Ngoja leo tuangalia kidogo magonjwa kwani ndiyo adui mkubwa katika maisha ya binadamu:-
Namna ya uambukikizwaji
Kichocho ni ugonjwa usababishwao na vijidudu ambavyo mtu hupata anapotumia maji yaliyo na vijidudu vya ugonjwa huu hashwa katika nchi za kitropiki. Bilirhazia ni jina la kimelea cha ugonjwa huu.
Viini vilivyokomaa huishi katika mishipa katika kibofu na utumbo. Kimelea cha kike hutaga mayai mengi ambayo hutoka kwa mtu aliyeathiriwa kwenda kwenye maji wakati wa kukojoa au haja kubwa.
Mayai yanapokuta maji huanguliwa na kutoa viluwiluwi, ambao hupenya konokono hawa wa majini. Katika konokono hawa wa majini viluwiluwi huwa hukua na kuongezeka na kutoka. Viluwiluwi hawa wana uwezo wa kupenya kwenye ngozi na wakisha penya huingia hadi kwenye mishipa ya Ini ambapo hukua na kukomaa. Baada ya hapo huingia katika mishipa ya kibofu na haja kubwa.
Vimelea hivi hutaga mayai kwa wastani wa miaka mitatu na nusu lakini huweza kuwa zaidi. Mayai yanayotagwa katika kuta za utumbo mpaka na kibofu husababisha athari kubwa. Maambukizi yasiyotibiwa husababisha matatizo ya Ini, utumbo mpana na ugonjwa wa figo. Wakati mwingine mayai huingia katika uti wa mgongo au mara nyingine katika ubongo.
Jinsi ya kujizuia
Inasemekana hakuna chanjo iliyopatikana. Katika nchi ambazo ugonjwa huu upo, inadidi kujitahidi kuepuka maji ambayo si Safi na salama. Usidhani ya kuwa maji yoyote ni safi na salama katika sehemu zenye ugonjwa huu. Kingo za maziwa, mito na mabwawa ambapo maji yametuama na kuna uoto wa mimea, hizi ndizo sehemu za hatari.
Fukwe za bahari na fukwe zilizo na mawimbi si rahisi kuwa na konokono wa majini, hivyo hizi sehemu zinaweza kuwa salama. Viluwiluwi huweza kuishi kwa masaa 48 baada ya kutoka kwa konokono na huweza kusafiri mwendo mrefu, kwa sababu hii maeneo yenye maji katika sehemu zenye ugonjwa huu hayawezi kuwa salama kabisa.
Maziwa katika nchi ya Tanzania na Malawi yana vimelea vya kichocho, lakini fukwe nyingi karibu na mahoteli ya kitalii yana uoto mdogo wa mimea hivyo huwa ni sehemu ambazo si rahisi kupata ugonjwa huu.
Mabwawa ya kuogele ni salama kama yana dawa ya klorini(chlorine) na hakuna konokono wa majini.
Bahari ni salama
Maji ambayo yamatuama kwa siku tatu ni salama endapo hakuna konokono wa majini.Maji ya kuoga yanayochukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye mito na maziwa yanaweza kusabaisha maambukizi.
Namna ya kujikinga na kichocho
Kama uanapopalilia, vaa mabuti marefu ya mpira. Viluwiluwi hawa hufa haraka mara tu wanapokuwa nje ya maji na hawawezi kuepuka kifo. Nguo na ngozi zenye maji zikikaushwa kwa haraka husaidia kujikinga na maambukizo.
Dalili za maambukizi
Wasafiri wengi walioambukizwa huwa hawaonyeshi dalili yeyote ya ugonjwa huu
Kunakuwa na mwasho katika sehemu alipoingilia kimelea kama “mwasho wa muogeleaji”.Unapata homa baada ya wiki nne baada ya kutumia maji yaliyoambukizwa. Unapatwa na kikohozi kikavu ndiyo dalili ya hatua hii ya maambukizo. Kupungua kwa uzito na kujihisi kuchoka. Damu katika mkojo na haja kubwa kama ugonjwa umekomaa. Na pia kuvimba kwa miguu. Na muda wa kuambukizwa huchukua wiki nne (4) kwa mayai kuonekana katika choo na kuonekana kwenye mkojo. Lakini hata hivyo ikishajua tu umetumia maji yenye vimelea basi inabidi uchunguzi ufanyike miezi mitatu baada ya kutumia.
Tiba ya kichocho
Kichocho hutibiwa na madawa maalumu dhidi ya vimelea hivi ambazo hupatikana katika kliniki na hospitali yoyote ile iliyo karibu na makazi yako. Ni vizuri kupima mara kwa mara unapopatwa na mashaka ya kuambukizwa na kichocho hasa baada ya kutumia maji yenye vimelea vya kichoccho
5 comments:
Nimependa naona leo umemwaga darasa la kutosha.
nakutakia mwisho mzuri wa juma.
ndiyo kwani naona huu ni uganjwa hatari sana kwani mwili wote unatekenya kabisa
Hongera dada kwa kutukumbusha kuhusiana na hili gonjwa,maana sisi binadamu tuna hili suala la kujisahau.
darasa kali, na kuanzia leo siogi tena mtoni maana hapa nyasa ndiyo zetu wazee wa kazi kuchimba mabwawa
ndio maana nimeandika hii maana nakumbuka jinsi nilivyokuwa naogelea katika mabwawa kule Lundo mhm naogopa sana
Post a Comment