Friday, November 28, 2008

SALAMU KUTOKA SEMINARY YA PERAMIHO


Karibuni sana Peramiho kuna mengi ya kuangalia

14 comments:

Fadhy Mtanga said...

Da Yasinta,
ahsante sana kwa kuweka picha za Pera.
Nimepata impression kiasi kikubwa kuziona.
Mama yangu alisoma hapo Peramiho Girls miaka ya 60 mwishoni. Lakini pia nilifika hapo hospitali kwa mara ya kwanza Januari 90, mama alikuwa akipata upasuaji wa kidoletumbo.
Mwaka 2001 nikafika hapo wakati nikisoma Kigonsera High School. Nilinunua kitabu cha hadithi hapo bookshop kinaitwa Radhi ya Wazazi.
Nimefurahi kuziona picha hizo.
Ni hayo tu.
Kazi njema.

Yasinta Ngonyani said...

Nimefurahi kama wewe umefurahi. na pia nimefurahi kwa kunitembelea karibu sana tena na tena. Je? mama ana hali gani leo?

Fadhy Mtanga said...

Nashukuru sana.
Mama hajambo kabisa na Mungu akipenda mwakani atastaafu utumishi wa umma.
Picha huhuisha kumbukumbu. Tunakushukuru sana kwa kumbukumbu nzuri ambayo imemfanya bimkubwa awakumbuke swahiba zake aliosoma nao hapo.
Ni kazi nzuri, ninawiwa kukiri hivyo.
Alamsiki.

Yasinta Ngonyani said...

Namshukuru mungu kama mama amefurahi. Labda ilikuwa ni kwa ajili ya yeye. masalimie sana.

Umesema ulisoma kigonsera nina mdogo wangu wa kiume ambaye alinifuata mimi pia alisoma huko jina lake Savio Ngonyani alimaliza form four. Sijui kama unamfahamu. yaani mpaka raha. Salimia sana mama.

Anonymous said...

Du, leo kweli hapa pamekuwa pema sana, mimi huwa napita bila kuacha maoni, lakini leo nimelazimika, umenikumbusha nyumbani Peramiho, kwa sisi watu toka Nakahuga, Peramiho ni kila kitu kwetu, maana hospital, na mambo mengine, soko kubwa la bidhaa zetu ni Peramiho, na pia nimekuta salam toka Kigonsera (Kaigo), safi sana maana mimi nilikuwa mpinzani wao, nimesoma Likonde, baadae nikaendelea katika shule za serikali, mwishowe nikaenda kusoma hapo seminari kuu Peramiho japokuwa sikufanikiwa kumaliza masomo hapo, lakini nilijifunza mambo muhimu sana katika maisha yangu na yananisaidia sana na hasa huku ughaibuni ambako watu imani zimechoka. Du, nimeimiss sana Peramiho our way to Nakahuga. Ahsante sana Nangonyani kwa foto ya lelu.

Fadhy Mtanga said...

Salamu kwa mama zimefika. Tunashukuru sana.
Sikumbuki vizuri jina hilo kwa sababu tuliokuwa A level tulikuwa tukiwapa kampani kitaaluma wa O level, nna hakika anaweza nikumbuka. Mpe salamu. Mwambie bado navikumbuka vile vitafunwa vilikuwa maarufu sana pale shule. Pia wale dagaa waliokuwa wanalowekwa tu kwenye maji kisha kuletwa mesini na ugali mbichi. Mambo ya shule, we acha tu.
Pia nimefurahi mheshimiwa mseminari wa Likonde. Kuna wakati tulipita hapo kwa dharura na basi la Madamba. Na tulikuja pia michezoni na lori la shule.
Jamani, hivi kile kibasi Stela Matutina bado kinapiga ruti za Songea-Mbinga? Na basi la Madamba?

MARKUS MPANGALA said...

Waungwana mnisaidie eee ndiyo nitamwelezaaa!!! MADAMBA, KISUMAPAI kama kawaida ruti bado ila STELA limekwisha habari yake hakuna kitu.
Pia kuna haya ya SAJDA yaani ni express kwelikweli mambo safi tu, ni mwendo wa machicha bila BIA.
karibu sana. Ile bookshop ya Peramiho inaendelea iko safi sana nilinunu kitabu mwezi Januari cha KESI YA SOKORATI(ni tafsiri toka katika kitabu cha Classic kilichozungumzia kesi ya mwanafalsafa Socrates) Peramiho safi sana. najua ulikuja wakati hata barabara ya lami hakuna ila kwasasa full kujilamba yaani LAMI mpaka hospitalini pale hakuna vumbi tena mkuu.
ni hayo tu

Fadhy Mtanga said...

Umenikumbusha kaka, Kasumapai pia ilikuwepo. Napata furaha kusikia hayo. Basi pale Songea ilikuwa ukichelewa ile saa 9 alasiri kupanda Stela basi andika imekula kwako.
Lakini kulikuwa na Land Rover 110 ambazo kule nyuma zilikuwa zikifungwa spade na jembe kwa ajili ya kukwama njiani.
Sasa naambiwa full lami hadi Peramiho. Ni maendeleo makubwa kwani kutakuwa na urahisi katika kuwakimbiza wagonjwa pahala pale panapookoa uhai wa watu wengi.
Nawashukuruni sana kwa kunipa updates hizo.
Kazi njema.

Fita Lutonja said...

Haya nimeferahi sana Da Yasinta kwa kazi nzuri kama hiyo keep it up one day one time utawakonga wengi sana

Yasinta Ngonyani said...

Asante sana wote.Kwa kunitembelea na kutoa maoni yenu mazuri.

Ni kweli sasa kuna LAMI mpaka mlangoni Hospital Pera, nilishangaa sana mwaka jana hakuna vumbi tena. Raha kweli. Karibuni tena.

Anonymous said...

Yasinta,
Wao! Nimefurahia kuona chuo changu cha zama za 1984/5 nikuwa mwanafunzi wa upadre na shirika la wabenedictine kutoka Kenya. Keep it up and will try to see how the blog is growing.
Karibuni Kenya

Martin Amlima said...

I was happy to see Peramiho Seminary entrance. The portion of the building is called "Peace to All".
Peramiho Seminary is a place where I acquired Benedictine Spirituality. Well done Ngonyani, the photo has impessesed me so much.
Thanks
Amlima Martin

Martin Amlima said...

I was happy to see Peramiho Seminary entrance. The portion of the building is called "Peace to All".
Peramiho Seminary is a place where I acquired Benedictine Spirituality. Well done Ngonyani, the photo has impessesed me so much.
Thanks
Amlima Martin

Martin Amlima said...

I was happy to see Peramiho Seminary entrance. The portion of the building is called "Peace to All".
Peramiho Seminary is a place where I acquired Benedictine Spirituality. Well done Ngonyani, the photo has impessesed me so much.
Thanks
Amlima Martin