpaka wapi?
Kuna watu wengi wanapata shida katika ndoa kwa sababu hawakujua ni kwa nini wanaoa au kuolewa, inawezekana, waliunganishwa na tendo la ndoa zaidi na sio upendo, na hapo ndipo wanpokuja kugundua kuwa walifanya makosa.
Nadhani imefikia wakati sasa ya watu kujiuliza ni kwa nini wanaoa au kuolewa, kwani ni hii itapunguza magomvi na talaka katika ndoa.Inabidi kila mtu awe na sababu yake mwenyewe ya kuamua kufanya hivyo sio kwa kuangalia sababu zilizowekwa na jamii au kusukumwa na matakwa ya jamii bali uwe ni uamuzi wake mwenyewe bila kushurutishwa au kusukumwa na matakwa ya jamii.
Kama hujaoa au kuolewa isikupe shida tulia, na ukitaka kuoa au kuolewa ufanye hivyo ukiwa na sababu yako binafsi.
16 comments:
Hata mimi nimekuwa nikiuliza muda mrefu kuhusu maana ya ndoa au watu kuoana, lakini sipati jibu muafaka....
naona dada Yasita umetuacha hewani, nadhani wewe unalo jibu la kwa nini watu wanaoana, kwani mwenzetu wewe tayari uko ndani ya ndoa siku nyingi, naomba utufafanulie hilo fumbo.
Kwa mfano mimi nikikutana na mwanaume akiniambia nakupenda namjibu ahsante. Lakini kumbe neno nakupenda kwa wanaume wengi linamaanisha kuomba tendo la ndoa pasipo ndoa, na hapo ndipo ninapobaki nikijiuliza kwamba upendo wa dhati utauonaje kwa wanaume wa siku hizi wenye tamaa ya fisi kwa wanawake.
Yaani hawana simile wala kujiheshimu kwao ngono ndio kitu cha msingi kabisa katika kudumisha uhusiano vinginevyo hakuna upendo. Hebu kuwa na boy friend halafu uwe na matatizo ambayo yanakuzuia kufanya tendo, atakuvumilia sana kwa siku mbili tu, baada ya hapo humuoni tena, yuko kwa wengine, ili kutafuta ridhiko, hivi hapo kuna upendo? ndio maana sifikirii kuolewa.....
Duh!! Dada zangu mmeua. Yaani K unasema hutaki kuolewa?? Kwa sababu ya hao wachache unaowaona wanakuwa walivyo? Kwani unawafahamu wanaume wangapi na ni wangapi unaoona wanafanya uyachukiayo? Tusishituke tunapoambiwa kuwa wananchi MILIONI MOJA wameandamana kuunga mkono upuuzi tukashituka wakati tunajua kuna wananchi milioni 40.
Angalia idadi ya uwajuao na ile ya watendao hayo na kisha niambie ni asilimia nbgapi ya hao wanatenda uyachukiayo.
Kisha tutasonga kuanzia hapo
Lakini kuna ukweli katika mengi uliyosema Dada
Baraka kwako na kwa Da'Mdogo K.
Koero mdogo wangu! wala usiogope kama alivyosema kaka Mubelwa sio wanaume wote wapo hivyo. Ila najua au inasemekana mwanaume anaweza kuvumilia kushindwa katika elimu, kazi, na hata jamii, mradi tu yeye na mke wake wanashirikiana vizuri sana katika chumba cha kulala. Kwani wakishindwa tendo hili basi inaonyesha kushindwa katika maisha.
Na kuna wale ambao huwatesa wake zao kwa vile wanakuwa katika hali ya ulevi nk. kwa hiyo nakuomba usiogope kuolewa nataka kuja kwenye harusi yako:-)
Mubelwa sante kwa maoni yako mazuri.Nimekuelewa nadhani Koero pia. Tupo pamoja na tutafika tu.
