Sunday, September 14, 2008

WANAWAKE UGHAIBUNI NA WANAWAKE AFRIKA

....... ...................... ............


Kama waswahili wasemavyo tembea uone, basi mimi nimeona:-


Kwani nakumbuka, pia najua ya kwamba wanawake Afrika ni wanyenyekevu mno kwa waume zao.

Lakini kwa uzoefu wangu hasa hapa Sweden baada ya kuishi miaka 14. Nimeona ni kinyume kabisa. Hapa ni wanawake ndio wanaamua/uamuzi ndani ya nyumba.


Bado sijajua nani nimwonee huruma Afrika au ughaibuni/Sweden.Nategemea sitaambukizwa na hali/tabia hii Mungu nisaidie. Na hii inachangia sana hapa Sweden kuwa na asilimia kubwa ya kupeana talaka

2 comments:

Anonymous said...

Kazi kwelikweli,
Hapa Canada naona mtoto akishafikisha miaka 10 yeye ndo anakuwa mtawala wa nyumba then anayefuatia ni mama then baba ndo wa mwisho na ole wako ujidai eti unataka talaka, maana shida utakayopata unaweza ukaambiwa hata nyumbani hapo usikanyage, imefikia mahali wanaume hawataki kabisa kuoa.
Naamini tungefuata misingi ya Bible bado ndoa zingeweza kuwa raha sana kwani kila mmoja angemtanguliza mwenzake na kumpa kile anastahili.
Lazarus 2nyi

Anonymous said...

bado napigani lugha kaka mbilinyi, kwanini unatumia lugha mbili katika kitendo kimoja?{natania}. ndiyo maana namwambia dadangu Yasinta kuwa mimi kuoa asahau kabisa bado nipo nipo kwanza ngoja nizeeke. Halafu kwanini upande wa waafrika umeweka picha ya mzungu wewe dada Yasinta? Hao ndiyo waafrika wenyewe au macho yangu mabovu- omba radhi{natania}