Friday, November 21, 2008

HADITHI YA MWANA MPOTEVU

Hiii hadithi inanikumbusha mambo mengi sana sijui wenzangu mnasemaje?

Kulikuwa na baba mmoja aliyekuwa na watoto wawili wa kiume. Siku moja yule wa mwisho akamwambia baba yake : baba mimi sasa ni mkubwa naomba haki yangu nataka kuondoka kwenda mbali kutafuta maisha. Baba yake akampa pesa nyingi tu. Akaondoka akaenda zake na pesa zote.

Muda si mrefu akapata marafiki wengi tu. akawa anakula na kunywa nao pamoja na yeye ndiye aliyekuwa analipa kila kitu.

Lakini muda si mrefu pesa zote zikamwishia. Akawa hana kitu cha kula. Marafiki zake wote hawakumpa wala kumsaidia chochote isipokuwa walimtupa barabarani.

Siku moja akaondoka akaenda kwa mkulima mmoja na kusema ya kwamba anaomba chakula, aina yoyote ile, na halafu atafanya kazi kwake. Mkulima akamhurumia akampa chakula na akamwambia kazi yake ni kuchunga nguruwe wake.

Hata hiyo kijana bado alikuwa ana njaa. Akaanza kuwaza: kwa nini napata taabu hapa wakati baba yangu ana chakula kingi tu. Narudi nyumbani kwa baba tena. Nataka kufanya kazi kwa baba kuliko hapa.

Mara akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Na kusema baba, naomba radhi nimekosa. Ilibidi nisirudi na wala usinipokee tena hapa nyumbani kwako. Lakini baba kwa uchungu wa furaha akamkumbatia na kumpokea. Kwa furaha kubwa baba akamfanyia kijana wake sherehe kubwa kwa kufurahia kwa sababu kijana wake alikuwa amerudi tena kwake.

Kaka mtu akawa anarudi toka kazini(shambani) akakutana na babake asemaye. Mdogo wako amerudi tena nyumbani njoo tumsherehekee. Alipotea sasa amerudi tena.

Swali: Je? Hadithihii wewe inakufundisha nini?
Na je? ungekuwa wewe ni yule kaka mkubwa ungefanyaje?

9 comments:

Rama Msangi said...

Kitabu cha wageni kiko wapi dada? Kiweke bwana kwa ajili ya sisi tunaopita pita kujiandikisha huko. Ni msangi mdogo hapa na sijapotea kama Bwaya alivyosema, ila nilibadili maskani kutoka msangi mdogo hadi uchambuzi.

Nitembelee katika www.uchambuzi.blogspot.com/ ujiandikishe katika kitabu cha wageni pale. karibu wewe na wadau wako.

Yasinta Ngonyani said...

Asante sana kaka Ramadhani kwa kunitembelea. na karibu tena na tena. Nitatembela uchambuzi

Unknown said...

kwa hadithi yako mimi nimejifunza kutoka kwa kaka mtu jinsi alivyokuwa hajui haki zake na kwamba vyote vilivyokuwa pale nyumbani alikuwa ana haki navyo na angeweza kutumia (kujichana) kadri anavyotaka ila alikuwa hajui.
Hii inanifundisha kwamba unaweza kuwa na rasilimali zinazokuzunguka na ukashindwa kujua zinaweza kukupa utajiri na matokeo yake ukawa unaishi bila kujua.
Pia inanifunisha kwamba haijalishi nimechafuka na kuwa machafu namna gani bado Mungu ananipenda na anaweza kunikubali pale nikitubu na kuacha njia mbaya.

Ndivyo nimejifunza

Yasinta Ngonyani said...

sawa kaka Lazarus. Mimi nimejifunza mtoto ni mtoto hata ukifanya mabaya au mazuri kwa wazazi wewe ni mtoto tu. Pia kama ulivyosema hata ukiwa mchafu mungu atakupokea tu.

asante kwa maoni.

Unknown said...

Nashukuru dada kwa kutupa mambo ambayo muda mwingine inabidi tuumize kichwa,kwangu mimi nimegundua kuwa,tunatakiwa kuwa wepesi kusamehe,na kuwa na ushirikiano na wenzetu,kwan mtu anapoanguka inabidi tumtie moyo na kushrikiana kwakila jambo.
Kwangu mimi ni hayo tu.
Muwe na wakati mzuri na week end njema,
na mnakaribishwa kwenye blog yangu ambayo ni
www.gshayo.blogspot.com

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

swali la msingi ni nani katyi ya hao wawili alikuwa mpotevu. ukweli ni kwamba yule aliyekuwa nyumbani ndiye aliyekuwa mpotevu kwa sababu alijipendenkeza ili apendwa badala ya kumpenda nduguye.

tuwapende wenzetu.

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli G.Shayo kusamehe ni kitu muhimu sana katika maisha, hata kama imekuuma kama nini.

Na kamala ni kweli inawezekana yule aliyebaki nyumbani ndiye aliyekuwa mpotevu. Lakini pia tukumbuke ya kwamba yule aliondoka sasa anakula mali ya kaka yake pia.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hapo ndipo lilipo tatizo la binadamu wa kizazi hiki. mali za kaka yake ni zipi? nai kasema kuna kitu tunamiliki katika dunia hii? mbona vyote tutaviacha?
mali ni zao wote na lazima wanufaike wote sasa kaka yake anataka afurahie mali pekee? je dunia hii kuna kufurahi kweli?
yawezekana nawe Yasinta umepotea bado

Yasinta Ngonyani said...

Labda inawezekana mimi pia ni mwana mpotevu. lakini hapa hii hadithi inatufundisha kwamba kusamehe ni jambo muhimu sana katika maisha.