Naungana na waliotoa maoni hapo juu, hata hivyo ni swali limeulizwa kwamba "kwa nini watu tunaoana?" Binafsi jibu tunaoana kwa sababu kuoana ni hitaji lililo ndani yatu kwa ajili ya kuondoa upweke na katika upendo wa kweli hii ni pamoja na wakati wa raha na matatizo, tunaoana kwa sababu tunahitaji kuendeleza familia (vizazi) ni hitaji lililo ndani yetu kwamba siku moja niwe na familia bora.
Pia tunaoana ili kufurahia maisha na yule unampenda (mwanamke na mwanaume).
Achana na wachache ambao akikwambia anakupenda ana lake wengi tunataka kuwa na familia bora na kuwa na mwenzi ambaye pamoja katika shida na raha maisha huendelea.
Upendo daima!
koero nimekuonya sana juu ya kuwachukia wanaume lakini hutaki, hiyo itakupelekea kuolewa na usiyempenda nakwambia.
watu wanaoana kwa sababu wanapenda kufanya ngono kwani sisisote nimatokeo ya ndoa na ngono.hata miminimeoa kwa sababu hiyo.
eti ukiwa mbali na mwenziohuwa unamwambia umem-miss, huwa unamisi niniyeye kweliau? si ngono tu??
nimeoa kwa sababunapenda ngono!!!
mhh, hii mada kali, nimefurahishwa na Koero na wote mliochangia mpaka ss, kifupi nimekuwa nikimsoma soma Koero, yaonekana anawaogopa ogopa sana wanaume, "sijui walishamtenda".usiogope sana kwani kwa kufanya hivyo unaweza kuja tumbukia pabaya kama mshauri mmoja alivyosema, pia kama nakumbuka vizuri habari uliyoitundika kwenye blog yako siku ya akina mama, nilitegemea ile habari ikupe motivation nawe ya kuwa na familia yako na kuilea kwa mfano uliojifunza toka kwa mamako. pamoja na hayo, najua sasa hivi unachomoa chomoa habari za kuolewa kwa vile hujampata mjanja wako, siku ukimpata utatamani ndoa ifungwe hata usiku usiku! tehetehe!
Kwanza samahanini wadau kupotea hewani kwa muda flani hapa katikati, mambo yalikua yamebanana sana kuweka hatma yangu sawa.
Nije kwa mada.Ni swali la msingi sana kuuliza kwanini watu wanaoa au kuolewa.Huwa kuna sababu nyingi sana.Binafsi naamini kwanza mapenzi unapoingia lazima aidha kwa kuficha au kwa kuweka wazi, ni lazima uangalie maslahi.Najua watu watasema kamwe mapenzi hayaangalii maslahi.Mimi msichana ukisema unanipenda nikikuuliza nipe sababu za msingi, wengi husema jinsi ulivyo.Nipo vipi??Swali la msingi.Maana mimi nina kaka zangu mapacha, ni identical, majina yao ni jina moja limemegwa, wanaitwa Alex na Alexander.Wamesoma pampoja kuanzia primary hadi Chuo kikuu, na hadi sasa wanakaa chumba kimoja.Sasa wewe useme njinsi ulivyo, in terms of what?Hapo ndipo mambo ya kimaslahi yanakuja.
Maslahi yapo yanayoonekana na yaliyojificha.Kuna mtu kusema ni "kipanga" ana akili darasani mfano, hilo ni moja ya maslahi, mwingine atasema huyu dada ni mwanamke wa shoka, mambo yatakua sawa.Hivyo kuna mambo mengi, na mara nyingi sababu hizo zinaweza kuisha then ndipo hapo kizungumkuti kinapoibuka.
Kuna wengine wanaoa kwa sababu za mishe, kikazi nk.Mfano, kwa Tanzania ni ngumu mtu kuwa rais kama huna mke.Hivyo hata kama ulikua huna mpango wa kuoa, inabidi uoe ili uingie uraisini.Mfano mzuri ni issue ya Mramba, Mkapa na Mama Anna Mkapa, hapo ndio utaona kazi ya Urais na ndoa umuhimu wake.
Wengine huoa kwa sababu za kitamaduni.Ni mazoea ya jamii nyingi mfano Tanzania mtu kuheshimika zaidi anapokua ndoani.Mfano ni kwa mwanamke kutoolewa na kuwa ndoani ktk umri fulani inaondoa heshima flani, hiyo inafanya wasichana wengi waingie ndoani ile kutafuta tu "heshima", na wengine kusema kuondoa nuksi, mkosi.
