Wednesday, November 5, 2008

TATIZO NI LIPI?

Mpaka watu wawe na roho mbaya ya:-

Usafirishaji haramu wa watu/biashara ya watu(Human Trafficking) ni nini?
Usafirishaji na biashara haramu ya watu (Human Trafficking) ni nini?

Usafirishaji na biashara haramu ya watu (human trafficking) ni uhamisho wa mtu kutoka kwenye jumuiya yake na kwenda sehemu nyingine ndani au nje ya nchi kwa ahadi za uongo, matokeo yake ni kunyonywa kunyanyaswa, na kutumikishwa kwa kupindukia bila ya ujira kwa faida ya mtu mwengine, hii hujulikana kama utumwa mamboleo na ni moja ya matishio makubwa ya haki za binadamu. Ingawa usafirishaji na biashara haramu ya watu (human trafficking) huwatokea wanaume, wanawake na watoto, lakini inaonekana wanawake na watoto ndio wanaoathirika zaidi.


Usafirishaji na biashara haramu ya watu hutokea duniani kote na unyonyaji wa watu hutofautiana kati ya nchi na nchi (watoto kutoka Togo wanatumikishwa na kunyanyaswa katika mashamba ya kakoa Ghana, Wasichana wa Colombia wanalazimishwa ukahaba Japan n.k.)

Usafirishaji haramu wa watu/biashara ya watu katika Tanzania

Hali ya Usafirishaji na biashara haramu ya watu Tanzania.

Usafirishaji na biashara haramu ya watu (human trafficking) hutokea ndani ya Tanzania na kimataifa. Watu huletwa Tanzania kutoka Kenya, Uganda, Malawi na Burundi. Usafirishaji na biashara haramu ya watu unaoonekana kutapakaa sana ni ule wa ndani kwa ndani ya nchi unaolenga kuwanyonya watoto katika kazi za ndani.
Tanzania pia inatumiwa kama nchi ya kupitishia wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu toka nchi za pembe ya Afrika(Ethiopia, Somalia) wanaopelekwa Afrika kusini: Kuna wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia
Tanzania ambao serikali ya Tanzania inahisi miongoni mwao wapo wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu. Kuna ushahidi wa matukio ambayo yanaonyesha kuna wahanga wa usafirishaji na biashara haramu kutoka India na Pakistan kuletwa Tanzania.

Watoto wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu waliosaidiwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji/International Organization for Migration (IOM) wengi wao hutokea sana mikoa ya Iringa, Morogoro, Mbeya, Mwanza Singida na Dodoma. Zipo dalili kubwa kwamba Dar es Salaam na Zanzibar ndio vituo vikubwa wanaopelekwa wahanga hao. Watoto hao kawaida hutolewa vijijini kwa kuahidiwa maisha bora na elimu mjini na ndugu zao wa karibu au watu wanaoaminiwa na wazazi wao. Wakati mwingine watoto hawa hutolewa na wazazi wao kwa ndugu kwa mategemeo watoto wao watapata maisha bora wakiwa mjini.
Lakini wakati mwingine hali huwa sio kama walivyotegemea. Unyonyaji ni pamoja na kumlazimisha muhanga kufanya ukahaba, kazi za ndani, biashara za mitaani, kuosha magari bila kupewa nafasi ya elimu na matibabu, bila chakula au chakula kidogo sana, kunyanyaswa kijinsia, kutukanwa, kupigwa, kutishwa na kufanyishwa kazi bila ya ujira. Wengi wa watoto hawa wakifanikiwa kutoroka, huishia mitaani.

Sababu

Elimu ni moja ya sababu kubwa. Upatikanaji mkubwa wa elimu mjini huvutia vijana wa kike na kiume kutoka vijijini, wahanga wengi waliosaidiwa na IOM ni watoto walioacha shule au hawajawahi kwenda shule kabisa kijijini mwao (watoto wa kike 24 kati ya 34 waliosaidiwa mwaka 2007 hawakuwahi kwenda shule kabisa).
Kupoteza wazazi wote wawili. Hali hii husababisha watoto kulazimika kutegemea walezi.

2 comments:

Christian Bwaya said...

Inashangaza kwamba karne tunayoishi ni ya ishirini na moja. Narudia. Ishiri na moja. Lakini bado tunasafirishana kuuzana kama watumwa!

Kweli bado sielewi tatizo ni nini hasa. Kwa sababu siku hizi karibu kila familia ina msichana wa kazi. Eti akina mama hawawezi kulea watoto kwa sababu ya kazi nyingi. Basi. Jukumu la kulea watoto waliowazaa wenyewe eti ni la msichana mtumwa anayeitwa ni wa kazi. Kazi kweli kweli.

Kweli bado sielewi dada Yasinta...

Yasinta Ngonyani said...

Bwaya, Sio kwamba hawawezi kulea watoto ni unyonyaji tu. kwa sababu wao wasichana wa kazi wanasema nina kazi na hela anazolipwa ni kidogo sana. Na hii ya kusafirisha watu ni unyama tu utamsafirishaje binadamu mwanzako kama mnyama. Wapi huruma imekwenda ni kweli kaisa bado tu hatuja amka hii ni karne ya ishirini na moja. Ni kweli KAZI KWELI KWELI