Saturday, May 30, 2009

UJUMBE WA LEO

Kila siku nimekuwa nikiwaza ipi ni afadhali:
Mnajua ya kwamba afadhali mtu akupige makofi/viboko. Kuliko kumpiga mtu kwa maneno/ kumdharau. Kwa saabu kuna watu ambao hawawezi au hawataki kumpiga mtu ila maneno yake asemayo yanaonekana ni kama kipigo. Au wenzangu mnaonaje?

6 comments:

Anonymous said...

Yasinta, ebu sema sasa hivi nani kakupiga kwa maneno nipate kumshughulikia sa hii hii! Ala, analeta mchezo au nini?
Uliyosema ni kweli. Kuliko kuanzisha vita ya maneno ni bora kuchukua jembe ukaenda kulima hata kama ni majira ya kiangazi itakuwa bora kuliko mavuno utakayovuna kutokana na vita ya maneno.
Wakale walisema, 'afadhali ya mchawi kuliko mfitinii', waliyaona haya.
Uzuri wa mfitini na mwenye kidomo domo ni kupuuzia kauli zake zote ikiwa za ugomvi, japo vigumu lakini inawezekana kabisa.

Mzee wa Changamoto said...

Subi naye kwa mikwara? Eti
nipate kumshughulikia saa hii hii" Lol
Kuna ukweli wa athari za kisaikolojia kwa waathiriwao kimaneno. Viboko vyaweza kukuchubua na kisha kidonda kikapona lakini ukishamharibu mtu kiakili kwa maneno, hakuna "aspirini" ya kuifuta hiyo athari kirahisi. Huishia kujidharau, kusongoka kimawazo na wengine kufanya ya hatari zaidi kama kuhatarisha maisha yao
Asante kwa elimu kubwa lakini fupi.

EDWIN NDAKI (EDO) said...

inategema hayo hicho kipigo unachosema ni cha kiwango gani..


Kuna mtu anaweza kukupiga kiasi kwamba ukifika hospitali wanakuuliza umegogwa na gari au umepeta ajali kutoka kwenye ndege kwa jinsi mtu anavyokuwa kaharibika au hata kupelekea ulemavu.

so mi nashauri ni bora KUELEWANA kuliko yote mawili uliotaja maana hayana nafasi katika dunia iliyo bora.

tutafika tu

Koero Mkundi said...

Lakini ni vyema tukikumbuka kwamba kuna vipigo vingine hufundisha....
Hiyo nimesoma pale kwa kaka Mtambuzi, kuna mahali alisema kila jambo baya lichunguze lina uzuri wake pia...
kwa hiyo dada Yasinta kama kuna mtu kakuchapa leo iwe ni kwa bakora au kwa maneno basi mshukuru kuna jambao kakufunza mwenzio.... kama umeshindwa kung'amua, basi ni vyema ukimuuliza nae atakujuza.....

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ndakiiiiiiiiiii!!! kipigo chako ni noma, kimenifurahisha sana. au tufananishe na roba la manzese nini.

anyway, we piga kwa maneno tu harafu tuone. kusema si ni haki yako na una uhuru na kila ukisemacho ni mtizamo wako tu!

Anonymous said...

Mzee wa Chchzzz wewe ndiwe umemkorodisha Yasinta sasa unaogopa kipigo changu unaita mkwara? Sasa usubiri nitoke chumba cha mazoezi ndiyo ujue habari yake. Unapata kichapo mpaka nahakikisha nakuachia fursa ya Daktari Bingwa tu kufany a matibabu kwa maana hao wengine watakuwa hawajui kilichokutokea kama alivyoainisha Edo.