Mimi sijajua nitaoa kwa kigezo gani mpaka sasa.Ila lazima maslahi yawepo mbele.Nitaoa mtu najua naye atanisaidia sio mimi tu.Kunisaidia sio lazima kifedha, kimawazo, na hata kugawa chomozome ili mtoto awe na bongo iliyochangamka.
MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
Nawashukuru wote mlionipa changamoto, kaka Mubelwa, Kaka Kamala, kaka Mbilinyi, kaka Makulilo na wewe usiye na jina.
Nilijua kwa kuwa nimewazodoa wanaume basi wengi mtajitokeza kutetea mfumo wenu dume. Nakubaliana na Kaka Mubelwa kuwa sio wanaume wote wenye tabia ya ukware kama nilivyoeleza, ingawa asiye na jina anahisi kuwa huenda wanaume walinitenda, kutokana na msimamo wangu pindi ninapochangia maoni kuhusiana na maswala ya ndoa.
Nakumbuka siku moja kabla sijawa binti Kigori(Nadhani mmenielewa) niliwahi kumuuliza Namsifu (mama yangu) kuwa kwa nini aliolewa na baba, jibu lake lilikuwa ni rahisi sana, alinijibu kuwa alioana na baba kwa sababu walipendana.
Lakini upendo aliouzungumzia mama yangu ulikuwa ni upendo wa dhati.
Kwa mujibu wa simulizi za bibi Koero, aliwahi kuniambia kuwa enzi zao walikuwa wanakaa uchumba hata miaka mitano bila kugusana mpaka pale watakapofunga ndoa, ndio wanajuana, lakini wanaume wa siku hizi thubutuuu!!! Akikuchumbia tu leo, kesho anataka kuonja, ukimshauri kuwa asubiri mpaka mfunge ndoa atakushangaa sana na kukuambia tena bila hata aibu, kuwa hawezi kumuoa mwanamke bila kumuonja, He imekuwa mchuzi!
Na iwapo mwanamke akikataa basi na uchumba utakufa, kisa amenyimwa kuonja!
Na ndio maana nasema kuwa siku hizi upendo katika ndoa hakuna kwa sababu wanaume wa siku hizi ni wasanii na upendo kwao ni tendo la ngono kama alivyokiri Kamala kuwa alioa kwa sababu anapenda sana ngono, na ndio maana nampenda sana Kamala kwa sababu ni mkweli wa nafsi yake, hatafuni maneno.
Asilimia kubwa ya wanaume wa siku hizi wamegeuza upendo kuwa tendo la ngono, na ndio maana wanaoongoza kwa kulalamika ukweni kuwa wananyimwa tendo la ndoa ni wanaume ukilinganisha na wanawake.
Mimi sijawahi kuingia katika mitego ya wanaume wa aina hiyo na wala sikatai kuwa ipo siku nitaolewa, ila sipendi kuharakisha jambo hilo. Kwa nini nikimbilie kuolewa?
Ili iweje? Mimi naona kuolewa ni au kuoa ni uamuzi wa mtu binafsi na haihitaji kushwawishiwa au kulazimishwa, ni jambo ambalo linajitokeza lenyewe, na kwa mtu mwenye busara anajua tu kuwa huyu ndiye anayenifaa.
sasa Koero umeongea "wala sikatai kuwa ipo siku nitaolewa, ila sipendi kuharakisha jambo hilo. Kwa nini nikimbilie kuolewa?
