Leo nimekumbuka kweli mika ya tisini; wakati nilipokuwa nasoma Songea. Familia yangu walikuwa wanaishi kijiji kimoja kiitwacho Kingoli. Sijui nisemeje ili mnielewe kwani wengine msije mkasema ni kudeka tu. Haya semeni mtakavyo. Yaani nilikuwa natembea toka Kingoli mpaka Peramiho kwa miguu kulikuwa hakuna magari. Pale kijijini kulikuwa na lori moja tu lilikuwa linasafiri kwa wiki mara moja.
Baina ya Kingoli mpaka Peramiho kuna vijiji kama vitano hivi, hivi safari hiyo ilikuwa inachukua siku moja – mbili nilikuwa nalala katika kijiji kimoja kiitwacho Mgazini. Wakati mwingine sikuwa na maji wala chakula, na kama nilikuwa na chakula basi nilikuwa na (CHIMBONDI) = karanga zilizokaangwa na kutwangwa pamoja na chumvi. Au kama ni ule msimu wa maembe basi kuzitwanga kweli embe. Kwani wengine wana maisha ya raha, wengine ya kuteseka, ndugu zangu hivyo ndivyo maisha yalivyo.--
8 comments:
Lakini kuna ambao mtu mwingine utafikiri wana maisha ya raha kutokana na kuona labda wana pesa kitu ambacho ni tatizo kwangu na kwako, lakini hawataacha kukushangaza pale wajiuavyo kwa kudai hawana raha wala furaha.
Ni kweli kabisa kama huna raha wala furaha. Lakini una pesa ni sawa na sifuri.
@yasinta: Dada yangu alisomea Peramiho kwa masista kidogo kabla ya kwenda Songea girls.Kila nikisikia Peramiho huwa nakumbuka stori zake za jinsi wasichana wenziye walivyo kuwa wanakabwa usiku mabwenini na wachawi au majini. Nakumbuka badao peramiho ilivyokuwa imekaakaa Kijerumani enzi hizo. Hivi bado pazuri kama zamani?
Halafu Dada Yasinta nikiangalia picha zako siku hizi sidhani kama unaweza tena kutembea siku nzima halafu bila msosi:-)Lakini ndio Maisha!
Kaka Simon! Kama ulivyosema inabidi kuamini, ila kitu kama una imani basi kipo. Kuhusu kutembea usione hizo picha labda inawezekana maisha ni kuridhika au labda zimekuzwa tu. kutembea au kukimbia hunipiti kama au unabisha. Peramiho ndiyo bado pazuri au pazuri zaidi nilikuwa kule mwaka jana tu.
Ni vizuri kukumbuka yaliyopita. Historia ina utamu wake.
Yasinta hongera kwa kuwa mwanablogu machachari. Huwa naipitia kila siku japo siachi maoni saa nyingine.
Kazi yako ni nzuri. Hongera dada.
Asante sana kaka bwaya, kwa yote
Hongera dada kwa kukumbuka historia.
Baina ya Kingoli mpaka Peramiho kuna vijiji kama vitano hivi, hivi safari hiyo ilikuwa inachukua siku moja
black pakistani suit ,
black salwar suit ,
Post a Comment