Tuesday, October 7, 2008

MAISHA YA NDOA

Kuna wasichana na wavulana wengi ambao wanaishi maisha ya ndoa bila kuyafurahia maisha kama inavyotakiwa. Kuna wengine wanaolewa/oa bila kufikiri kwa busara. Wanakuwa na haraka/hawapangi kwa utulivu wala makini. Na kuna wengine wengi wanaolewa/oa bila hiari kwa lazima yaani inakuwa ni lazima kufanya hivyo ili wanafamilia/ndugu wafurahi au pengine sio wafurahi isipokuwa kwa kuwatesa. Au kuwaonyesha ni nani anaweza kuyatawala maisha yake.Yaani hii yote inatokana na kuwa na hasira, pia kwa vile hakuna mtu mwingine anayemsaidia msichana au mvulana huyu ni nini aamue. Na baada ya ndioa, miaka inapita na akili zinaongezeka na ndipo anapogundua uamuzi aliouchukua haukuwa wa busara. Basi anaona hakuna maisha tena katika dunia hii. Sasa labda itakuwa tatizo kuamua tena uamuzi wa kuondoka/achana kwani sasa ameshakuwa mama/baba.Kwa hiyo wasichana na wavulana wote msioolewa/oa kaeni chini na tafakarini kwa busara, kweli huyu kijana/msichana ni ndiye mungu aliyenipangia kuishi naye miaka yote? Kweli ni mapenzi au kuna kitu nakikimbilia? Pia jaribuni kuwa wachumba kwa muda mrefu kwani hapo ndio mtaweza kujuana tabia na kuona kama kweli ni mapenzi ya kweli aula.

Jambo jingine ambalo limekuwa likinisumbua sana akili yangu, ni kwamba kwa nini? Wazazi wengi wanapenda sana kuingilia uamuzi wa watoto wao. Nina maama kwa nini mabinti na vijana wasichague wenyewe wenzi wao ambao wataishi nao maisha yao yote. Hivi ni nani ataishi na msichana au mvulana huyo? Wazazi, msichana au mvulana? Nimekuwa nikijiuliza hili swali miaka yote tangu nipate akili. Lakini bado sijapata jibu na bado naona katika jamii nyingi za kiafrika zinaendelea na tabia hiyo. Najue wengi watasema nimesahau utamaduni/mfumo wa maisha ya kiafrika. Eti wazazi wanasema sisi hatumtaki/ hatuutaki kijana/binti/ukoo huu. Na ukijaribu kuwaeleza haya ni maisha yangu na ni mimi ndiye ninayempenda kijana au binti huyo na ndiye nitakayeishi naye. Na hii imewafanya baadhi ya mabinti na vijana kuchukua uamuzi bila kuwaza kwa makini/busara au utulivu. Na matokeo yake yanakuwa hakuna raha katika ndoa, na mwisho huanza kuwaza mawazo mabaya na hata inaweza ikatokea hatari kubwa katika maisha.

2 comments:

MARKUS MPANGALA said...

kazi kwenu wanandoa na mnaotafakari kuhusu ndoa. jamani kuishi na mtu kazi kubwa sana. yaani kila siku unaamka kitandani unamuona mtu mmoja, aise kila sikua mmm mwenzangu ipo kazi hapo. kuoa siyo lelemama kazi mnayo. nafikiri suala la wazazi kuingilia lipo kwa kiasi kikubwa lakini linapswa kubadilika ingawa kwa namna fulani linaepusha mambo juu ya mambo. sijui bwana nisje nikashindwa kujieleza maana sina uzoefu wa ndoa miye. kwali mwavene mufiloli kutama mewawa kyani? ha ha ha ha mutu guvina na? pole

Fita Lutonja said...

Dada Yasinta unajua wazazi hawapaswi kuwachagulia watoto wao mchumba wa kuwaoa kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi na kutowatendea haki.