Ili iweje? Mimi naona kuolewa ni au kuoa ni uamuzi wa mtu binafsi na haihitaji kushwawishiwa au kulazimishwa, ni jambo ambalo linajitokeza lenyewe, na kwa mtu mwenye busara anajua tu kuwa huyu ndiye anayenifaa". hapo ndio nilikuwa na hoja napo, kwamba siku ukipata mwenyewe utatamani hiyo ndoa ifungwe haraka haraka hata usiku wa manane. mhh Koero hizi habari za kuona kwamba samaki mmoja akioza basi wote wameoza, noma, unataka kuniambia kwa utaratibu huu siku ukimpata huyo jamaa na akiomba kuonja utamuonjesha sio? maana wahuni wanasema kabla ya kwenda kuwinda ni vyema ukanoa mshale wako "before you go hunting sharpen your spear". kwa kadiri ya simulizi za bibi Koero, basi na mimi nimekuwa kama mzee wa zamani, maana nipo katika umri wa mwanzo mwa miaka ya 30 na mke wangu nilifahamiana nae yapata miaka tisa iliyopita na tulikuja kuoana baada ya miaka sita tangu tufahamiane na kuwa marafiki-wachumba, na hatukucheza kale kamchezo anakokaogopa Koero! haya kila la kheri Koero, utapata tu huyo mjanja wako na ukimpata kweli na kumuonjesha itakuwa imo tu!! mhh hivi kuna ndoa bila tendo la ndoa (ngono) jamani!! wacha watu walalamike kama wananyimwa "uhausi", ila kwenda kulalamika ukweni noma!!
Darasa, darasa, darasa. Naendelea kujifunza tu. ASANTENI NYOTE
Naona usiyena jina unaonekana kunishupalia sana. Ukweli ni kwamba sitarajii kuonjwa wala kuonjesha na kwangu mimi hakuna mjanja yeyote anayeweza kuthubutu kutaka kunionja...
Kwa taarfa yako nimeshapambana na vijanadume kibaao mpaka wale wanaoazima nguo na magari ili kuwatokea mademu lakini sibabaikiii vitu vya kupita..kwani mimi ni zaidi ya mwanamke.
Kwanza ngoja nikwambie unajua kama nawaonea huruma sana wanaume wanaojifanya wajuaji wa kutongoza.
Tena wengine wana mbinu zakitooto....lakini kawaida yangu mwanaume akijifanya anajiongelesha....nikimkazia macho mwenyewe anaanza kujiumauma,halafu mimi ndio nageuka muongeaji.....nishamtaimu zamaaani....
Anyaway kwa kifupi mimi sio mtu wa kubabaishwa na vijanadume....kwangu mimi life goes on........
labda nikipata mjanja nitaolewa......ha ha ha ha haaaaaa
utangoja saaaaaana!!!!!!!!!!!!!
naona majadala unakuwa wa koero sijui kwa nini shauri zenu.
koero sema umekutana na wajinga na masupastaa wa bongo na kinachokusaidia ni kutokuwa na tamaa za kijinga wala kuendeshwa na vitu vidogo na kuvumilia mihemko kama vile nyege nk. kwa hiyo hutamani cha mtu bali mekamili, umejipokea na kujikubali jinsi ulivyo kwa hiiyo unajipenda. ukosefu wa kujipenda ndio unaowapoteza wasichana wenzio kwamba wanatafuta ukamilifu wao kwa wengine. wanavaa ili wasifiwe, watongozwe nk. kwa hilo nakupongeza.
onyo! kuwotolea macho wengine yaweza kuwa noma kidogo.
kwa wanaojua nguvu ya macho na jinsi ya kuyatumia wanaelewa. hili nitalijadili siku chache zijazo.
hata jinsi ya kumpata mkwelini rahisi kwani ukimwiti anaitika vyema na kukufikia.
labda tujadili juu ya ndoa nini na kufundishana tendo la ndoa. matatizo yote ya ndoa yanatokana na upungufu wa uelewa juu ya tendo la ndoa. wengi hulifanya lakini hawalijui na hivyo hupotea ndio maana niliwahi kuliandikia kwa kina. tendo la ndoa likiwajema na likinoga, hamna tena maswala ya haki sawa kwani nyoote mnaipeana kitandani.
Da Koero kuna msemo mmoja unasema hivi, MEN GIVE LOVE IN ORDER TO GET SEX, AND WOMEN GIVE SEX TO GET LOVE. Maelezo yako yapo hapo kwa kiasi kikubwa.Na mimi binafsi naliona hilo kuwa ndio limeenea kwenye jamii zetu.
Lakini vile vile sio kila wakati anayetaka kuonja ni mwanaume tu.Hiyo ni changamoto iliyo mbele yetu.Kuna mabinti ukiwa nao ktk urafiki wa kimapenzi, na ukawa na mawazo kuwa utafanya nao ngono hadi ndoani, aidha atakwenda kwa jamaa mwingine kufanya nae kiuficho wewe usubiri hadi ndoa, wengine wanasema hawawezi kununua mbuzi kwenye gunia, both wake kwa waume, wengine wamefikia hatua ya lazima kucheki kama wana uwezo kuzaa kwa kupeana mimba kwanza ndio ndoa ifungwe nk.
Kazi kwelikweli hapo.Nami napata darasa kama Mdau Mbelwa, Mzee wa Changamoto alivyosema.
MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
Duh! Mjadala mzito sana huu,
Naona walionitangulia wamesema karibu yote. Ila nina machache ambayo ningependa kuchangia katika mjadala huu.
Nakubaliana na tafsiri ya kaka mbilinyi juu ya dhana nzima ya ndoa, lakini labda niulize, hivi hivyo alivyosema Mbilinyi ndivyo ilivyo?
Je dini zinatafsirije neno ndoa? Hilo naona tuwachie wanazuoni, nadhani wao wako kwenye nafasi nzuri ya kulieleza hilo.
Ukweli ni kwamba kila mtu anayo sababu yake binafsi ya kwa nini ameoa au kuolewa, wote hatuwezi kuwa na tafsiri moja, Inaweza kuwa ni kwa sababu ya uzuri, yaani mmoja kamtamani mwenzie kwa sababu ya uzuri, inaweza ikawa ni umbile, inaweza ikawa tendo la ngono ambalo nalo limepewa nafasi kubwa sana na jamii kama mhimili wa kushikilia ndoa, kitu ambacho hakina ukweli kabisa, inaweza ikawa fedha, au hata umaarufu.
Kuna wanadoa wengine wamejikuta wameoana kwa sababu ya kuunganishwa na marafiki, familia kuwa karibu, au hata kushawawishiwa na ndugu rafiki au hata wazazi.
Dini nazo zinatajwa kama chanzo kizuri cha kukutanisha watu, .
Hata hivyo pia kuna sababu ambazo ukizichunguza hazina kichwa wala miguu na nyingine ni za kipuuzi tu.
Lakini ndizo zilizowakutanisha watu hao wawili wakaamua kuoana na kuishi pamoja.
Tatizo ni pale kila mmoja anapoona kuwa mwenzake hakidhi matarajio yake au hana zile sifa ambazo mwenzie alitarajia kuwa angekuwa nazo, pia wapo wale ambao wanajua kabisa kuwa mwenzie hana sifa anazozitaka, lakini hukubali tu kuoa au kuolewa kwa matarajio kwamba atambadilisha mwenzie na matokeo yake anapoona kwamba mwenzie habadiliki ndipo migogoro inapoanza na hatimaye ndoa kuvunjika,
Lakini ni bora ivunjike kwa amani, kwani wengine hufikia hata kuuana au kutiana vilema vya maisha.
huu ni mwaka 2011 nimepitia mjadala huu na nimeuelewa. nami namuunga mkono dada kowero .
nafkiri ni unyanyasaji mpya kwa wanawake kwamba hadi uze nae au ufanye nae sana mapenzi na kujionyesha wewe una adabu sana yaani unampenda unamjali akifanya makosa useme 'dear nimekusameha naomba usirudie tena 'kumbe roho yako imeshazimia kwa maumivu. naomba tusitesane jamani. upendo wa kweli na uaminifu udumishwe mwisho wa siku maisha ni kama ndoto tutakapoondoka. asanteni.
mapenzi ya kweli na amani ya rohoni viambatane na wawili hawa wawe wamejitayarisha vizuri ili waweze kufaidi ndoa yao. looooove comes first na mengine yatafuata.na maendeleo pia. kama anavyosema kaka makulilo.
Post a Comment